MTEULETHEBEST.COM
30/01/2026
ALIPINDULIWA KWA KUKATA MIRIJA YA MABEBERU IRAN.
Dkt. Mohammad Mossadegh alikuwa Waziri Mkuu wa Iran, aliyechaguliwa na Bunge la 16 la Iran (16th Majlis) mwaka 1951.
Anakumbukwa kwa kutaifisha sekta ya mafuta ya Iran ili kujenga uchumi imara wa taifa na watu wake. Hatua hiyo, iliwaudhi mabepari wa Magharibi. Mirija ya Uingereza na Marekani ilikaushwa na kuzua hasira kubwa kwa makampuni vigogo vya uchimbaji na uchakataji mafuta ya nchi hizo.
Agosti 19, 1953, mapinduzi ya kumuondoa madarakani Mosaddegh yanafanikiwa. Mashirika ya Ujasusi, CIA ya Marekani na MI6 ya Uingereza yalikiri baadae kuhusika na mapinduzi hayo.
Nafasi ya Mossadegh anaichukua Jenerali Fazlollah Zahedi aliyependekezwa na MI6 ili kulinda maslahi ya wakubwa wa Magharibi. Mapinduzi hayo yaliimarisha zaidi utawala wa Reza Shah wa Iran.
Baada ya Mapinduzi, Mossadegh alik**atwa, akatupwa gerezani kwa miaka mitatu, kisha akahukumiwa kifungo cha maisha cha nyumbani, hadi alipofariki dunia mwaka Machi 05,1967 kwa ugonjwa wa saratani na vidonda vya tumbo vilivyochachamaa na kuanza kuvuja damu ndani kwa ndani.
Utawala wa Shah ulikataa kumzika licha ya ombi lake la kuzikwa kwenye makaburi ya umma pembeni ya waathirika wa vurugu za kisiasa waliouawa mwaka 1952.
Ili kuepusha taabu na wenye nchi, familia ilimzika sebuleni kwake. Hadithi ya mwanamageuzi, mwanasiasa aliyetishia umaarufu wa Shah, Mtunzi wa Vitabu na Mwanasheria nguli ikazikwa kwa namna ya fedheha kabisa.
Kupinduliwa kwa serikali ya kidemokrasia iliyotikisa meza ya vinywaji vya gharama vya Magharibi kumeacha alama isiyofutika kwa historia ya Iran, kiasi Waajemi wengi hawana imani kabisa kwa madola ya Magharibi yanayohubiri demokrasia na utawala bora na haki za binadamu, yakiwapaka mafuta mataifa mengi kwa mgongo wa chupa.
Dkt. Mossadegh alizaliwa Juni 16, 1882 na kufariki dunia Machi 05, 1967 akiwa na umri wa miaka 84. Aliacha Watoto watano.
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X
KILINGENI - WhatsApp channel Follow KILINGENI's WhatsApp Channel. Kituo hiki kimeundwa mahususi kukuletea taarifa sahihi na za haraka kuhusu Soka, Teknolojia, Biashara, Habari za Kimataifa]. Lengo letu ni kukupa maarifa, habari, na vidokezo muhimu moja kwa moja kwenye simu yako. Jiunge nasi na uwe wa kwanza kujua kinachoendelea!. Join 153 followers for the latest updates.
29/01/2026
Ndege moja aina ya Airbus A321-231 inayomilikiwa na kampuni ya ndege ya Meraj, iliyosajiliwa k**a IRAN07, ambayo kwa kawaida hutumiwa na viongozi wakuu wa utawala wa Kiislamu, iliondoka Tehran kuelekea Moscow, Urusi, mapema leo
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X
23/01/2026
Mkuu wa majeshi nchini Uganda ambaye pia ni mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugana amesema siku ya Ijumaa kuwa wanachama 30 wa upinzani wameuawa na watu 2,000 kuk**atwa baada ya uchaguzi.
