JAMII Helper media
01/05/2026
JAMII HELPER recognizes You 🤞🤞🤞
JODIC YATUNUKIWA CHETI CHA SHUKRANI KUTOKA JAMII HELPER
Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali (JODIC) cha Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kimetunukiwa cheti cha Shukrani kutoka kwa taasisi ya “Jamii Helper” ikiwa ni katika kutambua mchango wa kituo hicho kwa kuwezesha kuanzishwa kwa taasisi hio.
Akizungumza wakati wa kukabidhi cheti hicho Bw. Kukwaja Kilaja, Mwenyekitii wa taasisi hio alisema “ Tumeamua kuja kukabidhi cheti hiki cha shukrani kwa uongozi wa Chuo kupitia JODIC kwa kutulea kipindi ni wanafunzi na kutuwezesha kuanzisha taasisi yetu ambayo imejikita katika kusaidia jamii”.
Naye Bw. Mejoel Kirika, Meneja wa kituo cha JODIC alikuwa na haya ya kusema “Tumefurahi kuona wanafunzi tuliopewa kazi ya kuwalea wanafanikiwa, na leo wamerudi kuonesha matunda ya kazi waliyoifanya wakati walipokuwa wanafunzi”.
“Natoa rai kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na wanajamii waje katika kituo, tuwape elimu ya ujasiriamali na ubunifu watakayoweza kuitumia hata baada ya kumaliza masomo yao” alielezea Bw. Kirika.
Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali kilichoanzishwa mwaka 2019 kikiwa na lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza ubunifu, Uanagenzi na Ushirikishwaji wa Jamii ndani na nje ya Taasisi. Kituo hiki kinahudumia wanafunzi waliosajiliwa kusoma kwenye Taasisi hii lakini pia wananchi wanaozunguka maeneo ya jirani na chuo katika wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
#2026
18/12/2025
Happy Birthday Director! ✊✊
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Address
Sing'isi
Arusha