LINDA AFYA YAKO
17/10/2019
*JE, UNAJUA UGONJWA WA BAWASIRI (HEMORRHOIDS) NI NINI????!!*
~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.
~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu unaitwa HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika k**a PILES. Katika jamii yetu ya KiTanzania ugonjwa huu unatambulika kwa majina tofautitofauti yakiwemo *bawasiri, mgolo, mang'ondi n.k*
~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa _karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50_
*AINA ZA BAWASIRI*
~Kuna Aina mbili za bawasiri
*(A) BAWASIRI YA NDANI*
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika
(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.
(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.
(4)DARAJA LA NNE : hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.
*(B)BAWASIRI YA NJE*
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu hilo. Pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha aina ya bawasiri iitwayo _THROMBOSED HEMORRHOIDS_
*NINI CHANZO CHA BAWASIRI?*
Bawasiri ni tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Huu mfumo ukishakua mbovu una kupelekea kutokupata choo vizuri.
Mfumo mbovu wa mmeng'enyo wa chakula unasababisha chakula kisimeng'enywe vizuri kwenye utumbo mdogo na hivyo kupelekea chakula kupitiliza kwenda moja kwa moja k**a kilivyo kwenda kwenye utumbo mkubwa ambapo maji maji kutoka kwenye chakula hufyonzwa na kuacha chakula kikiwa kikavu. Inapofikia wakati wa kupata choo; choo kinakua kikavu hivyo unatumia nguvu nyingi kukisukuma choo kitoke.
Sasa kitendo hicho kinapelekea misuli & mishipa ya haja kubwa kutanuka na kupelekea kukwanguliwa na choo kigumu na hivyo kinyama kuanza kujitengeneza, na hapo ndipo utaanza kusikia maumivu na miwasho kwa ndani, na mara nyingine kupata choo chenye damu.
Kadri unavyoendelea kupata choo kigumu mishipa inaendelea kukwanguliwa na kinyama kuongezeka mpaka kinatokezea nje na hicho kinyama kinaitwa Bawasiri (Hemorrhoids).
Mtu mwenye afya nzuri anapata choo kulingana na milo anayopata kwa siku. K**a anauwezo wakupata milo mitatu kwa siku, anastahili kupata choo mara tatu kwa siku, tena choo chako kitoke na urefu sawa wa ndizi mbivu, bila kujikatakata k**a kile cha mbuzi.
_VIFUATAVYO NI MIONGONI MWA VITU VINGINE VICHANGIAVYO MTU KUPATA UGONJWA HUU WA bawasiri:_
๐ Kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
๐ Kuharisha kwa muda mrefuยท
๐ Tatizo la kutopata choo laini au kujisaidia kinyesi kigumu *(Constipation)*
๐ Umri mkubwaยท
๐ Uzito kupita kiasi (Uzito uliopindukia)
๐ Ujauzito (kwa baadhi ya wajawazito)
๐ Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu.
*DALILI ZA UGONJWA WA BAWASIRI*
โCHUKUA TAHADHARI MAPEMA, uonapo dalili hizi:
โ kuwashwa katika ngozi ya eneo la tundu la haja kubwa. Huu muwasho unakuja kwa kujirudia mara kwa mara baada ya muda fulani.
โ Kukatishwa kwa haja kubwa na kurudi ndani wakati wa kujisaidia.
โ Kuhisi kutomaliza haja (kuhisi kitu kigumu kubaki ndani) baada ya kujisaidia haja kubwa.
โ Kujitokeza kwa uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa . Uvimbe huu unaanza kuota k**a upelepele.
โ Kujitokeza kwa kijinyama katika tundu la haja kubwa. Kinyama hiki kinaanzia ndani ya tundu la haja kubwa. kikitokea nje, ujue kwamba una hili tatizo la bawasiri kwa muda mrefu.
โ Kujisaidia kinyesi chenye damu mbichi na chenye kunuka harufu mbaya sana.
โ *MADHARA YA UGONJWA HUU:*
Hebu tupitie angalau kwa uchache madhara ya bawasiri, ili upate sababu za msingi za KUCHUKUA TAHADHARI NA HATUA YA KULISHUGHULIKIA MAPEMA:
๐ฃ Kupata *maumivu makali wakati wa kujisaidia* haja kubwa na kusababisha mishipa ya sehemu ya haja kubwa kukwanguliwa.
๐ฃ Kuna uwezekano mkubwa wa kupata *saratani ya utumbo (Cancer)* kwa sababu kile kinyama kinakaa k**a kidonda
๐ฃ *Kutopata hamu ya tendo la ndoa* _kwa jinsia zote._
๐ฃ *Upungufu wa nguvu za kiume* kwa mwanamume , ikiwemo *uume kushindwa kusimama kwa muda unaotakiwa* hivyo kupelekea kupotea kwa heshima ya ndoa.
๐ฃ Kuathirika *kisaikolojia*
๐ฃ *Kutojiamini/kutokuwa na amani katika hadhara ya watu* kutokana na adha zake ikiwemo ile ya kujikuna kutokanako na kuwasha kwa ngozi ya eneo la tundu la haja kubwa (puru).
๐ก *JINSI YA KUJIEPUSHA (Kwa wewe usiyenalo bado KABLA HALIJAKUPATA) NA KUDHIBITI (Kwa yeye aliye tayari analo) TATIZO HILI LA BAWASIRI:*
๐๐ฝJitahidi kupata mlo kamili kila siku. Tumia _matunda na mboga za majani kwa wingi (kila mlo)_,
๐๐ฝ Kunywa maji ya kutosha. _Angalau lita 3 kwa siku_ (kulingana pia na uzito wako),
๐๐ฝ Epuka kukaa chooni kwa muda mrefu,
๐๐ฝJifunze mkao sahihi & salama wa kutumia Choo cha kukaa ili kujiepushia na tatizo hili,
๐๐ฝJiepushe na vilevi,
๐๐ฝ K**a usafishavyo mwili wako mzima kwa kuoga, tena zaidi ya mara moja kwa siku, _Jenga pia utaratibu wa kusafisha ndani mwili wako mzima_ kwa kutumia program za kilishe za kusafisha mifumo ya mwili mzima yaani *Whole Body Cleansing Program*, na _*hii huhusisha na usafi wa mfumo mzima wa usagaji chakula)*_
ili utoe taka mwili zote _*(zikiwemo za utumboni),*_ na uondoe sumu mwilini. Hii huepusha sana tatizo hili.
(Wasiliana nasi kwa uhitaji wa program hii ya kusafisha mwili mzima, kuondoa sumu na kupunguza mafuta mwilini), *UKIHITAJI!*
๐ก *MATIBABU:*
Ugonjwa huu unatibiwa kwa namna mbalimbali kuu zikiwa za kihospitali ambapo kuna upasuaji (surgical operations) na kwa dawa bila upasuaji. Pia zipo za kiasili/kijadi (Traditional).
โ *NB:* Una dukuduku, swali au jambo lolote kuhusu tatizo hili au tatizo lingine lolote la kiafya? au umesumbuka/ kuna ambaye amesumbuka na kuutibu ugonjwa huu, _*kwa muda mrefu,*_ kwa njia hizo pasi mafanikio ya kuumaliza kabisa? au umekuwa ukijirudiarudia.
Utapata majibu/Utasaidika/Atasaidika maana kuna suluhu nyingine ya kudumu, salama na ya hakika ya hilo la bawasiri na mengine pia.
Kwa msaaada na ushauri piga +255758112230
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Mwanza
112230