ANIRA Health Services

ANIRA Health Services

Share

12/01/2026

Happy revolution day everyone

25/12/2025

Merry Christmas…. eat well stay healthy!!
Better life better health.

13/12/2025

Ukifika Anira, unatoka salama 💚
Asante kwa kutuamini.

Photos from ANIRA Health Services's post 12/12/2025

Good news‼️🚨Melela, Vianzi & Kibaoni! 🔥 Anira Pharmacy imefunguliwa — dawa & huduma bora zote zipo hapa!

15/10/2025

Malipo yote yanafanyika kwa Urahisi sasa

31/08/2025

KWANINI? UTI imekuwa ikikurudia mara kwa mara!
• UTI sikuhizi imekuwa ngumu kutibika kwa dawa za kawaida au ikijirudia mara kwa mara baada ya matibabu.
• Hii ni kwasababu bacteria wamejifunza kupambana na dawa ambazo tumekuwa tukizitumia kwa muda mrefu (Antibiotics).
• Tafiti zinaonyesha kuwa nusu ya bacteria wanaosababisha UTI kwa Tanzania wanausugu au uwezo wa kuzizuia dawa za kawaida mfano k**a Amoxicillin na Ciprofloxacin. Usugu wa dawa (antibiotics) ukiwa ni 61%.
• Hii inamaanisha wanauwezo wa kuzaliana na kuendelea kuishi hata k**a ukifanya matibabu.
• Na wana uwezo wa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwenye familia mahospitali au kwenye jamii.

NINI KINASABABISHA BACTERIA WATENGENEZE USUGU WA DAWA?
• Matumizi ya kuzidi ya dawa(antibiotics), watu wananunua na kutumia dawa bila vipimo au ushauri wa daktari.
• Kushindwa kumaliza dozi, watu wengi hutumia dawa nusu na kuacha bila kumaliza dozi k**a walivoelekezwa na wataalamu wa afya na kusababisha bacteria wawe na usugu wa dawa hio.
• Matibabu yasiyo sahihi, kutumia dawa (antibiotics) kwa kutibu magonjwa yasiyo sahihi, mfano yanayosababishwa na virusi mfano Mafua au hata kifua.
• Kuathiriwa na hospitali, kulazwa mara kwa mara na kutibiwa na antibiotics mara kwa mara pia kunatengeneza usugu wa dawa kwa bacteria.

NINI UNATAKIWA UEPUKE?.
• Kununua madawa(antibiotics) bila vipimo au ushauri wa daktari
• Kutumia mabaki ya dawa(antibiotics) nyumbani au za rafiki pale tu ukiwa unajisikia homa au tatizo lolote la kiafya.
• Kuacha kunywa dawa k**a ulivyoelekezwa na mtaalamu wa afya pale baada tu ya kupata mafuu(kuto maliza dozi).
• Kuhimiza matumizi ya dawa(antibiotics) kwa kila homa au mafua bila vipimo au ushauri wa daktari.
• Usafi duni, kushikiria mkojo kwa muda mrefu, kutojisafisha baada ya tendo la ndoa, Kurudia nguo ya ndani chafu, usafi wa vyoo, na kwa wanawake usafi na kuzingatia afya hasa wakati wa hedhi.

JINSI GANI UNAWEZA ZUIA UTI?
• Kunywa maji mengi.
• Nenda haja ndogo baada ha tendo la ndoa (Kukojoa).
•Zingatia usafi na ukavu, epuka kuvaa nguo za ndani mbichi au zilizo chafu.
• Usafi wako na wa chooni. Wanawake wanatakiwa wajisafishe kutoka mbele kwenda nyuma baada ya haja.
•Zingatia mlo, mlo kamili unasaidia kuongeza kinga ya mwili.
• Fanya vipimo, Jitibu kwa vipimo na sio kwa kuhisi.
• Maliza dozi yako kikamilifu, hata k**a unahisi umeshapata nafuu.

