BINA TV
14/06/2026
simba sc wamefanikiwa kuonesha ukubwa wao mbele ya pamba jiji kwa kuibuka na ushindi wa 2:1
Kundi la muziki wa Hip Hop nchini WABETI limetambulisha rasmi wimbo wao mpya unaoitwa “Kausha”, wimbo uliowashirikisha nguli wa Hip Hop Tanzania Juma Nature, P Mawenge, pamoja na Skwiza.
Wimbo huo kwa sasa unapatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali ya kusikiliza muziki, ukiwa umebeba ujumbe mzito unaogusa maisha ya kila siku. Wakizungumza na waandishi wa habari, WABETI wamewataka mashabiki na wadau wa muziki kuusikiliza kwa makini ili kupata maudhui na ujumbe walioukusudia.
Kwa upande wake, Juma Nature amelipongeza kundi hilo kwa nidhamu, kujituma na uelewa wao mkubwa wa muziki wa Hip Hop. Amesema sifa hizo ndizo zilizomshawishi kukubali kushiriki kwenye wimbo huo, akieleza kuwa anaamini WABETI wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Mwanza
NONE