Sports extra large
25/06/2025
Ubaya ubwela
15/01/2025
Nyota wa Yanga wanatakiwa kuongeza umakini wakati wakipambania ushindi, Jumamosi katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger kutokana na rekodi ya ajabu ya mwamuzi, Patrice Milazare kutoka Mauritius 🇲🇺 ambaye anatarajiwa kuamua mchezo huo.
Katika michezo mitatu aliyoamua msimu huu, rekodi ya Milazare ni ya kutisha, hakuna timu yoyote iliyofunga bao, hivyo kocha wa Yanga, Sead Ramovic na vijana wake wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanabadilisha rekodi hiyo kwani uhitaji wao wa kushinda ni mkubwa kulinganisha na wapinzani wao MC Alger hata sare inawabeba.
Katika michezo aliyochezesha msimu huu, Milazare aliongoza mechi mbili muhimu za kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, Oktoba 10, 2024, Ghana walikuwa wenyeji wa Sudan matokeo yalikuwa 0-0.. Mwezi mmoja baadaye, Milazare alichezesha mechi nyingine kati ya Libya na Benin matokeo 0-0.
Mchezo wa tatu wa msimu huu kwa Milazare ulikuwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, na MC Alger walicheza ugenini dhidi ya TP Mazembe huko DR Congo. Katika mechi hiyo, hakuna timu iliyofunga bao na mechi hiyo ilimalizika 0-0.
Kulingana na rekodi za mwamuzi huyo, kila hatua itahitaji umakini wa ziada ili kupambana na si tu wapinzani wao MC Alger, bali pia na mwamuzi huyu ambaye ni k**a vile ‘mfalme wa suluhu
25/12/2024
Nimeanza kuelewa kwanini Yanga waliwakomalia Widad Casablanca.
Ukweli ni kwamba Mzize ni mchezaji mwenye thamani kubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Mzize anacheza K**a right-winger,Left-winger na number 9.
Mzize anakupa kasi,mashuti,pressing,magoli na nguvu ya kukimbia k**a kichaa uwanjani…..siyo kila mchezaji ana mapafu k**a Mzize.
Leo kaweka goli la 5 la NBC Premier League.
Ni basi Watanzania tumeamua kuwasifia akina Dube,Ateba na Mukwala Ila Mzize ni mshambuliaji bora mzawa kwa sasa.
Msimu huu ametulia sana mbele ya goli….na tukumbuke huyu bado ni kijana Wa miaka 20
Anaandika Mchambuzi wa Michezo kutoka Crown FM, Hans Rafael.✍️
25/12/2024
🚨⚠️Haitochukua muda Wananchi wataanza tena kurejea ule mpira wao na mabao yao, haitochukua muda kabla Clement Mzize aanze kupokea ofa nyingi huko nje, haitochukua muda kuanza kutenganisha maji na mafuta, haichukui muda kugundua Prince Dube kamba zote hajafunga penati, haitochukua muda timu zitaanza kuitwa Matawi.
K**a hii hali itaendelea haitochukua muda jina la GSM na udhamini kuanza kuwa kiitikio kwenye ule wimbo maarufu, haitochukua muda kusikia Marefa na TFF wote ni Wananchi, haitochukua muda sana😀
Click here to claim your Sponsored Listing.