K**A JAMII:
WAZAZI; tunzeni dawa vizuri na mtumie kwa ufasaha.
WAHUDUMU WA AFYA; Pima kwanza, tibu kwa akili na ufasaha.
JAMII; Sambaza elimu hii kwa ndugu jamaa na marafiki na sio dawa(antibiotics).

Leo hii maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) yamekuwa magumu kutibika kwa sababu ya usugu wa dawa (antibiotic resistance) lakini tukibadilisha tabia, kufanya vipimo kabla ya kutumia dawa, na kutumia dawa kwa uangalifu, tunaweza kulinda afya yetu na vizazi vijavyo.

KARIBUNI ANIRA HEALTH SERVICES KWA VIPIMO NA USHAURI.

14/06/2025

Know the signs, avoid the risks. Get tested today. 💬
Karibuni Anira medical lab upate vipimo mapema.

24/10/2024

Tangazo Muhimu: Uchunguzi wa Kisukari na Shinikizo la Damu Bure Jumamosi Hii!

Habari wapendwa,

Tunafurahi kuwataarifu kuwa Jumamosi hii, tarehe 26 October, tutakuwa na tukio maalum la uchunguzi wa magonjwa sugu ya kisukari na shinikizo la damu, bure kabisa!

Hii ni fursa ya kipekee kwa wale wenye magonjwa haya au wanaoshuku kuwa nayo kupata uchunguzi na ushauri wa kiafya bila malipo. Lengo letu ni kuwasaidia watu wengi zaidi kujua hali ya afya zao na kupata msaada unaohitajika.

📍 Tarehe: Jumamosi tarehe 26 October
📍 Muda: Kuanzia saa 2 asubuh
📍 Mahali: ANIRA MAABARA KOLOLO

Tafadhali tusaidie kusambaza neno hili kwa watu unaowafahamu ambao wana kisukari au shinikizo la damu ili waweze kufika na kupata huduma. Afya yao ni muhimu, na hii ni nafasi nzuri ya kuchukua hatua!

K**a una maswali zaidi, usisite kutuuliza hapa au tutumie ujumbe moja kwa moja. Tunatarajia kuwaona wengi wenu!

Asante sana na tuzidi kusambaza ujumbe huu kwa jamii yetu. 🙏

Karibu Sana!

24/10/2024

“Je, Unapata Maumivu ya Tumbo Baada ya Kula? Hizi Ndizo Sababu na Vyakula Unavyopaswa Kuepuka!”

VYAKULA VYA KUEPUKA KWA WENYE VIDONDA VYA TUMBO
K**a una vidonda vya tumbo (peptic ulcer), lishe bora ni sehemu muhimu ya kuzuia maumivu na kuongeza kasi ya uponyaji. Vidonda vya tumbo hutokana na ukuta wa tumbo kuwa na kidonda kinachotokana na asidi nyingi au maambukizi ya H. pylori.
Vyakula unavyokula vinaweza kusaidia au kuzidisha hali hii. Hapa kuna vyakula unavyopaswa kuepuka na kwa nini:

🚫 Vyakula vya Kuepuka:

1. Vyakula Vyenye Viungo vikali (K**a Pilipili):
Viungo vikali k**a pilipili vinaweza kuwasha na kuongeza maumivu kwenye utumbo wenye vidonda. Viungo hivi vinaweza kusababisha ongezeko la uzalishaji wa asidi tumboni, na kufanya kidonda kibaki wazi zaidi au hata kuongezeka.

2. Vyakula Vyenye Mafuta Mengi (Chipsi, Kukaangwa): Vyakula vya mafuta mengi, k**a vyakula vya kukaangwa, hushushwa/kumeng’enywa tumboni polepole. Hii inaweza kusababisha uzalishaji wa asidi kuendelea kwa muda mrefu, kuongeza nafasi ya asidi kuchoma vidonda tumboni na kuleta maumivu makali.

3. Pombe:
Pombe huchochea uzalishaji wa asidi tumboni na inaweza kuchoma ukuta wa tumbo, hali inayoweza kuongeza ukubwa wa vidonda au kuzuia kupona kwake. Pombe pia inaweza kuwasha zaidi maeneo yenye kidonda tayari.

