IFYT Tz

IFYT  Tz

Share

16/10/2017

K**A VIJANA TUNATAKIWA KUFIKIRIA

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

👉🏾Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

🙇🏽📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 🚙magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

👉🏾Wapo 🙇🏽📚wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

👉🏾Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
👇🏽
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

👉🏾Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

👉🏾Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

🙇🏽📚Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
👇🏾
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

👉🏾Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

✋🏾Huwezi kufika mbali kiuchumi k**a utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

�Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: K**a ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

🛣Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

😎Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

Vumilia tu na jiongeze...hata mimi sijawa tajiri bado...... But nakaza mwendo Bila kuangalia vipingamizi au ugumu wa safari...

29/01/2017

Leo hebu tujifunze kitu kupia ujumbe huu mfupi
*ASSET AND LIABILITY*

*Asset* ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

*Liability*ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri,hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.
Matajiri wote wananunua Assets,lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kua ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu k**a,nyumba,gari,simu,laptop, duka.
Ni sawa k**a tu hivyo vitu vinakuingizia pesa,lakini k**a havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba,k**a una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana,maana haikuingizii hata mia,badala yake inakutolea pesa,utalipa umeme,maji,ukarabati na malekebisho ya vitasa,taa,furniture n.k,hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini k**a nyumba umepangisha,hiyo ni Asset. Gari,k**a unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa,itahitaji mafuta,service,na k**a umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi,ila k**a ni la biashara hiyo ni Asset.
Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchart,hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia,maana siku umelifunga huingizi chochote,matumizi yoote unategemea dukani,badala ya duka kukupa faida,unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiliwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities k**a furniture, TV,radio,simu kubw,gari,fridge,nguo,viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine,mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao,badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara(Income) ukiongezeka,matumizi(Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa dalasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato(Income) na kupunguza upande wa matumizi(Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities,wananunua Luxuries k**a gari,tv ,sm kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida,hivyo faida ndio inanunua magari,nyumba,TV nnk, ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili,lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka.
K**a unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

*Wealth* is a person's ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today,how long could you survive?
Maana yake,k**a leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato,una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani??
Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.
Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities, na pia ujiulize are you Wealth or not?

09/05/2016

WARIOBA: KWA NINI WATU WENGINE WANABAKI MASKINI?

Sababu zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli mtupu;

1. Kushindwa kuamua haraka fursa zinapojitokeza kwao

2. Fursa kali Zikitokea wanaziona k**a ni uongo na utapeli wa mjini

3. Kung'ang'ania kuajiriwa hata k**a ajira hiyo hailipi

4. Kudhania unajua sana hivyo huoni jipya la kujifunza

5. Kukosa ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi huu au mwaka huu ntafanya hili au lile. Lakini mwaka unaisha hujaanza!!!

6. Kutokuwa na ndoto ya kiasi cha pesa unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka. Unataka shs ngapi kwa siku? Wiki? Mwezi? Mwaka? Kwa nini unataka kiasi hicho? Matumizi yako ya lazima ni yapi? Ya starehe zako ni yapi?

7. Kununua vitu vya bei kubwa sana na visivyo na tija yoyote katika kuongeza kipato chako.

8. Kuwaza kwamba maendeleo yanapatikana uzeeni na siyo ujanani? Eti kumiliki mamilioni ya pesa mpaka uwe mzee k**a Reginald Mengi vile.

9. Kufikiri eti huwezi kufanikiwa kuwa na fedha kuubwa mpaka uwe freemason au fisadi. Ujinga.

10. Kuwa na wategemezi kibao nyumbani kwako wakati kipato chenyewe kinatosha kula watu 2 tu kwa mwezi. Hatari!!

11. Kusubiri siku utakayopata pesa nyingi sana eti ndipo utafanya biashara hii au ile! Utasubiri sana.

12. Kutokuweka akiba yoyote kwa malengo ya maendeleo ya watoto na wajukuu zao.

13. Kufikiria kuwa kuna siku utapata msaada kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au washikaji zako. Utangoja sana.

14. Kubadilisha mshahara wako au kipato chako kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo wenu anakuomba pesa na wewe unampatia. Usimpe mtu samaki mfundishe kuvua samaki naye hatakuomba tena samaki. Usimpatie maziwa ndugu yako mfundishe kufuga ng'ombe wa maziwa.

Mpendwa mawazo yako na ndoto zako ndizo zita kutoa hapo ulipo.

25/04/2016

"ukishindwa kuwa na ndoto zako, na kuhakikisha zinatimia kuna watu watakuajiri uwasaidie kutimiza ndoto zao..."
""if you fail to have a dream to work on, someone will hire you to help build their dreams..""

Photos 20/04/2016

"unemployment is the rampant problem in Tz especially to youths who make more than 50% of national population..
we are youths we have to think the ways to fight this problem"
Lets Meet And Make a Move

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


TCA Street
Arusha
P.O.BOX296