Église Rehema RDC

Église Rehema RDC

Partager

26/12/2025

𝗡𝗚𝗨𝗩𝗨 𝗬𝗔 𝗡𝗗𝗢𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗛𝗔𝗧𝗜𝗠𝗔 𝗬𝗔𝗞𝗢

𝙼𝚊𝚏𝚞𝚗𝚣𝚘 𝚢𝚎𝚝𝚞 𝚖𝚊𝚊𝚕𝚞𝚖 𝚔𝚠𝚊 𝚊𝚓𝚒𝚕𝚒 𝚢𝚊 𝚟𝚒𝚓𝚊𝚗𝚊 𝚢𝚊𝚝𝚊𝚏𝚊𝚗𝚢𝚒𝚔𝚊 𝚕𝚎𝚘 𝚜𝚊𝚊 𝚗𝚊𝚗𝚎 𝚖𝚌𝚑𝚊𝚗𝚊 (𝟷𝟺𝚑).

𝙽𝚓𝚘𝚘 𝚞𝚏𝚊𝚑𝚊𝚖𝚞 𝚞𝚜𝚑𝚊𝚠𝚒𝚜𝚑𝚒 𝚗𝚊 𝚗𝚐𝚞𝚟𝚞 𝚊𝚖𝚋𝚊v𝚢𝚘 𝚗𝚍𝚘𝚊 𝚒𝚗𝚊𝚠𝚎𝚣𝚊 𝚔𝚞𝚠a 𝚗𝚊𝚢𝚘 𝚔𝚊𝚝𝚒𝚔𝚊 𝚖𝚊𝚒𝚜𝚑𝚊 𝚗𝚊 𝚑𝚊𝚝𝚒𝚖𝚊 𝚢𝚊𝚔𝚘.

𝙈𝙖𝙛𝙪𝙣𝙙𝙞𝙨𝙝𝙤 𝙝𝙖𝙮𝙖 𝙮𝙖𝙩𝙖𝙩𝙞𝙧𝙞𝙧𝙞𝙨𝙝𝙬𝙖 𝙩𝙚𝙣𝙖 𝙢𝙩𝙖𝙣𝙙𝙖𝙤𝙣𝙞 𝙠𝙪𝙥𝙞𝙩𝙞𝙖 𝙪𝙠𝙪𝙧𝙖𝙨𝙖 𝙮𝙖 F𝙖𝙘𝙚𝙗𝙤𝙤𝙠 𝙮𝙖 𝘽𝙞𝙨𝙝𝙤𝙥 𝘿𝙖𝙣𝙞𝙚𝙡 𝙏𝙘𝙝𝙞𝙗𝙤.

𝙼𝚊𝚑𝚊𝚕𝚒: 𝙺𝚊𝚗𝚒𝚜𝚊 𝚕𝚊 𝚁𝙴𝙷𝙴𝙼𝙰 𝚒𝚔𝚘 𝚖𝚞 𝚁𝚘𝚞𝚝𝚎 𝚍'𝚞𝚟𝚒𝚛𝚊.

𝙸𝚔𝚘 𝚔𝚞 :

· 𝙼𝚒𝚝𝚊 𝟻0 𝚔𝚞𝚝𝚘𝚔𝚎𝚊 𝚔𝚞 𝙿𝚕𝚊𝚌𝚎 𝚍𝚎 𝚕'𝚒𝚗𝚍𝚎́𝚙𝚎𝚗𝚍𝚊𝚗𝚌𝚎.
· 𝙼𝚒𝚝𝚊 𝟷𝟻0 𝚔𝚞𝚝𝚘𝚔𝚊 𝚔𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎 𝚂𝚘𝚔𝚘 𝚕𝚊 𝙼𝚋𝚊𝚘 (𝙼𝚊𝚛𝚌𝚑𝚎́ 𝚍𝚎𝚜 𝙿𝚕𝚊𝚗𝚌𝚑𝚎𝚜) 𝚞𝚔𝚒𝚝𝚘𝚔𝚎𝚊 𝚔𝚞 𝙴𝚜𝚜𝚊𝚗𝚌𝚎.

30/07/2025

𝗠𝗶𝗺𝗶 𝗔𝘀𝗸𝗼𝗳𝘂 𝗗𝗔𝗡𝗜𝗘𝗟 𝗧𝗖𝗛𝗜𝗕𝗢 – 𝗡𝗔𝗞𝗨𝗔𝗟𝗜𝗞𝗔!

