LangMedia Tz
09/09/2019
KWA MAHITAJI YA VIFARANGA BORA WA KUROILER KARIBU SUPER BRAND KEY STONE KUKU FARM BEI -@1800/=
PITA UTAJIPATIA VYUNGU VYA JOTO-@12000/=INCUBATORS,NIPPLE@3000/= NA VIFAA VYAKUTENGENEZEA INCUBATORS
TUPO ARUSHA NA BIDHAA INAKUFIKIA POPOTE ULIPO TANZANIA NZIMA KWA USALAMA NA UAMINIFU MKUBWA 0715 064 992 -/- 0754 064 992
05/02/2017
WADUDU NI CHAKULA BORA
Na Baraka Kaaya
Senene.
Wadudu ni chanzo kikubwa cha protini, mafuta mazuri kiafya, madini na kamba lishe. Aidha, wadudu wameelezwa kuwa ni rafiki wa mazingira na ni rahisi kuwafuga au kuwak**ata.
Inakadiriwa kuwa kiasi cha watu bilioni 2 duniani wanatumia wadudu k**a sehemu ya milo yao ya kila siku. Imeshauriwa watu kupendelea kula wadudu kutokana na ukweli kwamba protini inayopatikana kwenye wadudu hao ni bora zaidi kuliko ile inayopatikana kwenye nyama ya kuku, ng’ombe, nguruwe na samaki.
Mbali ya wadudu kuwa ni chanzo kikuu cha protini na mafuta mazuri k**a ya samaki (fish oil), lakini pia ni chanzo kizuri cha madini ya kashiamu (calcium), chuma (iron), seleniamu (selenium), zinki (zinc) na Vitamini B
WADUDU WA TANZANIA
Bwa Alex Bulugu alisema Kuna aina zaidi ya elfu tisa ya wadudu wanaoliwa sehemu mbalimbali duniani. Lakini kwa nchini Tanzania, kuna aina kuu mbili za wadudu ambao wanajulikana na kutumiwa k**a sehemu ya kitoweo katika familia nyingi nchini, hasa vijijini.
Aina hizo mbili maarufu nchini Tanzania ni Senene na Kumbikumbi, ambao hupatikana kwa wingi zaidi nyakati za masika sehemu za vijijini. Senene na Kumbikumbi ni miongoni mwa vyakula vyenye faida nyingi mwilini na ni vitamu pia.
Kutokana na kuwa na faida nyingi za kiafya mwilini, ndiyo maana wamekuwa wakiliwa tangu enzi na enzi na mababu zetu. Ingawa idadi kubwa ya wadudu hao wanaoliwa hupatikana kwa kuwak**ata kwenye makazi yao porini, lakini katika siku za hivi karibuni, mifumo ya kisasa ya kuwak**ata wadudu hao imebuniwa na hivyo kurahisisha ukusanyaji kwa idadi kubwa na kwa mara moja.
Kwa kuona umuhimu na faida za kiafya zinazoweza kupatikana kwa kula wadudu, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa nchi zote duniani kufuga wadudu hao kwa wingi kibiashara, shirika linaamini nchi nyingi zikitilia mkazo suala hili, zinaweza kupunguza tatizo la njaa kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo kuboresha afya za watu wengi.
Bila shaka hii ni habari njema na ya kutia moyo kwa watu ambao tayari wanafuga na kuvuna Senene kibiashara, k**a ambavyo tunavyoona wakiuzwa baadhi ya sehemu za mijini. Nitoe wito kwa watu wengine ambao hawajawahi kuonja Senene au Kumbikumbi kufanya hivyo, kwani siyo tu wana faida kiafya mwilini, bali ni watamu sana. (so delicious)!-GPL
04/02/2017
Fahamu kuhusu Ng'e na Hatari zake.
