House Of Prayer Ministries Int

House Of Prayer Ministries Int

Share

18/05/2026

📍Ibada ya Shukrani tunapohitimisha Mfungo wa siku 14 ni kesho saa kumi jioni.Andaa Sadaka yako ya Shukurani. 📍

19/03/2026

❗️RATIBA YA IBADA ZA MAOMBI NA MAOMBEZI ( House Of Prayer Ministries Int)❗️

1)LISAA LIMOJA LA MAOMBI

-Wiki ijayo kwanzia Jumatatu ya Tarehe 23 hadi Jumapili Tarehe 29.Tutakutana kila Siku jioni kwanzia Kumi na Moja Jioni hadi kumi na mbili Jioni.

MAELEKEZO YA MAOMBI

-Kumshukuru Mungu kwa Kumaliza ROBO MWAKA WA 2026,Na kuombea ROBO INGINE IJAYO YA MIEZI MITATU 2026.

-Njoo na Mipango yako ya mwaka 2026 uliyoiandika Januari wakati mwaka unaanza ulomwomba Mungu itimie Mwaka huu 2026.ITAOMBEWA.

2) TUTAKUWA NA SEMINA YA PASAKA.

-Itaanza tarehe 3-7.Tutakutana kila Siku Madhabahuni kwanzia Saa Tisa na nusu Mchana na kuendelea.

-Zitakuwa ni Siku za KUHUISHWA..Neno,Maombi,Miongozo ya Ki-Ungu,na majibu ya maswali na utatuzi wa kila changamoto ya Kiroho unayopitia.WAGONJWA NA WENYE SHIDA MBALI MBALI WATAOMBEWA.

📍KUMBUKA NI MOSHI - KILIMANJARO || KIBORILONI || NYUMA YA SEKONDARI YA KIBORILONI.📍

N:B.ZINGATIA MUDA WA IBADA.

(Waebrania 10:25)

25.wala tusiache kukusanyika pamoja, k**a ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa imekaribia.

HOUSE OF PRAYER MINISTRIES INT.
©️Apostle Emmanuel Malisa. || 📞+255 743 010 082

26/01/2026

❗️IJUMAA HII || MOSHI KILIMANJARO || NYUMA YA SEKONDARI KIBORILONI || KWANZIA SAA NANE MCHANA NA KUENDELEA.❗️

22/01/2026

❗️DAY 04 OF 12 DAYS OF PRAYER AND FASTING | SIKU YA 04 MFUNGO SIKU 12❗️

(2 Nyakati 20:15)

"BWANA awaambia hivi, Msiogope wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu."

1.Mungu atakupigania mwenyewe mwaka huu kwa jina la Yesu...!

2.Haijalishi idadi ya walio kinyume chako, Mkono wake ni mkuu sana na atajidhuhirisha kwako k**a jemedari na komando wa vita kwa yeyote atayesimama kukushambulia na kutaka kukudhuru mwaka huu, kwa jina la Yesu...!

3.Pamoja na kwamba watajaribu kukurushia mishale yao ya uovu na uharibifu; kwa sababu ya Mungu kuwa upande wetu, mishale yao haitatufikia kwa jina la Yesu.

4.Mungu atapigania familia yako mwaka huu...
-Mungu atapigania ndoa yako mwaka huu...
-Mungu atapigania mahusiano yako mwaka huu....
-Mungu atawapigania watoto wako mwaka huu kwa jina la Yesu...
-Mungu atapigania biashara na kazi yako mwaka huu...
-Mungu atapigania mifugo na mashamba yako mwaka huu...
-Mungu atapigania masomo na taaluma yako mwaka huu....

-Yeye aliyekuita kumtumikia,Atapigania na kutetea nafasi yako ya wito, na hakuna atakayekudhuru wala kuchukua nafasi yako kwa jina la Yesu.

-Mwamini Mungu, tenga muda wako kufuatisha maombi haya kwa imani.

📍Kumbuka, maombi ya mwenye haki yafaa sana akiomba kwa bidii na kwa imani.
Yesu anakupenda sana...

Shalom 🙏!

NB:
K**a Hujafunga Anza leo Kilele cha maombi haya ni tarehe 30|01|26 SIKU YA IJUMAA.Na Tutakuwa na KONGAMANO Kubwa la KUANZA MWAKA NA BWANA KWANZIA SAA NANE MCHANA.Anza Kujiandaa Kuhudhuria.

Apostle Emmanuel Malisa
House Of Prayer Ministries Int
0743010082

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Arusha
23101