TSCA
01/01/2021
Kheri ya Mwaka mpya, ukawe mwaka wa Mafanikio, Furaha na Amani.
28/12/2020
unaifahamu BROKOLI??, hii ni mboga na wachache sana wamewahi itumia , , , twende pamoja sasa👇👇👇👇👇👇👇👇👇
wataalamu wanasema kwamba ni moja ya mboga rahisi mno kupanda, hustawi vizuri maeneo yasiyopokea kiwango cha mvua ya kuikidhi, mfumo wa kunyunyizia mimea maji kwa mifereji utafanikisha kilimo chake, kwakua Brokoli zinahitaji maji mfululizo ili kuzinawirisha na kupata mazao bora,
upandaji wake👇👇
Brokoli hupandwa mbegu moja kwa moja au kupitia miche. Aidha, miche inachukua karibu muda wa wiki sita kitaluni. Matunzo yake yanawiana na ya kabichi au mboga zingine zinazopandwa kupitia miche.Watalaamu wa masuala ya kilimo wanashauri kuweka madini mengi ya Nitrogen na Potassium. Mkulima anahimizwa kabla ya kupanda, aweke mashimo mbolea hai kwani imesheheni Nitrogen, Phosphorous na Potassium. Inapaswa kuwa iliyoiva sawasawa,(decomposed).
Palizi ni shughuli muhimu katika kilimo cha brokoli. k**a ilivyo kwa kabichi, brokoli pia hushambuliwa na wadudu k**a viwavi
zao hili huanza kuvunwa kati ya siku 45 – 60, baada ya kupandwa.
FAIDA👇👇👇
√ Brokoli ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fibre) ambazo ni muhimu katika kusaidia mmeng'enyo wa chakula mwilini.
√ hupunguza kiwango cha mafuta ya cholesterol.
√ Virutubisho vingine ni Vitamini C, Protini, Potassium na Calcium; madini yanayosaidia kuimarisha mifupa.
√ pia, Wenye shida ya ugonjwa wa Kisukari, wanahimizwa kula brokoli kwa wingi kwani huudhibiti.
Naamini tutakua tumejifunza machache na ya msingi juu ya huu mmea au mboga BROKOLI
Click here to claim your Sponsored Listing.