Na Baraka kaaya
Ng'e ni mdudu mweusi au kahawia mwenye
miguu minane na mkia mrefu wenye
sumu kali
Tafsiri ya majina haya kibaolojia
Kiingereza: scorpion
Kipoland: skorpion
Huduma ya kwanza kwa aliyeng'atwa na ng’e
Bw Elias Manase mtaluma Wa sayansi ya viumbe hai amesema nnge Ingawa wanaweza kusababisha maumivu makali, matukio mengi ya kuumwa na ng’e hayasababishi madhara makubwa au madhara ya muda mrefu.
Usiitikise sehemu iliyoumia na tumia barafu au maji baridi kupunguza maumivu.Usikate au kuchana wazi sehemu ya jeraha au kufunga sehemu hiyo kwa kutumia toniketi au bandeji. Joto halisaidii, lakini kutoitikisa sehemu ya jeraha husaidia. K**a unajua kuwa aina ya buibui au ng’e aliyemuuma ni hatari, au k**a baada ya kuuma kuna dalili za matatizo k**a vile maumivu ya tumbo, mwasho, kutokwa jasho, na shida katika kupumua, basi tafuta msaada wa kitabibu. Huenda kukawa na dawa dhidi ya sumu hiyo.
Kwa ajili ya matukio ya kunga’twa na ng’e hatari, unaweza kumpa majeruhi diazipamu kuzuia misuli kukak**aa na pia kumtuliza mgonjwa wakati mnafanya maandalizi ya kwenda hospitali au kituo cha afya.
Buibui na ng’e
Ingawa wanaweza kusababisha maumivu makali, matukio mengi ya kuumwa na buibui na ng’e hayasababishi madhara makubwa au madhara ya muda mrefu. Usiitikise sehemu iliyoumia na tumia barafu au maji baridi kupunguza maumivu.Usikate au kuchana wazi sehemu ya jeraha au kufunga sehemu hiyo kwa kutumia toniketi au bandeji. Joto halisaidii, lakini kutoitikisa sehemu ya jeraha husaidia. K**a unajua kuwa aina ya buibui au ng’e aliyemuuma ni hatari, au k**a baada ya kuuma kuna dalili za matatizo k**a vile maumivu ya tumbo, mwasho, kutokwa jasho, na shida katika kupumua, basi tafuta msaada wa kitabibu. Huenda kukawa na dawa dhidi ya sumu hiyo.
Kwa ajili ya matukio ya kunga’twa na buibui na ng’e hatari, unaweza kumpa majeruhi diazipamu kuzuia misuli kukak**aa na pia kumtuliza mgonjwa wakati mnafanya maandalizi ya kwenda hospitali au kituo cha afya.
31/01/2017
Fahamu zaidi Maisha ya Chura
Na Baraka Kaaya
Baada ya kufamu zaidi Maisha ya chura wa kihansi kwenye post ya Nyuma karibu tena upate kufahamu zaidi kuhusu aina zingine za vyura na Maisha lakini pia hadisi ya kukujenga kuhusu mdudu huyu.
Maisha ya chura huaanza k**a yai
lililotegwa kwenye maji pamoja na mayai maelfu. Hutoka kwa umbo la
ndubwi (pia: kiluwiluwi) ambayo ni
funzo la chura huendelea na kipindi cha kwanza cha maisha yake katika maji. Hupumua kwa yavuyavu na mwanzoni huku akiwa hana miguu bali mapezi k**a samaki na mkia . Viluwiluwi wengi wakiwa kwenye maji wanakula majani au mwani hata k**a baadaye k**a chura mzima wanakula wadudu wengine.
Baada ya muda kiluwiluwi hulaga miguu minne na mapafu . Utumbo unabadilika na kujiandaa kwa chakula kipya kinachopatikana kwenye nchi kavu. Umbo hufanana na chura mzima.
Kipindi hiki cha utoto kwenye maji hudumu kati ya wiki tatu hadi miaka miwili kutegemeana na spishi za chura. Mara nyingi ni k**a wiki 10 - 15.
