GADI TV
Baada ya kuwepo kwa madai kuwa kuna wanafunzi wawili wakike wanaosoma shule ya msingi wanauzwa kwa siri kingono na mwanamke mmoja aliyeamua kuwafungia ndani ya chumba chake katika kata ya Baraa Jijini Arusha, Binti mmoja ambaye tunampa jina la Chausiku, ameibuka na kueleza jinsi mwanamke huyo alivyokuwa akiwatafuta wanaume kwa ajili vitendo hivyo Jijini humo.
Binti huyo akizungumza na waandishi wa habari, mbali na kusimulia mbinu anazotumia mwanamke huyo, amedai kuwa amenusurika kuingizwa kwenye biashara hiyo baada ya kutafutiwa mwaname asiyemjua huku akitakiwa kwenda kundishiriki naye tendo hilo la kingono.
Ikumbukwe inaelezwa kuwa baada ya tukio hilo kubainika na kuzua taharuki kwa wananchi, uongozi wa eneo husika walimchukua mwanamke huyo na kisha kumpeleka mikononi mwa jeshi la polisi Jijini humo.
Wanafunzi wawili wa shule ya msingi waliokuwa wanatafutwa na wazazi wao baada ya kutokuonekana nyumbani kwao kwa takribani siku nne katika kata ya Baraa Jijini Arusha, hatimaye wamepatikana, huku ikidaiwa kuwa wamekutwa kwenye chumba cha mwanamke mmoja wakiwa wanatumikishwa kingono na wanaume tofauti tofauti Jijini humo.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limebainika, Mei 31, 2026, baada ya ndugu wa mmoja wa watoto hao kufika anapoishi mwanamke huyo anayefahamika kwa jina moja la Linnah, kwa lengo lakumweleza kuhusu upotevu wa watoto hao, k**a iwapo amewaona popote, lakini ghafla baada ya mlango kufunguliwa ndugu huyo aliwaona watoto hao wakiwa ndani ya chumba hicho.
Kufuatia kuwepo kwa kampeni ya kuchanja chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa inayoendeshwa na shirika la Mbwa wa Afrika Jijini la Arusha, hatimaye wananchi wamenufaika na zoezi hilo na kueleza kuwa idadi ya vifo vya binadamu ambavyo vilikuwa vinasababishwa na kuumwa na mbwa mwenye kichaa vitapungua.
Inakadiriwa kuwa, kila mwaka hapa nchini Tanzania, watu 1500 huwa wanapoteza maisha kutokana na kuumwa na mbwa mwenye changamoto hiyo.
Katika zoezi hilo ambalo limetolewa siku za mapumziko (Weekend), Mei 30, 2026 na Mei 31, 2026, linatarajiwa kutolewa tena June 07, hadi 08, 2026, Jijini humo.
Baada ya kukadiriwa kuwa, watu 1500 huwa wanapoteza maisha kila mwaka Nchini, kutokana na kuugua kichaa cha mbwa, hatimaye Uongozi wa hospitali ya Mbwa wa Afrika, umekuja na kampeni ya kuchanja chanjo ya ugonjwa huo kwa mbwa wote wa mitaa katika Jiji la Arusha, bila malipo, ikiwa nisehemu yakupunguza idadi ya vifo hivyo.
Uongozi huo ukizungumza na GADI TV Mei 28, 2026, umesema kuwa kampeni hiyo imekuja ikiwa sehemu ya mikakati ya kuhakikisha kuwa kila mbwa aliyepo kwenye mtaa anachanjwa ili kuepukana na ugonjwa huo hatari unaoweza kuambukizwa binadamu.
Aidha, inaelezwa kuwa chanjo hiyo itaanza kutolewa kuanzia Mei 30, 2026 kwenye vituo maalum vilivyotengwa kila kata ndani ya jiji hilo, k**a ambavyo inaonekana katika kipeperushi hiki, huku siku ya juma mosi na juma pili kwa kila wiki, ikiwa ndio siku zilizotengwa kwa ajili ya zoezi hilo.
Kadhalika, Uongozi huo umesema kuwa utendaji kazi wa hospitali hiyo, ni pamoja na kutibu mbwa koko wa mitaani ambao wamekuwa wakipata majeraha kutokana na kugongwa na magari barabarani, ambapo wakati mwingine baadhi ya mbwa hulazimika kulazwa wodini na baadae kuruhusiwa baada ya kupona.
Hata hivyo, uongozi huo unaeleza kuwa, hulazimika kupita mitaani nakuwakusanya mbwa wenye changamoto mbalimbali nakufikisha hospitalini hapo, ambapo wengine hutibiwa kwa kufanyiwa upasuaji, baada ya kufanyiwa vipimo kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Arusha