“Tumewak**ata zaidi ya wahuni 2,000 ambao Kabobi alidhani angewatumia,” aliandika mkuu wa majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba kwenye mtandao wa X, akitumia jina la kumkejeli Bobi Wine (Kabobi).
“Mpaka sasa tumewaua magaidi 30 wa NUP,” alisema, akiashiria chama cha Bobi Wine, cha National Unity Platform (NUP).
Kiongozi wa upinzani Bobi Wine bado yuko mafichoni baada ya kushtumu vikosi vya usalama kwa kuvamia nyumba yake kufuatia uchaguzi uliofanyika Januari 15.
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X
20/01/2026
Chama cha upinzani cha People's Front for Freedom nchini Uganda kinachoongozwa na Kizza Besigye, kimesema leo kuwa afya ya kiongozi huyo aliyefungwa inadhoofika, baada ya kukimbizwa usiku kwenye kituo cha matibabu katika mji mkuu wa Kampala.
Katika taarifa yake, chama hicho kimesema kuwa Besigye yuko katika hali mbaya kiafya. Aidha, kimetoa wito kwa maafisa wa Uganda kuhakikisha madaktari binafsi pamoja na familia yake wanaonana naye bila vikwazo vyovyote.
Chama hicho kimeendelea kusema ni jambo la kusikitisha kwamba mtu ambaye amejitolea maisha yake kwa afya na uhuru wa wengine ananyimwa haki yake ya kupata utu wa matibabu.
Kwa upande wake, msemaji wa mfumo wa magereza nchini humo Frank Baine, amekanusha taarifa hiyo .
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X
20/01/2026
Mkuu wa majeshi ya Uganda Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa rais wa muda mrefu Yoweri Museveni, amesema anataka kuona kiongozi wa upinzani Bobi Wine akiwa amekufa, siku chache baada ya Wine kudai kuwa alilazimika kujificha.
Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X jana usiku, Kainerugaba amesema wamewauwa magaidi 22 wa chama cha NUP tangu wiki iliyopita na kwamba anaomba gaidi wa 23 awe Kabobi, akimzungumzia Wine na chama chake cha National Unity Platform (NUP).
Katika chapisho lingine, amesema amempa Wine muda wa saa 48 kujisalimisha kwa polisi la sivyo watamchukulia k**a muasi na kumshughulikia ipasavyo.
Wine amekosoa vitisho hivyo vya Kainerugaba na kuwataka wanajeshi kuondoka kwenye nyumba yake, na akaongeza kuwa mke na watu wake hawako salama.
DW
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X
20/01/2026
Simba SC imetambulisha ingizo jipya la tatu kwa maana wachezaji wapya kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
Asubuhi ya leo Wekundu wa Msimbazi wameweka hadharani kuingia mkataba wa miaka miwili na beki wa kati, Ismael Olivier Traore kutoka Falme za Kiarabu.
Mwamba huyo ana uzoefu na soka la Afrika baada ya kucheza Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa akiwa na timu k**a vile Asec Mimosas, Marumo Galants na Stellenbosch.
Usajili huo wa raia huyo wa Ivory Coast unakuwa ni wa tatu mpaka sasa baada ya awali kutambulishwa winga, Lebasse Guey na mbavu ya kushoto, Nickson Kibabage.
Wakati huo taarifa za ndani zikieleza muda wowote atatambulishwa kiungo wa mpira, Clatou Chota Chama ambapo atakuwa anarejea nyumbani kwa mara ya tatu.
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X
17/01/2026
Meja Jenerali Soren Andersen, Kamandi ya Pamoja ya Aktiki ya Denmark huko Greenland, mnamo Januari 16 alikanusha madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba meli za China na Urusi zinazunguka Greenland na kuthibitisha kwamba hakuona meli zozote za kijeshi za Urusi au China katika eneo hilo katika kipindi cha miaka miwili na nusu ambayo amekuwa k**anda, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBK1DyAInPleGrQw71X