Mr Meshacking
19/04/2026
: Mahak**a ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imewahukumu maofisa wawili wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Thadeus Mtui na Florian Kilango, kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni nane.
Watumishi hao walipokea fedha hizo kutoka kwa mfugaji Yuda Male kwa nyakati tofauti ili wasichukue hatua za kisheria baada ya kumkuta akilisha mifugo katika Hifadhi ya Msitu wa Chimala.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Daniel Mono, alieleza mahak**ani kuwa washtakiwa walichukua shilingi milioni mbili mnamo Novemba 2025 na kisha milioni sita nyingine Januari 2026.
Mfugaji huyo aliamua kutoa taarifa katika vyombo vya dola baada ya kuchoshwa na usumbufu wa maofisa hao licha ya kuwa alikuwa ameshatoa kiasi hicho kikubwa cha fedha k**a hongo ili aachiwe.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Irvan Msacky, mbali na kutoa adhabu ya faini, ameamuru washtakiwa hao kurejesha fedha zote milioni nane walizochukua kwa mlalamikaji.
Mahak**a imesisitiza kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa watumishi wa umma wanaokiuka dhamana ya kulinda maliasili za nchi na badala yake kujiingiza katika vitendo vya udhalimu na hujuma dhidi ya juhudi za serikali za kuhifadhi mazingira. Mr Meshacking Meshacking Raphael Mtanda
19/04/2026
Meli mbili za India, zimeshambuliwa na Jeshi la Iran wakati zikijaribu kupita katika mlango wa bahari wa Hormuz, mara baada ya Iran kutangaza kufunga njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.
Tukio hilo limethibitishwa na vyanzo vya India, huku zikielezwa kuwa meli hizo zilishambuliwa kwa risasi za onyo na baadhi kulazimika kurudi nyuma ili kujinusuru.
Hatua hiyo imekuja wakati Iran ikirejesha tena udhibiti mkali wa mlango huo, ikisema haitaruhusu meli kupita kutokana na mvutano unaoendelea na Marekani.
Ripoti zinaonyesha kuwa baadhi ya meli zilipokea maonyo kupitia redio zikizuiwa kuingia eneo hilo, na hata zingine zililazimika kubadili mwelekeo kutokana na hatari ya kushambuliwa.
Mlango wa Hormuz ni njia muhimu sana duniani, ambapo takribani asilimia 20 ya mafuta ya dunia hupitia hapo. Kufungwa au kuzuiwa kwa njia hiyo kuna athari kubwa kwa usafirishaji wa nishati na bei za mafuta kimataifa, jambo linalosababisha hofu katika masoko na sekta ya usafirishaji.
Wakati huo huo, juhudi za kidiplomasia zinaendelea ili kupunguza mvutano huo, huku kukiwa na mazungumzo yanayoweza kufanyika kati ya Iran na Marekani. Hata hivyo, hali bado ni tete na inabadilika haraka, huku hatari ya kuongezeka kwa mgogoro huo ikiendelea kuwepo. Meshacking Raphael Mtanda Mr Meshacking
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Arusha