Maasai Channel

Maasai Channel

Share

Photos from Maasai Channel's post 25/05/2026

Bonanza la madiwani kati ya wilaya za Longido na Monduli limefanyika katika viwanja vya
Polisi Longido, ambapo timu ya Monduli iliibuka na ushindi wa goli 1-0 katika mchezo wa
mpira wa miguu uliokuwa na ushindani mkubwa.

Bonanza hilo lilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa serikali pamoja na wananchi waliojitokeza kushuhudia mchezo huo wa kirafiki
na kuimarisha mshikamano kati ya wilaya hizo mbili.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Mkuu wa Wilaya ya Longido Salum Kalli alisema kuwa
michezo ni njia muhimu ya kuwakutanisha viongozi na wananchi huku ikisaidia kujenga afya na
mshikamano. Alisema, “Ni jambo zuri kukutana kimichezo ili kufurahi pamoja na kujijenga
kiafya kwani muda mwingi mnakuwa mkitekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido Thomas Ngobei alisema mchezo
ulikuwa mgumu lakini wanaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayofanyika
Monduli.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Kisioki Moitiko alieleza furaha yake
kwa ushindi walioupata na kuwakaribisha Longido kwenda Monduli kwa mchezo wa marudiano
huku akiahidi maandalizi makubwa zaidi.

11/05/2026

ILARIKOK LE MAA 💪

11/05/2026

Orbungei Steven Kiruswa - Namayiani Kashingo

Want your business to be the top-listed Media Company in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Longido
Arusha
23501