Jesus Power Ministry

Jesus Power Ministry

Share

01/04/2024

UNAJIONA UKIWA WAPI KWA MIAKA 30 IJAYO?

K**a una miaka 30 Leo na bado haujapata kujua nafasi uliyonayo sasa inakupa picha ipi au matokeo yapi baada ya miaka 30 ijayo,Kuna shida mojawapo inayokusumbua kati ya hizi

1.Kutokujua k**a mahala ulipo ni sahihi na kwasababu hiyo kujikutaka unapoteza muda mwingi pasipo kuona matokeo.

MUNGU akamwambia Ibrahim atoke nyumbani kwa baba yake akiwa na takribani miaka 70.Mungu alimwelekeza Ibrahim njia sahihi ya kufanikiwa kwake,k**a neema hiyo isingemjia Ibrahim anegishia kuridhi kasehemu kadogo kwenye Mali ya baba yake na hako kasehemu kadogo ndiko angekagawanya kwa watoto wake.

Yakobo alikaa kwa mjomba wake Rabani kwa zaidi ya miaka 17 bila kuona matokeo halisi ya maisha yake anaona anaongeza watoto katika nyumba ya baba yake bila kujua hatima ya watoto itakuwaje baada yake mpaka pale alipofanya maamuzi ya kusema maisha haya yatosha.

2.Kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa kile unachokifanya kwa sasa.

K**a unafanya biashara na hauoni biashara hiyo katika picha ya mafanikio kwa miaka 30 ijayo maana yake hiyo biashara utaiua.Kuwa na ufahamu wa kutosha na kuwa na mikakati endelevu dhidi ya hiyo biashara yako usipojituma katika kuilisha biashara yako maarifa huwe na hakika biashara hiyo itadumaa.

Uko kwenye ndoa,k**a hauoni mafanikio kwenye ndoa yako kwa miaka 30 ijayo maana yake unachokifanya sasa ni kazi bure.Kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu chanzo Cha amani kwenye ndoa yako,na chanzo Cha kipato kwenye ndoa yako.

MUNGU akawaambia Adamu na Hawa wazae na kuijaza Dunia,Neno wazae maana yake ni mbegu na neno kujaza maana yake ni matokeo ya mbegu wanayoipanda wao,kwa lugha nyingine Kila mbegu unayopanda lazima izae na kwasababu ya kuzaa kule ndoa hiyo itakuwa Bora na yenye heshima.Mungu anaposema mzae hamaanishi tu watoto watokao kwenye viuno vya Mwanaume,anamaanisha kuibua mawazo mapya yaletayo uchumi kwenu, kwahiyo lazima muazimie nyie wawili kushik**ana kwenye zao la kiuchumi.

3.Kusikiliza mawazo ya watu wengine kuliko mawazo yako mwenyewe.

Unapotumia muda mwingi kufanyia kazi mawazo ya watu wengine maana yake unageuka mtumwa, na hakuna mtumwa yeyote duniani aliyewahi kuwa huru.

4.Hofu.

K**a haujioni mtu mwenye thamani sana kwa miaka 30 ijayo,ujue umezingirwa na hofu ya maisha inayokupelekea kutofanya maamuzi ya kukabili kesho yako.Mtu yeyote mwenye hofu ni ngumu sana kuleta mabadiliko yoyote.
Na kwasababu hiyo miako 30 ijayo utakuwa msumbufu sana kwa wale unaohisi unawasaidia Leo maana na wao watakuwa na majukumu pia.

Hofu inafukuza Imani,na mahala pasipokuwa na Imani hapana mavuno.

Zaidi ya yote k**a unajiona mtu flani kwa miaka 30 ijayo.
Zingatia haya mambo muhimu.

1.Jifunze namna ya kuomba kimkakati.
2.Funga kimkakati
3.Jifunze kuweka muda wa utekelezaji wa mipango yako.
3.Kuwa sahihi kwenye malengo yako.
4.Jifunze kuhimili hisia binafsi.(Usiwe mtu wa kuhama hama hivyo.
5.Jibidishe katika elimu
6.Uwe mtu wa Imani
7.Ambatana na mtu sahihi anayeweza kuwa Mwalimu wako au mshauri wako. Na
8 Always stay positive (Daima waza chanya na siyo hasi)

God bless you
Geofrey Julius-Jesus power ministry Tz

23/03/2022

Bwana Yesu asifiwe,
usikose kujiunga nami katika semina yetu leo jioni kupitia mtandao wa zoom saa kumi na moja za jioni 5:00
Ili iweze kushiriki vyema kuwa na app ya zoom kwenye simu yako au kwenye computa yako.
Karibuni.