Itakuwa heshima kubwa kwetu, na uta tajirisha KIROHO yako kwa kushiriki katika 𝗺𝗸𝘂𝘁𝗮𝗻𝗼 𝗵𝘂𝘂 𝘄𝗮 𝘂𝗮𝗺𝘀𝗵𝗼 𝘄𝗮 𝘀𝗶𝗸𝘂 𝟱, kuanzia 𝘁𝗮𝗿𝗲𝗵𝗲 𝟭𝟮 𝗵𝗮𝗱𝗶 𝟭𝟳 𝗔𝗴𝗼𝘀𝘁𝗶 𝟮𝟬𝟮𝟱, 𝘀𝗮𝗮 𝟴:𝟯𝟬 𝗺𝗰𝗵𝗮𝗻𝗮 𝗵𝗮𝗱𝗶 𝘀𝗮𝗮 𝟭𝟮 𝗷𝗶𝗼𝗻𝗶, chini ya mada:

"𝗠𝗮𝗺𝗹𝗮𝗸𝗮 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗼 𝗽𝗲𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗮𝗱𝗮𝗺𝘂 𝗻𝗮 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂 𝗶𝗽𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮𝗻𝗮𝘆𝗼 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗶𝗴𝘂𝘂."

Mkutano huu utafanyika katika kanisa la 𝗥𝗘𝗛𝗘𝗠𝗔, 𝗹𝗶𝗹𝗶𝗹𝗼𝗸𝗼 𝗺𝘁𝗮𝗮 𝘄𝗮 𝗞𝗶𝗯𝗼𝗺𝗯𝗼 𝗻°𝟬𝟵𝟳𝗧 /𝗥𝗼𝘂𝘁𝗲 𝗱'𝗨𝘃𝗶𝗿𝗮, 𝗺𝗶𝘁𝗮 𝟱𝟬 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗸𝗮 𝗻𝗴𝗮𝘇𝗶 𝘇𝗮 𝗸𝗮𝗻𝗶𝘀𝗮 𝗹𝗮𝘄𝗮 𝗕𝗿𝗮𝗵𝗻𝗮𝗺𝗶𝘀𝘁𝗲 (𝘂𝗸𝗶𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮 𝗣𝗹𝗮𝗰𝗲 𝗱𝗲 𝗹’𝗜𝗻𝗱𝗲́𝗽𝗲𝗻𝗱𝗮𝗻𝗰𝗲) 𝗻𝗮 𝗺𝗶𝘁𝗮 𝟭𝟱𝟬 𝗸𝘂𝘁𝗼𝗸𝗮 𝘀𝗼𝗸𝗼 𝘆𝗮 𝗺𝗶𝘁𝗶 (𝘂𝗸𝗶𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮 𝗘𝘀𝘀𝗮𝗻𝗰𝗲).

𝗠𝗸𝘂𝘁𝗮𝗻𝗼 𝗵𝘂𝘂 𝘂𝗺𝗲𝗮𝗻𝗱𝗮𝗹𝗶𝘄𝗮 𝗻𝗮𝗺𝗮 𝗣𝗮𝘀𝘁𝗮 𝗩𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮 𝘄𝗮 𝗷𝗶𝗷𝗶 𝗹𝗮 𝗕𝘂𝗸𝗮𝘃𝘂.

Karibu sana! Uwepo wako utakuwa baraka na msaada mkubwa.

22/07/2025

𝗕𝗨𝗦𝗧𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗘𝗗𝗘𝗡𝗜 – 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂 𝗮𝗹𝗶 𝗮𝗻𝗱𝗮𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝗸𝗶𝘁𝘂 𝗸𝗮𝗯𝗹𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗸𝘂𝘂𝗺𝗯𝗮 !

Kabla Mungu kuumba mwanadamu, alitengeneza kwanza Bustani ya Edeni, akajaza humo kila kitu mtu angehitaji. Hakukuwa na ombi, shida, au mahitaji—byote bilikua tayari.
Na hata leo, byote unabyomwomba Mungu biko tu hapa duniani : mke mwema, kazi, afya, nyumba, heshima, amani—biko. Mungu alishaviweka tayari.

Lakini angalia : Adam na Eva waliishi humo, hadi walipomkorofisha Mungu. Ndio, wakaondolewa. Na kuanzia hapo, malaika mwenye upanga aliwekwa kulinda bustani, ili asiingie tena mtu yeyote atakaye tumia baraka hizo bila kumpa Mungu nafasi yake.

➡️ Edeni ni jumla ya byote Mungu alitengeneza kwa ajili ya mwanadamu kuishi maisha mazuri chini ya jua. Lakini kila mtu ana “malaika wa kuzuia”, na huyo malaika anakuzuia kufikia vitu fulani kulingana na nafasi unayompa Mungu ndani ya maisha yako.

Usinieleze k**a watu wa dunia wana mali—wanaipata, lakini hawaifurahii. Ni baada ya kuwa na utajiri ndipo magonjwa yanakuja : diabète, cancer, goutte, tension...

