Arusha One Fm 101.7
Moscow, Urusi
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitoa shahada ya heshima ya uzamivu aliyotunukiwa nchini Urusi kwa wanafunzi, wazazi na walimu wanaopambana kuboresha maendeleo ya nchi kwa kutumia elimu.
Akizungumza mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo ya honoris causa, Rais Samia amesema ameipokea tuzo hiyo kwa unyenyekevu mkubwa lakini anaamini ni kwa niaba ya wengi wengine.
kutokana na uongozi usio kifani na mchango wake kwa maendeleo ya taifa lake.
Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN) cha Patrick Lumumba kimempa Rais Samia heshima hiyo kwa sababu ya uongozi uliotukuka na jitihada zake za kuiletea Tanzania maendeleo.
Nilipopata taarifa ya kupewa hadhi hii, niliona kwamba hii heshima si yangu pekee bali ni kwa wale wote ambao elimu ina maana kwao. Kwa walimu wanaofundisha kote, kwa wanafunzi want guys maarifa na kwa wazazi wanaopambana kusomesha watoto wao.
“ Jina la chuo hiki, likichukua jina la mmoja wa viongozi wanamapinduzi wa Afrika la Patrice Lumumba ni kielelezo cha ushahidi wa uhusiano unaojali ukombozi, utu na umoja wa kweli,” alisema.
RUDN ni miongoni mwa vyuo mashuhuri duniani – kikijipatia sifa kutokana na kusomesha kada ya wasomi wa miaka ya mwanzoni ya Uhuru barani Afrika, Asia na Amerika ya Kusini na kujulikana kwa jina la Patrice Lumumba.
Shahada hiyo ya heshima ya RUDN ni ya nane kwa Rais Samia tangu aingie madarakani mwaka 2021.
Moscow, Urusi
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amesifu mchango wa Chuo Kikuu cha Urafiki cha Watu wa Urusi (RUDN) katika ukombozi wa nchi za Afrika akisema kimesadifu maono ya viongozi wa zama za ukombozi wa Bara la Afrika.
Rais Samia ameyasema hayo jijini Moscow, Urusi wakati wa tukio la kutunukiwa kwake Shahada ya Heshima ya Uzamivu (Honoris Causa) na chuo hicho kutokana na uongozi uliotukuka na mchango wake katika maendeleo ya taifa.
Akizungumza mara baada ya kupewa heshima hiyo, Rais Samia alisema amepokea shahada hiyo kwa unyenyekevu mkubwa ukizingatia historia kubwa ya chuo hicho katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.
“Jina la Patrice Lumumba ambalo chuo hiki kilipewa kilisadifu jukumu kubwa ambalo mwanamapinduzi huyo wa Afrika na viongozi wenzake wa Afrika waliona k**a wajibu mkubwa wa uongozi.
“Kwamba elimu inatakiwa isiwe tu kuingia darasani bali ni mlango wa ukombozi, utu, maendeleo na uhusiano wa kuheshimiana. Historia ya chuo hicho imesadifu maono yao na kwa hakika heshima waliyonipa ni kubwa” alisema.
RUDN imekuwa na mahusiano ya muda mrefu na Tanzania, kikiwa kimesomesha zaidi ya Watanzania 1,100 tangu kianzishwe mwaka 1960 iliyopita na sasa wanafunzi wa Kitanzania 72 wanapata mafunzo katika ngazi mbalimbali chuoni hapo.
Rais Samia anakuwa Rais wa karibuni zaidi kupewa heshima hiyo na chuo hicho, huku marais wengine sita wakiwa wamewahi kupewa tuzo hiyo. Baadhi ya marais hao ni Sam Nujoma wa Namibia, Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Olesegun Obasanjo wa Nigeria.
Vyuo vikuu vingine saba ambavyo vimewahi kumtunukia Rais Samia shahada za namna hiyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Jawahral Nehru nchini India, Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki, Nasarawa nchini Nigeria, Chuo Kikuu cha Anga cha Korea Kusini, Chuo Kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Rais Samia yuko nchini Urusi katika ziara ya kitaifa iliyoanza jana na itahitimishwa kesho baada ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi wa St. Peterburg nchini hapa.
CHUO Kikuu mashuhuri nchini Urusi leo kimemtunukia shahada ya heshima ya Uzamivu (honoris causa) Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na uongozi usio kifani na mchango wake kwa maendeleo ya taifa lake.
Chuo hicho kinachojulikana kwa jina la Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN) ni miongoni mwa vyuo mashuhuri duniani – kikijipatia sifa kutokana na kusomesha kada ya wasomi wa miaka ya mwanzoni ya Uhuru barani Afrika, Asia na Amerika ya Kusini na kujulikana kwa jina la Patrice Lumumba.
Akipokea shahada hiyo ya heshima – ya nane tangu aingie madarakani, Rais Samia alisema amepokea tuzo hiyo kwa unyenyekevu mkubwa na haichukulii k**a yake binafsi.
“Nilipopata taarifa ya kupewa hadhi hii, niliona kwamba hii heshima si yangu pekee bali ni kwa wale wote ambao elimu ina maana kwao. Kwa walimu wanaofundisha kote, kwa wanafunzi want guys maarifa na kwa wazazi wanaopambana kusomesha watoto wao.
“ Jina la chuo hiki, likichukua jina la mmoja wa viongozi wanamapinduzi wa Afrika la Patrice Lumumba ni kielelezo cha ushahidi wa uhusiano unaojali ukombozi, utu na umoja wa kweli,” alisema.