4. Vinywaji Vyenye Kafeini (Kahawa, Chai, Soda):
Vinywaji hivi vina kafeini ambayo huongeza asidi tumboni na inaweza kusababisha maumivu kwa wale wenye vidonda. Kafeini pia huchangia kuvuruga mfumo wa usagaji chakula na kuleta hisia za kichefuchefu au kiungulia.

5. Chokoleti:
Chokoleti sio tu ina kafeini, bali pia ina viambata vingine vinavyoweza kuchochea kutolewa kwa asidi zaidi tumboni. Hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa maumivu na kufanya hali ya vidonda kuwa mbaya zaidi.

6. Vinywaji vya Soda na Maji ya Gesi:
Vinywaji hivi vina gesi ambayo inaweza kusababisha kuvimba kwa tumbo (bloating), hali inayoweza kuathiri jinsi tumbo lako linavyosikia na kuongeza uzalishaji wa asidi, ambayo hufanya vidonda kuwa vikali zaidi.

🚶‍♂️ Badala Yake, Kula Vyakula Hivi vya Afya:

-Matunda Yasiyo na Asidi (Ndizi, Maembe):
Matunda haya ni laini na hayana asidi nyingi, hivyo yanaweza kusaidia kutuliza tumbo lako bila kusababisha maumivu ya vidonda.

-Maji:
Kunywa maji mengi husaidia kusafisha asidi tumboni na kuboresha usagaji chakula. Pia, maji husaidia kuweka tumbo katika hali ya unyevu, ambayo ni muhimu kwa afya ya utumbo.

-Mboga zisizo na Viungo Kali (Spinach, Broccoli):
Mboga hizi zina virutubisho muhimu na haziwashi tumbo. Zinaweza kusaidia kuimarisha mfumo wa kinga na kusaidia utumbo kupona haraka.

-Nafaka Nzima (Oatmeal, Ugali wa Dona):
Nafaka hizi husaidia kuweka tumbo lako likiwa sawa kwa kuwa zina nyuzinyuzi nyingi, ambazo husaidia kusaga chakula kwa urahisi na kupunguza kiwango cha asidi tumboni.

KUMBUKA:
Lishe sahihi ni muhimu sana kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo. Unapozingatia vyakula vya kuepuka na kula vyakula vyenye afya, unaongeza nafasi ya kupona haraka na kuzuia maumivu makali zaidi. Kwa ushauri wa kitaalamu zaidi na huduma za uchunguzi wa afya, wasiliana nasi kwa 0710391261/0712181427 au tembelea ANIRA MEDICAL LABORATORY !

Afya Yako, ni kipaumbele chetu 🍀

24/10/2024

Karibu kwenye Ukurasa Rasmi wa ANIRA HEALTH SERVICES
Habari na karibu sana! Tunafurahi kukuona hapa kwenye ukurasa wetu rasmi ambapo tutakuwa tukishirikiana kwa karibu kuhusu huduma zetu za kiafya na habari muhimu zinazohusu afya yako na ya wapendwa wako.

🎯 Huduma Tunazotoa:

• Uchunguzi wa afya kwa magonjwa mbali mbali
• Vipimo vya maabara vyenye usahihi mkubwa.
• Ushauri wa afya na matibabu bora zaidi.

Tutakuwa tukishirikiana:

• Vidokezo vya afya ya kila siku.
• Elimu kuhusu magonjwa mbali mbali na ya kudumu na jinsi ya kuyadhibiti.
• Habari za huduma mpya tunazoanzisha na matangazo maalum.

Tutumie ujumbe moja kwa moja k**a unahitaji huduma yoyote au k**a una maswali kuhusu afya yako. Tunajali sana afya yako, na tuko hapa ili kukusaidia kufikia maisha yenye afya bora!

Asante kwa kujiunga na sisi – pamoja, tunaweza kufanya afya bora iwezekane kwa kila mtu!

Tafadhali like na follow ukurasa wetu ili upokee habari zote muhimu na matangazo maalum. 🙌

Want your business to be the top-listed Beauty Salon in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Melela Kololo
Morogoro