The Same Qualities Foundation

The Same Qualities Foundation

Share

01/06/2026

Video inaonesha maduka yaliyopo katika eneo la EmaXesibeni huko Eastern Cape yakiwa tupu na mtaa ukiwa na upweke baada ya kufukuzwa kwa wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika wanaoishi nchini humo.

Photos from The Same Qualities Foundation's post 17/05/2026

I got over 50 reactions on my posts last week! Thanks everyone for your support! 🎉
We continue to build pre hospital in the city of Arusha and Tanzania at large

Photos from The Same Qualities Foundation's post 16/05/2026

TAWIRI YAREJESHA MATUMAINI KWA WANANCHI KWA KUDHIBITI TEMBO KISAYANSI.

Wananchi katika maeneo yenye migongano na Tembo wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali k**a mabomu baridi na njia nyingine nyingi katika kukabiliana na kadhia hiyo hapa nchini. Hata hivyo, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imetumia mbinu ya kuwafunga mikanda yenye visukuma mawimbi (GPS) Tembo viongozi katika juhudi za Wizara ya Maliasili na Utalii za kupunguza migongano hiyo

Mtafiti na Daktari wa wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Iddi Lipende amesema mikanda iliyofungwa itakuwa inatoa taarifa ya mienendo ya tembo na watakapokuwa wanaelekea kwenye makazi na mashamba ambapo askari wanyamapori waliopo kwenye vituo vya uthibiti wa Wanyamapori wakali na waaribifu(PAC) watapata taarifa mapema na kuwazuia mapema kabla hawajafanya madhara kwa wananchi.

Aidha, Afisa Wanyamapori wa Wilaya ya Meatu, Bwana Joseph Sikawa, ameishukuru serikali kwa kuiwezesha TAWIRI kufanikisha zoezi hili katika wilaya ya Meatu. Wilaya ya Meatu imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya uvamizi wa tembo mashambani ambapo
Makundi ya tembo yameonekana kuingia katika mashamba katika vijiji vya Mwanyahina, Mwajidalala, Mwanzagamba, Mbugayabanya, Mwamashimba, Mang’wina, Mwangudo, Mbushi, Shushumi, Mbuyuni, Sungu na Paji

Mwananchi kutoka Meatu pia ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo, akisema hapo awali walilazimika kulala mashambani kulinda mazao yao dhidi ya tembo, lakini sasa teknolojia hiyo itasaidia kuwafuatilia wanyama hao mapema na kuwazuia kabla hawajafika katika maeneo ya kilimo, alisema Godfrey Mabula.

Kwa upande wake, Afisa Uhifadhi daraja la kwanza Bw. Ayubu Fundi kutoka (TAWA) amesema wamekuwa wakifanya juhudi kubwa kuwarudisha tembo hifadhini. lakini wakati mwingine wamekuwa wakichelewa kuwafikia kutokana na wanyama hao kutokea maeneo mbalimbali ya hifadhi. "matumizi ya vifaa hivyo yatawezesha udhibiti wa haraka zaidi kabla ya tembo hao kuingia kwenye mashamba ya wananchi" amesema.

na teknolojia ni Uti wa Mgongo katika Utafiti na Uhifadhi Endelevu.

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


P. O BOX 11641
Arusha