Geofrey Julius is inviting you to a scheduled Zoom meeting.
Topic: PROTECT YOUR BELOVED SON -SECOND EDITION
Time: Mar 23, 2022 05:00 PM Nairobi
Join Zoom Meeting
https://us04web.zoom.us/j/9924392382...
Meeting ID: 992 439 2382
Passcode: 860616

17/03/2022

PROTECT YOUR BELOVED SON.(MLINDE MWANAO MPENDWA).

Bwana Yesu asifiwe na ongera sana kwa majukumu yako ya kila siku,lakini pia kumshukuru Mwenyezi Mungu yeye anaetuwezesha kuwa hivi tulivyo leo hii.
Leo roho mtakatifu amenikumbusha nikushirikishe jambo hili na pengine kuna vitu inakuhitaji uvijue kuhusu watoto wako au mwanao ajae au aliyekwisha kuwepo.
Somo letu la leo linaitwa Protect your beloved son( mlinde mwanao mpendwa).

Ni ukweli usiopingika mzazi au wazazi wanaweza kuwa na watoto kumi au watano n.k lakini mzazi katika hao watano yupo mmoja apendwae sana,wakati mwingine mzazi anaweza kujitahidi kuficha upendo huo lakini mara nyingi ushindikana mpaka wote mle ndani mnajua baba au mama anampenda nani.
Sasa wazazi hawa wawili yaani baba na mama baba anaweza kuonyesha upendo wa wazi kwa mtoto flani lakini mama nae akawa na mtoto wake anaempanda.Unaweza ukawa hautoki katika familia za zaidi ya wake watatu au wawili unatoka kwenye familia ya baba mmoja na mama moja lakini baba asiposimama imara mzao wake wa kwanza wa haki atachukuliwa anaweza akafa ghafla,au madhabahu ya mama ya siri ikamfanya kuwa wa mwisho waswahili wanasema kupigwa zongo (mzee anapigwa zongo upendo unahama ghafla yaani mzee anahamisha uridhi wake kwa mtoto mwingine lakini si kwasababu anampenda huyo bali madhabahu ya mkewe imeamua kufanya hivyo.) Biblia inasema enyi waume ishini na wake zenu kwa akili,kitendo cha kuhamishwa fahamu mzee wa nyumba ukoo wako wote unauingiza mateka chini ya madhabu ya mkeo ambae yeye anauwakilisha ukoo wa nyumbani kwake,uzao wako na ukoo wako utaitegemea madhabu ya ujombani.

Sikiliza Mungu alimwambia Ibrahim kwamba uzao wake utaingizwa matekani kwa muda ya miaka arobaini,lakini lilibaki fumbo kwa Ibrahim hakuambiwa kwasababu gani wataingizwa mateka watu hao. Okay,uzao wa Ibrahim wa haki yaani ISAKA akapata mke,na huyo mke aliyepata Mungu alihusika kabisa asilimia miamoja,.Isaka akapata uzao katika uzao ule ISAKA akampenda sana Esau kuliko yakobo na mkewa akalijua hilo,jambo hilo halikufanyika baraka kwa mkewe ISAKA, Yakobo akajikuta anapendwa sana na mama yake kuliko baba yake.Swali ni je kwa nini upendo wa ISAKA ulionekana mkubwa kwa Esau ni kwasababu Esau alikuwa akimletea mzee chakula kitamu alichokiwinda mwenyewe.
Bilashaka mawindo ya Esau yalikuwa yanaliwa na familia yote,je kwa nini hilo halikumpendeza mama yake Esau,mama akaona afanye hila kwa mtoto wake mwenyewe aliyemzaa tena na uchungu alipata lakini akaigeuza kesho ya Esau kwa hila.

