Epak Capital

Epak Capital

Share

05/08/2024

Kisasi bora zaidi ni kutolipiza kisasi kabisa. Pona, songa mbele na usiwe k**a wale waliokuumiza.

25/07/2024

BINTI WA MAZIWA NA NDOO YA MAZIWA

Siku moja binti wa maziwa alikuwa akitembea njiani kijijini, akiwa amebeba ndoo ya maziwa kichwani. Alikuwa akitokea shambani kwake akienda kijijini kuuza maziwa aliyobeba. Wakati akiwa njiani, alianza kuota ndoto za mchana.

"Nitauza hii ndoo ya maziwa kijijini. Pesa nitakayoipata, nitaweza kununua kwa uchache angalao mayai mia tatu.
Kati ya hayo mayai mia tatu, kwa uchache mia mbili yataanguliwa na kukua hadi kuwa kuku. Nitauza sokoni kuku mia na hamsini kati ya hao mia mbili muda utakapowadia. Hamsini watakaobaki nitawatunza shambani ili watage mayai mengi zaidi.

Na nitakapoipata hii pesa nitanunua gauni zuri. Nitavaa gauni hili na kuhudhuria sherehe za Krismasi. Wanawake wote wadogo watanitamani sana na vijana wote watapenda kucheza nami muziki.
Lakini sitakuwa mwepesi. Nitatingisha kichwa na kusema hapana kwa kila mtu, hadi pale mwana mfalme mwenyewe atakaponiomba nicheze naye muziki."

Akiwa anayasema hayo, alitingisha kichwa. Mara ndoo ya maziwa ikapiga chini na yote kumwagika.

Fundisho: Usihesabu kuku wako kabla hawajaanguliwa.
Chanzo : Hadithi za Esopo

Asante kwa kusoma na kushea 🙏🙏🙏

25/07/2024

Haijalishi wewe ni mwema au mkarimu kiasi gani; Huwezi kumridhisha mtu asiyekuwa na shukurani.

20/07/2024

SENTENSI 8 ZITAKAZOKUZA UWEZO WAKO WA MAHUSIANO YA KIJAMII:

1. "Kutatua jambo haraka, kuwa muungwana kwa mtu anayehusika na mkali kwa tatizo lenyewe"

Unapokumbana na changamoto au migongano, chukua mtazamo unaojali hisia na maoni ya wengine na kuwa muelewa. Unapoteza nguvu kwa kumwia mkali mtu aliyekosea wakati jambo la msingi ni kutatua tatizo.

2. "Dhania kuwa kila mtu alitumwa kukufundisha kitu."

Tazama kila fursa ya kujadiliana jambo na wengine k**a fursa ya kukua na kujitambua zaidi. Mchukulie kila mtu unayekutana naye k**a mwalimu, ukitambua kuwa kila mtu ana mambo ya kukufundisha na mtizamo wa kutoa. Kuwa tayari kukubali kutokuelewana na wengine. Kuwa mdadisi.

3. "Kuwa na Vituo Unapoongea + Tazama Machoni = kujiamini."

Jenga tabia ya kuwa na vituo(pozi) kabla ya kuzungumza, hii itakupa muda wa kupanga mawazo yako na kuwa na uwasilishaji mahiri. Kutazama machoni hukuwezesha kuonesha kujiamini na kuwa mkweli.

4. "Jifunze Jinsi ya Kuwafanya Watu Wajisikie Kuwa Muhimu."

Wafanye watu wajisikie kuonekana kwa kuwapa usikivu wa kweli na uwepo wako. Hakikisha wanajisikia kuwa wamesikilizwa kwa kuwasikiliza na kuuliza maswali ya kutaka kuelewa zaidi. Kuwa na bidii ya kukumbuka taarifa za muhimu za maisha yao, mambo wanayopenda na uzoefu wao.

5. "Sauti Bora Kabisa kwa Mtu ni Ile ya Jina Lake, Hivyo Likumbuke."

Kukumbuka na kutumia jina la mtu huashiria heshima, utambuzi, na uthibitisho ambao hutengeneza hali ya kuheshimiana na kuthaminiana.
6. "Kuwa na nia njema/chanya kabla ya kutoa mrejesho."

Kabla ya kutoa mrejesho chanya wenye manufaa, ni muhimu kuhakikisha kuwa watu wengine wanajisikia kuwa unawajali na unajali mafanikio yao ya muda mrefu. Hii husaidia kuonesha nia chanya.

7. "Sifia Hadharani. Kosoa faragha."

Kutambua hadharani hujenga utamaduni wa kuthamini na kuwatambua wengine. Lakini kwa kutoa mrejesho chanya unaojenga kwa faragha, kwa heshima huunda mazingira yaliyo salama kwaajili ya majadiliano na kukua bila kuhofia kuhukumiwa na kudhalilishwa.

8. "Mategemeo ambayo hayajaelezwa ni shina/chanzo cha chuki."

Jitahidi kuelezea matarajio yako kwa namna inayoeleweka na kwa heshima la sivyo tegemea kutoelewana, chuki, na mfarakano kwenye mahusiano.

Asante kwa kusoma na kushea 🙏🙏🙏

19/07/2024

Simtakii yeyote mabaya, lakini mtu huvuna kile anachopanda katika maisha. Huwezi kuwatendea watu k**a uchafu na ukaishi maisha yenye furaha.

Want your business to be the top-listed Finance Company in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


NSSF Mafao House, 7th Floor , Old Moshi-Arusha Road
Arusha

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00