Lofty Matambo
What a beautiful game this was.
FT Brazil 1-1 Morocco
Guys watch out this MOROCCO🔥🔥.
13/06/2026
Yaani World Cup ndo imeanza leo.
HT BRAZIL 1-1 MOROCCO.
Unaona itaishaje hii?
13/06/2026
IT'S A BABY BOY!!!
MY CRUSH!
Nilipoiona filamu yake ya kwanza 'Point of No Return' mwaka 2011(pale Bakarani, Kisauni, Mombasa kwenye kiBedsitter changu kimoja safii😀, na maridadi), nilimpenda sana Wema. Nilikuja kujua baadaye hiyo kitu ilikuwa inaitwa kucrushia mtu.
Wema alikuwa anaigiza k**a Dina(2008). Kidosho aliyelazimishwa kuolewa na mganga. Kwa ufupi Wema alikuwa crush wangu🤭.
WEMA!
Wema Isaac Sepetu.
Katika umri wa miaka 38(Wikipedia)ametangaza kubarikiwa na mtoto wake kutoka tumboni mwake, mtoto wa kiume.
Wema aligonga vichwa vya umaarufu Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika nzima punde aliposhinda shindano na kutawazwa Bi Urembo Tanzania mwaka 2006.
Kisha akaiwakilisha TZ katika shindano hilo la ulimwengu nchini Poland mwaka uo huo wa 2006.
Wema ameigiza zaidi ya sinema 20 kwa lugha ya Kiswahili na pia Kingereza akiwa na waGhana na WaNigeria.
Baadhi ya Tamthilia matata alizohusishwa Wema na nguli wa uigizaji TZ mwenda zake Steven Kanumba ni: 'Family Tears', 'Red Valentine', 'White Maria' na zingine kochokocho.
Wema amekula na wakuu wa nchi, wafalme, mabwanyenye, waite walala heri ukipenda, ila alichokikosa ni kimoja tu: Mtoto. Mtoto wake mwenyewe. Ampakate, amuongoe, amchekeshe, amdekeze. Aitwe mama fulani.
Alikosa raha, akanuna roho, akavimba mashavu, akalia, kilio cha zaidi ya miaka 10. Hatimaye ameonekaniwa. Amebarikiwa. Heko dada Wema👏👏.
Kweli Mungu si Athumani. K**a amemkumbuka Wema, bado wewe. Hachelewi wala haji upesi. Amini, pokea muujiza wako leo.
Picha: Insta ya Wema
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Kilifi