AFro-feeds
08/07/2025
UNAFAHAMU HILI
“Mfugaji anayejaribu kila kitu hupata matokeo madogo. Lakini Mfugaji anayejikita kwenye eneo moja, hujenga msingi wa biashara ya kweli.”
Chukua hatua hii leo
1. Andika aina ya kuku au bidhaa unayopenda zaidi
2. Tambua ni ipi ina soko rahisi kwako.
3. Jikite kwa miezi 3 – kisha panua taratibu.
📞 TAFUTA WATEJA KABLA YA KUVUNA
Usiwaze “nitauza nikifika wiki ya 8”.
Tumia muda wa kuku kukua kutafuta wateja kupitia simu, status, au kwa kutembelea maeneo ya soko/mapishi.
Weka oda mapema:
Mfano: “Naandaa broiler 50 kwa wiki ijayo, unahitaji wangapi?”
Toa Huduma ya Kusafirisha (Delivery)
Wateja wengi wako tayari kununua kuku k**a wakiletwa nyumbani/kazini.
Weka Uaminifu – Uwe Mkweli kwa Wateja
Usidanganye kuhusu uzito, afya ya kuku, au muda wa kupeleka.
Ukiaminika, wateja watakuletea wengine bila hata kuuliza.
🤝 Shirikiana na Maeneo ya Mahitaji
Pata mawasiliano na mahoteli, migahawa, shule, caterers, au wauzaji wa samaki/supu.
Wauzie kwa bei ya jumla au mkataba wa mara kwa mara.
FugaKitaalamu
**aKuku
28/06/2025
📝 ULISHAJI SAHIHI WA KUKU WA BROILER 🐥🍽️
Ufugaji wa kuku wa broiler unahitaji lishe bora yenye protini ya kutosha kwa kila hatua ya ukuaji—kuanzia chakula cha "starter" (wiki ya 1–4, protini 22–24%) hadi "finisher" (wiki ya 5 na kuendelea, protini 18–20%). Lishe hiyo hujumuisha mahindi, pumba za soya, madini, vitamini na viongeza kulingana na mahitaji ya kuku.
Kuku wa broiler hulishwa muda wote (free choice) na wanapaswa kupewa maji safi kila wakati.
Mwanga wa masaa 24 hutolewa wiki ya kwanza kusaidia vifaranga kula na kuzoea mazingira, kisha hupunguzwa hadi masaa 18 ya mwanga na 6 ya giza kila siku.
Pia, makazi yao yanapaswa kuwa safi, yasiyo na baridi kali, na yenye nafasi ya kutosha ili kuhakikisha ukuaji bora na afya njema.
20/05/2025
Je, wajua kwamba maganda ya mihogo ni mbadala mzuri wa chakula cha mifugo, yakiwa na nishati karibu sawa na mahindi? Yakikaushwa vizuri, hufaa kwa kulisha ng’ombe, mbuzi, nguruwe na hata kuku.
Majani ya muhogo yana protini nyingi na ni nyongeza bora ya lishe, huku mizizi ya muhogo iliyokaushwa (cassava chips) ikiwa chanzo kizuri cha wanga kwa mifugo.
Je, unahitaji mafunzo ya kuandaa lishe ya mifugo kwa kutumia muhogo kwa usahihi?
04/05/2025
Sababu 3 Kwanini Kuku Hukonda Hata K**a Unawapa Chakula Kingi
1. Chakula hakina virutubisho sahihi – Si chakula kingi huleta matokeo, bali mchanganyiko sahihi wa protini, madini, na vitamini.
2. Maradhi ya ndani (internal parasites) – Minyoo na coccidiosis huiba virutubisho kabla havijafika kwenye damu ya kuku. Hakikisha unafanya deworming na coccidiostat kwa ratiba.
3. Msongo wa mawazo (stress) – Kelele, joto kali, au msongamano hupunguza hamu ya kula na ukuaji wa kuku. Hakikisha banda ni tulivu, safi na lenye nafasi ya kutosha.
Unahitaji maelezo zaidi kuhusu kila moja?
Jiunge:https://chat.whatsapp.com/LLr2TX58soe4EVVEWiOeNJ
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the practice
Telephone
Website
Address
Arusha
0000