Chura mzima kwenye nchi kavu
Akitoka kwenye maji chakula chake ni wadudu. Lakini chura wakubwa wameonekana pia kula
mamalia wadogo, samaki na chura wadogo zaidi. Spishi kadhaa wana ulimu wa kunata wanashika wadudu wanaopita haraka lakini wengine wanak**ata windo kwa kutumia mikono yao.
Bali na maelezo haya kuna pia spishi kadhaa wanaorudi kuishi katika maji lakini wanapumua kwa mapavu na wachache sana wanaendelea kula majani. Spishi kadhaa wanaendelea kuishi kwenye miti.
Chura wenyewe wanaliwa na ndege , samaki, nyoka na mamalia. Katika nchi kadhaa watu wanakula chura, kwa mfano Ufaransa, China na Ufilipino.
Kuna takriban spishi 5,600 za chura.
Familia za Afrika
Archaeobatrachia
Alytidae, Vyura ulimi-sahani
Mesobatrachia
Pelobatidae, Vyura miguu-sepeto
Pipidae, Vyura-kucha
Neobatrachia
Arthroleptidae, Vyura-filimbi
Brevicipitidae, Vyura kichwa-kifupi
Bufonidae, Vyura sugu
Dicroglossidae, Vyura ulimi-panda
Heleophrynidae, Vyura pepo
Hemisotidae, Vyura pua-sepeto
Hylidae, Vyura-miti
Hyperoliidae, Vyura-mafunjo
Mantellidae, Vyura bukini
Microhylidae, Vyura domo-jembamba
Petropedetidae, Vyura-vijito
Phrynobatrachidae, Vyura-madimbwi
Ptychadenidae, Vyura vigongo
Pyxicephalidae, Vyura dubwana na
vyura maridadi
Ranidae, Vyura sahihi
Rhacophoridae, Vyura-povu
Sooglossidae, Vyura wa Shelisheli
Pia K**a ilivyo kwa wadudu wengine tunajifunza mengi na kuyakinganiasha na maisha ya binadamu na hii hadithi maarufu ya CHURA.
Mwanasayansi toka ujerumani
Heinzmann , aligundua kuwa chura akiwekwa kwenye chombo tuseme sufuria yenye maji baridi , halafu maji hayo yakaanza kupashwa moto kidogo kidogo , basi chura huyo wala hatohangaika kutoka kwenye maji, na hatimaye kufa wakati maji hayo yatakapokuwa ya moto kweli kweli. Ingawaje kuna mabishano ya kisayansi kuhusu usahihi wa madai ya Heinzmann, leo utajifunza kitu kuhusu habari hii ya chura.
Kumbuka ukimweka chura kwenye maji ambayo tayari ni ya moto , atakurupuka haraka. Utafiti nilioleza hapo juu ni k**a utamweka kwa maji ya baridi.
Mara nyingi ili binadamu akubaliane kwa urahisi na mabadiliko, basi mabadiliko hayo ni lazima yafanyike kidogo kidogo k**a hiyo habari ya chura.
Jamii yetu inaporomoka kimaadili siku hadi siku, kiwango cha elimu kinashuka na hata ufanisi makazini ni ishu. Hata hivyo matatizo hayo ya mfumo wetu wa maisha hayajaanza leo, hayakuwa makubwa kiasi hiki kipindi kirefu kilichopita, ila yameendelea kukua kidogo kidogo k**a vile yale maji yanavyoongezwa joto ili kumuunguza chura. Hatukusikii wala hatuoni ni shida, tumebaki kulaumiana ila mbaya zaidi k**a vile yule chura, bado hatuchui hatua ya kujikwamua kwa haraka kwa kuwa ni k**a tumekwishajizoelea hali hii.
Bado unayo nafasi ya kuamka, na kubadili kile kinachokukera. Usikatishwe tamaa na mfumo mzima wa maisha ya jamii, mabadiliko ya kweli ya jamii hayategemei wote sisi kubadilika kwa wakati mmoja. Kila mmoja wetu akibadilika kidogo kidogo jamii itafika mbali.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Address
Arusha