William Benedicto

William Benedicto

Share

07/03/2026

Mashabiki wa Barcelona soogeeni hapa kidogo tuzungumze hii detail ndogo kwenye hii mechi ya Barcelona vs Atletico.

Balde yupo na mpira alioupokea kutoka kwa Gerald Martin ila hakuna sehemu ya kupeleka mpira sababu Atletico wapo watatu (Lloente x Simeone x Koke)

Najaribu kujiuliza wangefanya hivi ingekuwa rahisi kuwawin hasa upande huu wa kushoto wa Barcelona na kulia kwa Atletico.

Gerald alipo ni mbali k**a angesogea karibu maana yake angemlazimisha Griezman kusogea ili kuweka presha kwa Gerlad na kufanya hivyo atamuacha Pedri kuwa huru nyuma yake na kufanya mikimbio kwenda karibu na goli.

Halafu Lloente na Coke wangekuwa eneo hilo hilo ili kutomruhusu Raphina kuleta madhara sasa kufanya hiyo movement tayari Balde anaweza kupokea mpira nyuma ya Simeone na kuangalia kati ya Torres ambae atakuwa ndani ya box au Pedri ambae atakuwa njee nani atampa mpira.

Vipi wewe ukiangalia picha hii unawazaje?

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Arusha