Mokia Ole Naputu
12/04/2024
E.M Sokoine ni K**a Elia Mtishbi. Alichipuka K**a mmea jangwani, akalivusha taifa, akawapenda watu wake kuliko nafsi yake.
Mwandishi ni yuleyule shahidi upande wa utetezi Professor OleNaputu a.k.a Sokoine wa Pili
Leo imetimia miaka 40 Tangu aliyekuwa kiongozi mashuhuri, muadilifu na kipenzi cha wengi Mhe. Edward Moringe Sokoine alipoaga dunia kwa kile kilichodaiwa ni ajali ya gari katika eneo la wami dakawa mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Bungeni Dodoma kuelekea jijini Dar Es Salaam kwenye majukumu yake ya kitaifa.
Ajali ile ilikuwa pigo kubwa sana kwa taifa ambalo lilimuhitaji mtu wa kaliba yake kwa wakati ule kutokana na Hali mbaya ya kiuchumi huku vitendo vya ulanguzi na uhujumu uchumi vikianza kuota mizizi. Haya wengi wanayajua na kudhamini.
Leo Nataka tuzungumzie upande mwingine wa hayati Sokoine ambao si wengi sana wanaujua hasa jamii ya wafugaji. Licha ya mapenzi yake ya dhati kwa taifa, Hayati Sokoine alikuwa ni mtu aliyependa sana jamii yake ya Maasai akitambua fika kuwa cheo chake ni nyenzo muhimu ya kuinua jamii kielimu na kuimarisha mshik**ano.
Katika kufanikisha hili, Sokoine alianzisha program mbili muhimu sana. Moja ni kuanzisha, kupitisha na kusimamia sera ya serikali kwa wafugaji kwamba kwenye kila familia walau mtoto mmoja atolewe kwenda shule kusoma kwani enzi hizo wafugaji wengi waliishi porini na hawakujua maana na umuhimu wa Elimu. Sokoine alihakikisha viongozi wote wa mila popote walipo wanaupata Huo ujumbe na kusaidia kwenye utekelezaji na wengine wetu Leo ni matunda ya juhudi za Hayati E.M Sokoine.
Jambo lingine kubwa alilolifanya Sokoine ni kuhakikisha kwamba anatumia nafasi yake kuwakilisha wananchi na sio matakwa yake binafsi. Alihakikisha pia kwamba kunakuwepo mfumo maalum wa kijamii wa kumsimamia na kumwajibisha yeye endapo ataenda kinyume na masilahi ya jamii.
Enzi hizo kulikuwa na baraza maalum la uwakilishi Ndani ya jamii ya Kimasai lilijulikana k**a “Engurashi”. Lilikuwa ni baraza lenye wawakilishi watatu kutoka kanda zote za wilaya ya Maasai.
Wajumbe wa baraza hili walichaguliwa na wazee wa kila kanda kufuatana na uadilifu, busara na uwezo wao wa kumudu nafasi za uongozi. Majukumu ya baraza la Engurashi ni pamoja na kumchagua/kumpendekeza jina la kiongozi mkuu wa kijamii, kumsimamia kiongozi Huyo baada ya kuchaguliwa na kutoa maamuzi na mwongozo kwenye mambo muhimu ya kijamii.
Japo baraza hili lilikuwepo Kabla hata ya Sokoine kuwa kiongozi, alitumia sana Engurashi kupata busara za uongozi na kujua matakwa ya wananchi. Ilisemekana kwamba Hayati Sokoine aliwaomba wazee wa baraza wamuwekee muda wa yeye kutakiwa kukutana na baraza ambapo kila wakutanapo alitoa hesabu ya yale anayoyafanya katika kuisaidia jamii yake. Pia alitumia nafasi hiyo kusikiliza matakwa ya wananchi kupitia baraza la Engurashi na kuhakikisha kwamba anayafikisha serikalini na kuhakikisha utekelezaji unafanyika.
Huu utamaduni wa kuwajibika kwa baraza la juu kabisa la uongozi katika jamii, ulimsababisha Hayati Sokoine kupendwa sana na jamii ya Wamaasai lakini pia ulimsaidia yeye mwenyewe kuwa muajibikaji na mzalendo kwa jamii na taifa.
Huyo ndiye Hayati Edward Moringe Sokoine. Waziri mkuu pekee aliyejikana lakini historia imekataa kumkana. Alichagua umasikini na jina jema kuliko Mali nyingi na historia mbaya.
We will always remember you the true son of the land.
nambari moja upande wa utetezi
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Arusha
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 16:00 |
| Tuesday | 08:00 - 16:00 |
| Wednesday | 08:00 - 16:00 |
| Thursday | 08:00 - 16:00 |
| Friday | 08:00 - 16:00 |