Mwl. Daniel Piniel
HAPPY NEW YEAR 2024
05/12/2023
HAKUNA THAWABU KUTOA FEDHA MADHABAHUNI IKIWA NDUGU ZAKO NI WAHITAJI
Naomba Mnisamehe ikiwa kauli yangu ni kwazo!
Watu husema “Fedha hizi zafaa kumtolea Bwana kanisani (madhabahuni) ili nitimize sheria ya Bwana”
Watu hudhani tu kumtolea Mungu Sadaka ni kwa njia ya kwenda Kanisani na kutoa fedha za uwiano, michango ya maendeleo au Shukrani kwa Bwana. Hayo ni Mapokeo ya Kanisa kwa maana ya desturi inayorithiwa katika madhehebu. Sisemi ni mbaya kuwa na mapokeo lakini Nahitaji kukumbusha Neno la Bwana lisiachwe kwa sababu ya Mapokeo hayo.
Mapokeo huja kwa sababu ya kulishika Neno fulani lenye manufaa binafsi ya dhehebu au Kanisa na kiliacha Neno lenye manufaa kwa waliokusudiwa na Bwana.
“Lakini k**a mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka..”Mathayo 12:7
Rehema maana yake ni kuwa na moyo wa kusaidia wenye udhaifu na wahitaji kwa kutoa nguvu au uwezo wako kwa ajili yao. Hilo ndilo Neno la Bwana katika kumtolea Bwana.
Hebu fikiri, kutoa fedha kwaajili ya Maendeleo ya Mtaa wa Kanisa au Dhehebu kwa kutumia Neno la kusema “Mheshimu Bwana kwa Mali zako” au “Leteni zako kamili ghalani mwa Bwana”, Na katika kutoa huko hakuna rehema kwa waliokusudiwa.
Nini maana ya Maneno haya? “Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao...”
Hebu fikiri, Umetoa fedha nyingi na ahadi nyingi kwa ajili ya Shukrani kwa Bwana Kanisani au kwa ajili ya maendeleo ya Mtaa, huku unayo ndugu wengi wenyi uhitaji wa chakula na mavazi au wengine kuhitaji fedha kidogo kwa ajili ya matibabu. Au natamani kujua Je, ni dhehebu lako ndilo lenye uhitaji zaidi ya ndugu zako?
Je, mwadhani kumtolea Bwana ni kwa Sadaka za sheria za Mapokeo au kwa kuwa na Rehema? Na Lipi ndilo Neno la Bwana kati ya kutoa Sadaka na kutoa Rehema?
“Heri wenye Rehema maana hao watapata rehema”
Kumbuka habari za Kornelio “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, 2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.” Matendo 10:1-2.
Kumbuka habari za Tajiri “Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.”
Habari hizi ni za utoaji kwa Bwana lakini ikiwa kwa Rehema; kwa ajili ya hao waliokusudiwa katika Neno la Bwana na wala si katika Mapokeo. Kwa maana Kumpenda jirani yako ndio bora kuliko kutoa sadaka nyingi madhabahuni. K**a vile Kornelio alitoa sadaka nyingi kwa watu na kumcha Mungu na kumcha Mungu ndiyo bora kuliko Mapokeo.
“Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.” Mithali 19:17 “Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.” Mithali 21:13.
Mniwie radhi kwa kwazo lolote.. ila Naomba kila mmoja wetu kujali rehema kuliko sadaka. Ndugu zako ni wahitaji na wanahitaji rehema kwa kile wanachokihitaji. Maskini tunao sasa kwa mapenzi ya Mungu na Madhehebu tunayo kwa Mapokeo yetu. Tulijali lile la Bwana kuliko lile la Wanadamu.
🙏
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the place of worship
Telephone
Website
Address
Arusha
123