Sasa tizama madhabahu za giza zilizo na nguvu,ni kitu gani kiliuteka moyo wa mama yake Esau na kuona kwamba anaestahili kupata mbaraka wa haki ni Yakobo.kumbuka mama yake Yakobo alikuwa na kaka yake anaitwa Laban na huyu kaka yake yeye alikuwa mshirikina kwahiyo madhabu ya kaka ikaukaba moyo wa dada yake,yaani Mama yake Esau alipokwisha kufanya tendo hilo la hila akamtuma kwa haraka Yakobo akae kwa mjomba wake Laban ajipatie mjtaji huko.
Lakini kwa sababu madhabahu ile ndio ilihusika kugeuza moyo wa dada yake Yakobo hakuweza kufanikiwa kwa mjoba wake matokeo yake akaingizwa mateka na mjomba wake.Yaani Laban akawa anahusika kula kwa Yakabo,kuvaa kwake,kulala kwake lakini pia kulisha wake zake na watoto wake kumbuka ni ujombaniiiiiiii.

Chunguza sana katika familia za kiafrika wajomba wanahusika sana kulea watoto wa dada zao upande wa baba wengi wao nguvu ya kiuchumi huwa ni changamoto k**a yuko mmoja anaonyesha kamwanga kwenye ukoo huo akifa ndio imeisha hiyo.
Nguvu ya Yakobo kutoka mikononi mwa mjomba wake ni Mungu mwenyewe,tena mjomba alipotaka kuinua kisasi dhidi ya Yakobo Mungu akamwambia usijaribu kumfanya chochote Yakobo,haikuwa mizimu ya baba yake ISAKA au mzimu wa ISAKA mwenyewe alikuwa ni Mungu mwenyewe.
Ninachotaka utambue hapa nini ni kwamba mtoto wako mpendwa anaweza kupolwa haki yake ya uridhi na akaashiria kupoteza mwelekeo kabisa lakini k**a Mungu anahusika katika upendo huo siku wasiyodhania watu huyo mtoto wako mpendwa Mungu atamkumbuka na sasa atahamisha upendo wake wote kwa huyo mtoto na atafanyika kuwa mridhi wake yaani YESU KRISTO BWANA ndicho kilichofanyika kwa Yakobo,Mungu anamwambia Yakobo hutaitwa Yakobo tena bali utaitwa Israel,neno hutaitwa Yakobo tena manake yakobo alikuwa mkiwa,tasa anajiona yuko na watu,familia alifikili yuko mahali salama kumbe alikwisha polwa na nafsi imefichwa kwenye vitunguli za mjomba wake.

Nakumbuka siku moja miaka imekwisha pita kidogo nikaona njozi katika njozi hiyo niliona mwanga mkubwa sana ukitoka mbinguni na nilikuwa naonekana niko kwenye msitu alafu katika mwanga ule ndani yake kunatoka sauti na sauti hiyo ilikuwa nzito sana na likatamkwa jina jipya () nimeliweka kwenye mabano niliposhtuka sikutaka kuifuatilia sauti hiyo kwasababu nilikuwa nakula,nakunywa,nalala bure kabisa sina mawazo lakini baada ya kuanza maisha yangu na nikaokoka ndio sasa sauti hiyo nikaweza kuitambua.

Nihitimishe kwa kusema hivi,kuna watu ni watumishi leo lakini kabla ya utumishi wao hawakuwa wanajua wanastahili kufanya nini katika maisha yao,ukipolwa haki yako ya upendo kwa mzazi wako au wazazi wako iwe umezaliwa kwenye familia ya zaidi ya moja,majira yako yatafika ya kuitambua sauti ya Mungu ambaye yeye ni mtoa uridhi usioweza kufananishwa wala kulinganishwa na jamii ya kwenu,mara nyingi fikra za wanafamilia wengi zipo katika kile wanachokiona na kwasababu ya hicho upendo wa kinafiki ni mwingi ndani mwake kukuua,kukufanya mgonjwa wa kudumu kwao siyo shida,sikiliza mama yake Yakobo hakuna mahali biblia inasema alijutia uovu wake yeye aliona ni sawa kufanya hivyo na hukuna mtu wa kumuuliza,lakini kwasababu ya kosa hilo uzao wa yakobo ukaingizwa mateka miaka arobaini.
K**a yupo mtoto unampenda ukijua kesho ya mtoto huyu ni ya wengi hakikisha unamshika Mungu,kwasababu madhabahu inayopinga upendo huo inamtafuta mwanao ipate kummeza.

Mungu akubariki sana.
Geofrey Julius

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


Usa-River
Arusha
255