imacrobot

imacrobot

Share

10/08/2021

SIKU AMBAYO MWANADAMU ATATAWALIWA NA KUWA MTUMWA WA TEKNOLOJIA.
Kwa dunia ya sasa tuliyopo sayansi na teknolojia zinazidi kukua kwa kasi kubwa sana.
Nadhani umewahi kusikia habari za SINGULARITY na k**a bado, basi twende pamoja.

Katika elimu ya fizikia, neno SINGULARITY linamaanisha sehemu katika shimo jeusi ambapo, endapo kitu chochote kile kitaingia ndani ya shimo hilo, kitu hicho kitasambaratishwa na kupotea milele.
Baadae neno SINGULARITY likaanza kutumika kuelezea mabadiliko makubwa sana ya teknolojia, ambapo, kompyuta zinazofahamika k**a ARTIFICIAL INTELLIGENCE (A.I) zitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kiakili kuliko mwanadamu.

Kwa mara ya kwanza, SINGULARITY ilianza kuelezewa na mwanasayansi aliyefahamika kwa jina la VENNA VINCI katika kitabu chake cha THE COMING TECHNOLOGOCAL SINGULARITY.Katika kitabu hicho, VENNA alielezea mambo manne muhimu, yatakayomfanya mwanadamu kuunda kiumbe mwenye uwezo mkubwa wa kiakili, kabla ya mwaka 2030.
VENNA aliendelea kwa kusema kuwa, kati ya mwaka 2030 mpaka mwaka 2045, hapo ndipo dunia itakuwa imeshaingia rasmi katika kipindi cha singularity, na kompyuta za A.I zitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kutoa maamuzi k**a wanadamu.

RAY KURZWELL, mwanasayansi na muandishi wa maono ya kiteknolojia, katika kitabu chake cha THE SINGULARITY IS NEAR, yeye anakubaliana na VENNA kuhusu ujio wa teknolojia hii, ila, kwa mtazamo wake yeye anaona teknolojia hii itakuwa na manufaa makubwa kwa wanadamu.Anasema kuwa, teknolojia hii itamsaidia mwanadamu kuongeza ujuzi wake, pia, itamsaidia kutafuta dawa za maradhi mbalimbali pamoja na kutibu magonjwa k**a kupooza na msongo wa mawazo.

Marehemu STEPHEN HAWKING, aliyekuwa mwanasayansi wa nchini Marekani, yeye aliipinga teknolojia hii na kusema kuwa, endapo haitodhibitiwa itaweza kuchukua nafasi kubwa na kuwatawala wanadamu.

Mpaka sasa kuna kila dalili inayoonyesha mwanadamu atatawaliwa na A.I kwani katika baadhi ya makampuni na viwanda leo hii, kazi nyingi hufanywa na ROBOTS.

Wacha tuone jinsi wanadamu watakavyopambana na teknolojia hii pale itakapofika hichooo kipindi cha 2030.

10/08/2021

DUNIANI TUNAISHI KATIKA NDOTO ZA WATU WALIOKWISHAFARIKI MIAKA MINGI ILIYOPITA.
Endapo k**a leo hii utamfufua mtu aliyefariki miaka 100 iliyopita na kumrudisha duniani,basi mtu huyo anaweza kustaajabu na kushangaa jinsi ulimwengu ulivyobadilika, kutokana na mapinduzi makubwa ya sayansi yaliyotokea na yanayoendelea kutokea duniani.
Maisha tunayoishi sasa yalikuwa ni ndoto kwa watu walioishi miaka ya zamani sana,na pia ni maisha ambayo yalionekana kuwa hayatowezekana kabisa kuwepo kwa ulimwengu wa sasa.
Katika ulimwengu wa sayansi kuna aina ya taaluma ijulikanayo k**a BUNILIZI YA KISAYANSI, ama kwa lugha ya kitaalamu hujulikana k**a SCIENCE FINCTION.
Hii ni aina ya fasihi,filamu,michezo ya video au sanaa iliyokuwepo toka miaka ya zamani sana ambapo watu walikuwa wakiandika na kutabiri habari za sayansi na teknolojia ambayo itakuja kutokea kwa miaka ijayo,pamoja na kuchukua nafasi kubwa katika maisha ya mwanadamu.Waswahili husema lisemwalo lipo na k**a halipo basi linakuja,hapa waswahili hawakukosea kabisa๐Ÿ‘.
Mara nyingi bunilizi ya kisayansi huelezea vifaa na sayansi ambayo haipatikani leo hii,bali itakuja kuwepo miaka ya mbeleni.
Mtu wa kwanza aliyewahi kuandika bunilizi yake ni mwandishi kutoka Ufaransa aliyejulikana k**a JULES VERNE, ambaye aliwaza matumizi ya bunduki kubwa itakayomwezesha mwanadamu kufika mwezini.Wakati anaandika haya,watu wengi walimshangaa na kuona kuwa ni kitu kisichowezekana kabisa, ila miaka ya sasa hilo limekuwa ni jambo linalowezekana na pia tunatarajia mwaka 2024 taifa la USA litafanya safari yake kwenda mwezini.
Nadhani sasa umeanza kunielewa kidogo.
Yupo mtu aliyefahamika k**a H.G.WELLS,ambaye aliwaza kuwa miaka ya mbeleni kutakuwa na mashine yenye uwezo wa kupaa angani (aeroplane),pia aliwaza kuwepo kwa mashine za kivita k**a vifaru lakini pia,aliwaza kuwa miaka ijayo kutakuwa na runinga.Hivi sasa vitu vyote alivyowaza mtu huyu vipo, wakati kipindi anayesema haya watu waliona ni ndoto za mchana.
Mtu mwingine ni ISAAC ASIMOV profesa wa masuala ya biokemia ambaye pia alikuwa mwandishi wa bunilizi za kisayansi,yeye aliandika kuhusiana na matumizi ya roboti.
Tusishangae kuona siku moja ELON MUSK akafanikiwa kumfanya mtu aishi milele.๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Arusha