AFYA BORA

AFYA BORA

Share

06/01/2019

EXCESS ALCIHOL USE
Too much alcohol use has impact on your health. Increased risk of cardiovascular DISEASES, diabetes mellitus, cancers, low body immunity and affects child before born in pregnant mother. Drink responsibly and lower your risks
Emanuel Ulomi, M.D

13/06/2018

Cardiovascular diseases are still the world's largest killer.
This is how you can reduce your risk of heart attack and stroke((WHO)

Photos from AFYA BORA's post 04/02/2018

SIKU YA SARATANI DUNIANI

Saratani hutokana na ukuaji usio wa mpangilio wa kawaida wa seli za mwili. Kuna vichocheo mbalimbali vinavyochangia k**a historia ya aratani kwenye familia au ndugu wa karibu, mionzi mkali, matumizi ya pombe nyingi Kwa mda mrefu, uvutaji wa sigara n.k

Saratani ya mapafu na tezi dume ni miongoni mwa saratani zinazoongoza Kwa wanaume Tanzania

Kwa wanawake saratani zinazoongoza ni Ile ya matiti na shingo ya kizazi. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza Kwa saratani ya shingo ya kizazi duniani.

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI/ CERVICAL CANCER
Husababishwa na kirusi kiitwacho Human Papiloma virus (HPV)
Huenezwa Kwa njia ya zinaa. Maambukizi hutokea mda mrefu mpaka dalili kuonekana.

Vichochezi vinavyoongeza hatari ya kupata maambukizi ni k**a ifuatavyo:
1. Kwanza ngono katika umri mdogo.

2. Maambukizi ya virusi vya UKIMWI

3. Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja

4. Uvutaji wa sigara

5......
n.k

Dalili zake ni:
1. Kutokwa na uchafu/maji yenye harufu sehemu ya siri ya mwanamke

2. Kutokwa damu tofauti na zile za kawaida za kila mweZi Kwa mwanamke

3. Maumivu wakati wa tendo la ndoa

4. Kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa

Kulingana na kusambaa Kwa saratani dalili zifuatazo huweza kutokea pia

1. Kushindwa kukojoa vizuri au mkojo kutoka sehemu ya ukeni

2. Kuvimba miguuu au mguu mmoja

3. Kupata choo kigumu au damu kwenye choo na maumivu

4. Upungufu wa damu mara Kwa mara

5. Maji kwenye figo ( hydronephrosis) husababisha figo kushindwa kufanya kazi vizuri

6. Kupumua Kwa shida. Mapafu yanapoathirika

7. Maumivu sehemu ya chini ya mgongo Kwa mda mrefu mara nyingi huambatana na miguu kufa ganzi

n.k

KINGA
Chanjo ya kirusi cha HpV ndo njia ya uhakika zaidi

Njia nyingine ni kukwepa ngono katika umri Mdogo

Kuwa na mpenzi mmoja na mwaaminifu

Kupima mara Kwa mara, hii hufanywa na mtaalamu wa afya Kwa kuchukua majimaji kwenye shingo ya kizazi na kuyapima

Kutumia dawa za kuongeza KINGA ya mwili Kwa walioathirika na UKIMWI

Kutumia KINGA. Kinga k**a kondomu hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya zinaa.

MATIBABU
Hakuna matibabu halisi ya kuua kirusi cha HPV.
Matibabu hulenga kupunguza kusambaa na madhara zaidi ya saratani.
Shauriana na mtaalamu wako wa Afya(Daktari) atakusaidia matibabu yanayokufaa.

USIONE HAYA KUTAFUTA TIBA HISPITALINI K**A UNAZO DALILI. HAITIBIKI KWA DAWA ZA KIENYEJI

01/12/2017

Today is world's AIDS day,It is certain that ending the AIDS epidemic will mean so much to so many. It will mean zero new HIV infections, zero people dying of AIDS—and all people living with dignity and without fear of discrimination. Ending AIDS will mean celebrating birthdays instead of attending funerals.

But make no mistake, stigma, denial and complacency are still among us, putting us in danger of failing the next generation. We must join our hearts and our voices––together we are stronger.

The world is poised to end AIDS and if we stay true to our vision we will remember this as the day that a lifelong of dreams began to transform into reality.

Leo ni siku ya ukimwi duniani, ni dhahiri kwamba kutokomeza ukimwi kuna maana kubwa sana Kwa wali wengi. Maambukizi mapya sifuri, kutokomeza vifo,na watu kuishi Kwa utu bila hofu ya kunyanyapaliwa.Kutokomeza ukimwi kuna maana ya kusherehekea kuzaliwa badala ya kuhudhuria mazishi.

Usifanye makosa,unyanyapaa na kutokukubaliana na hali halisi bado kupo katika jamii zetu,huku kunatuweka hataruni na kuharibu kizazi kijacho.
Ni lazima tuungane pamoja--pamoja tunaweza.

Dunia nzima imehabarishwa kutokomeza UKIMWI, k**a tukiwa wakweli katika hili tutaikumbuka k**a siku ambayo ndoto zetu zilianza kutimia kweli

Want your school to be the top-listed School/college in Njombe?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address

Njombe