Rais Samia alitumia hotuba yake ya kupokea heshima hiyo kwa kueleza kuhusu umuhimu wa elimu akisema imebadili maisha ya watu na mataifa mbalimbali.
“Hakuna taifa linalotaka kuachwa nyuma katika dunia ya sasa yenye mabadiliko makubwa katika maeneo k**a vile akili mnemba na sayansi za mashine. Jambo kubwa kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla si kwamba tuingie kwenye ushindani au la bali ni namna gani tutaingia kwenye ushirikiano na kufaidika na mabadiliko haya,” alisema.
Tukio hilo lilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Sayansi na Elimu ya Juu wa Urusi, Konstantin Mogilevsky, ambaye katika hotuba yake alisema Rais Samia ametoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa elimu nchini kwake katika kipindi cha miaka yake sita madarakani.
RUDN imekuwa na mahusiano ya muda mrefu na Tanzania, kikiwa kimesomesha zaidi ya Watanzania 1,100 tangu kianzishwe mwaka 1960 iliyopita na sasa wanafunzi wa Kitanzania 72 wanapata mafunzo katika ngazi mbalimbali chuoni hapo.
Rais Samia anakuwa Rais wa karibuni zaidi kupewa heshima hiyo na chuo hicho, huku marais wengine sita wakiwa wamewahi kupewa tuzo hiyo. Baadhi ya marais hao ni Sam Nujoma wa Namibia, Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Olesegun Obasanjo wa Nigeria.
Vyuo vikuu vingine saba ambavyo vimewahi kumtunukia Rais Samia shahada za namna hiyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Jawahral Nehru nchini India, Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki, Nasarawa nchini Nigeria, Chuo Kikuu cha Anga cha Korea Kusini, Chuo Kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Rais Samia yuko nchini Urusi katika ziara ya kitaifa iliyoanza jana na itahitimishwa kesho baada ya kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi wa St. Peterburg nchini hapa.
03/06/2026
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema Urusi itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania kwa kuongeza fursa za kiuchumi na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, akisisitiza kuwa uhusiano huo unaendelea kukua kwa kasi na una mustakabali mzuri zaidi.
Putin amesema hayo wakati ambao biashara kati ya Urusi na Tanzania imeongezeka kwa takribani asilimia 20 hadi 25 mwaka 2025, na kwamba bado kuna nafasi kubwa ya kupanua zaidi sekta ya biashara kupitia maeneo muhimu k**a nishati, usafirishaji, afya, elimu na utafiti wa kisayansi.
Akizungumza wakati wa mazungumzo na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu yw Kremlin, Putin amesema kuwa mwaka huu una umuhimu wa kihistoria kwa kuwa nchi hizo mbili zinasherehekea miaka 65 ya uhusiano wa kidiplomasia, akieleza pia furaha yake kuona Rais Samia akichagua Urusi kuwa nchi ya kwanza kufanya ziara ya kikazi baada ya uapisho wa uongozi wake kipindi cha pili.
Aidha, Putin amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo umeendelea kuimarika katika sekta mbalimbali za maendeleo, hususan nishati, miundombinu ya usafirishaji, afya, elimu na utafiti, ambazo zinaweza kuongeza manufaa kwa pande zote mbili.
Katika hitimisho, amesema Urusi inaendelea kuona Tanzania k**a mshirika muhimu wa kimkakati katika majukwaa ya kimataifa, na akatarajia ushirikiano zaidi kuimarika kupitia mikutano ijayo ikiwemo Jukwaa la Uchumi la St Petersburg na Mkutano wa Tatu wa Urusi na Afrika.
Ziara ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nchini Urusi, inatajwa kufungua fursa ya uwekezaji katika nishati ya nyuklia nchini, hasa ukizingatia mataifa mengi duniani yanaelekea kutumia vyanzo vya nishati mbadala badala ya mafuta pekee.
Dkt Samia, anakuwa mkuu wa nchi wa pili wa Tanzania kufanya ziara nchini Urusi, baada ya miaka 57 tangu Rais wa kwanza hayati Mwalimu Julius Nyerere, afanye ziara katika Taifa hilo mwaka 1969.
Katika ziara hiyo, Dkt Samia ameingia Ikulu ya Urusi ya Kremel na kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi na mwenyeji wake, Rais wa Taifa hilo, Vradmir Putin.
Hayo yameelezwa leo, Jumatano Juni 3, 2026 na Mchambuzi wa Siasa na Diplomasia, Paternus Niyegira, alipozungumza katika kipindi maalumu kilichorushwa na Televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
“Matukio ya hivi karibuni ulimwenguni, yanaonyesha mataifa ya Afrika yamefungua macho zaidi kwamba yanahitaji kuwekeza kwenye vyanzo vya nishati mbadala tofauti na mafuta.
“Tanzania ilishaanza kuzungumza habari za nishati ya nyuklia, sasa kwa Urusi ni muhimu kufahamu kwamba shirika la nyuklia la Urusi ni kubwa sana. Hivyo kuna fursa ya uwekezaji katika teknolojia, tafiti na elimu kupitia Urusi,” amesema.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokutana na Rais wa Urusi katika Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow, Urusi leo Jumatano Juni 03, 2026.
Dk. Samia yuko nchini Urusi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Putin, katika ziara inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi pamoja na kukuza ushirikiano katika sekta za uwekezaji na biashara.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Arusha