🚫 Uko na ng’ombe 500, lakini daktari amekuzuia kula nyama.

🚫 Uko na magari kibao, lakini afya imechoka—umeambiwa utembee kwa miguu.

🚫 Una pesa, lakini hakuna mtoto wa maana wa kukurithi; au ulionao hawana hekima—wataharibu yote uliojenga.

Lakini wewe sikiya !

Kitabu cha Mhubiri kinasema:
« Hakuna jambo jema chini ya jua k**a kula, kunywa na kufurahia matunda ya kazi yako… maana hiyo ndiyo sehemu Mungu aliyompa mwanadamu. »
Lakini usisahau kwamba ili kufurahia maisha kikamilifu, ni lazima umpe Mungu nafasi yake k**a Mwokozi na Bwana wa maisha yako — Yeye ndiye atawale juu yako, siyo ukabila, siyo uchoyo, siyo wivu, wala tabia mbaya yeyote ile.

Pia wekeza katika mambo ya thamani kweli: kazi ya Mungu. Weka hazina yako mbinguni, kwa maana unapo pita majaribu, Mungu atakumbuka maombi na sadaka zako ulizo zifanya kwa moyo.
Matendo ya mitume 10:4

Kumbukumbu hii maalum hugusa moyo wa Mungu, na kumu shawishi kuingilia kati katika nyakati zako ngumu.

🙌 Mungu akupe raha, ule kubyako, ufurahie kazi ya mikono yako. Upate vyote unavyohitaji na uvitumie kwa utukufu Wake, bila masharti wala mateso.

05/02/2025

𝗞𝗼𝘃𝘂 𝘇𝗮 𝗨𝗳𝘂𝗳𝘂𝗸𝗼

Ni kweli kwamba Yesu alifufuka na yuko hai. Lakini kuna mambo kadhaa ambayo hayakubadilika kwake: alirudi kutoka kwa wafu akiwa na makovu ya majeraha aliyopata msalabani. Makovu hayakuwa ishara ya udhaifu, bali uthibitisho wa kushinda migogoro na mashaka ya Thoma, ili "𝘸𝘦𝘯𝘺𝘦 𝘩𝘢𝘸𝘢𝘬𝘶𝘰𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘢𝘮𝘪𝘯𝘪" (Yohana 20:29).

Vivyo hivyo, kila mwana wa Mungu anayetoka katika majaribu au msimu mgumu afahamu kwamba hawezi kufufuka bila makovu. Makovu haya siyo kukumbusha aibu, bali ni kwa ajili ya 𝙪𝙨𝙝𝙪𝙝𝙪𝙙𝙖.

Maisha yetu ya jana yamebaki kwa muhuri katika maisha yetu ya sasa kudhihirisha ukweli huu: 𝙈𝙪𝙣𝙜𝙪 𝙖𝙡𝙞𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙥𝙖𝙢𝙤𝙟𝙖 𝙣𝙖𝙨𝙞 𝙟𝙖𝙣𝙖, 𝙮𝙪𝙠𝙤 𝙥𝙖𝙢𝙤𝙟𝙖 𝙣𝙖𝙨𝙞 𝙡𝙚𝙤, 𝙣𝙖 𝙖𝙩𝙖𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙥𝙖𝙢𝙤𝙟𝙖 𝙣𝙖𝙨𝙞 𝙠𝙚𝙨𝙝𝙤.

Makovu haya yatanyamazisha vinywa vya wapumbavu na wasioamini ambao hawajui kwamba 𝘔𝘶𝘯𝘨𝘶 𝘸𝘦𝘵𝘶 𝘩𝘶𝘵𝘦𝘯𝘥𝘢 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘷𝘪𝘵𝘢 𝘷𝘺𝘦𝘵𝘶, 𝘧𝘶𝘳𝘢𝘩𝘢 𝘻𝘦𝘵𝘶, 𝘶𝘴𝘩𝘪𝘯𝘥𝘪 𝘸𝘦𝘵𝘶, 𝘯𝘢 𝘩𝘢𝘵𝘢 𝘬𝘶𝘬𝘢𝘵𝘢𝘭𝘪𝘸𝘢 𝘬𝘸𝘦𝘵𝘶.

Vous voulez que votre lieu de culte soit Lieu De Culte la plus cotée à Bukavu ?
Cliquez ici pour réclamer votre Listage Commercial.

Téléphone

Site Web

Adresse


BUKAVU
Bukavu

Heures d'ouverture

Mardi 16:00 - 19:30
Jeudi 16:00 - 19:30
Vendredi 20:00 - 06:30
Samedi 09:00 - 12:00
16:00 - 19:30
Dimanche 09:00 - 15:00
16:00 - 19:00