Simulizi Zetu
31/12/2025
KEITH - MR ROMANTIC*
*__________________________________________*
*SEHEMU YA KUMI NA MOJA*
Basi wikiendi ikafika salama Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumapili. Nilivaa gauni refu jekundu, lina mpasuo pembeni lilinikaa poa ajabu.
Kwa kweli nilikuwa nimependeza sana. Nilipojiangalia kwenye kioo nikagundua mimi ni pisi kali ni kwa vile Jua la bushi lilipausha sana
Baada ya kumaliza kujiandaa, nikatoka. chumbani nikamkuta Keith ananisubiri sebuleni.
Aliponiona mara ya kwanza alishtuka akawa k**a amepigwa na butwaa. lla ghafla tu mood yake ikabadilika akanikunjia sura
"Unaonaje, nimependeza eeeh??" Nilimuuliza kwa nia nzuri tu jamani
"Umependeza but sijui k**a umependeza ivi coz tunaenda kwa Aunt au kwakua unajua Rico atakuwa pale
Nikashangaa "Unamaanisha nimependeza hivi kwa sababu ya Rico?
"Au nimekosea??"
"Kwani Keith Ni kosa kupendeza?? Pia mbona story za Rico tulishamaliza Na mimi sina mda nae kabisa
"Usinielewe vibaya ila Sitaki watu ambao
hawana hatia waumie"
"Watu k**a nani?"
"Watu k**a K**a Maya. Anampenda Rico sana
"Atauumiaje sasa? Nachojua Mimi sifanyi chochote kibaya na Rico. Tumeenda tu kwa sababu wametualika. Na pia ulisema umewa miss Aunt na Uncle unataka kuwaona. Tatizo
liko wapi?"
Hakusema chochote, Alisimama, akachukua funguo za gari akatoka nje hata hakusema Twende. Ilibidi nijiongeze nimfuate nyuma nyuma lasivyo angeondoka aniache
Mnajaua Nikaanza kujiuliza, Kuna nini kinaendelea? Kwa nini ananifanyia hivi?" Ghafla
tu anaanza kuwa k**a mume mwenye Gubu
Au pengine Keith ananipenda? Namna anavyofanya inaonekana kabisa ana wivu. Weeh sikutaka kuamini ila nilijikuta nimefural.
Sio siri hata mimi kuna namna nahisi ninapo kua na Keith. Sijui ni mapenzi au vipi lakini sichoki kumtazama, kumsikiliza mpaka mda mwingine
hadi namwota
Nikajisemea ikitokea k**a Keith atanitongoza
wallah sikatai. Apo najiliwaza ndani ya moyo nikasahau kabisa nina mimba ya mtu mwingine, Ila mimi
Haya Tukafika nyumbani kwa Rico. Tulikaribishwa vizun, lakini baba yake Rico alikuwa safarini. Nyumbani kulikuwa na mama.
yake, Maya na Rico mwenyewe.
Mama Rico aliponiona alishangaa
"Huyu ndiye yule binti wa kijijini?"
Keith akajibu "Si binti kijijini Ana jina lake
Aunt, Anaitwa Lola"
"Amebadilika sana, now kawa mrembo. Ni umaskini tu ndio ulikuwa unamharibu binti wa watu. Angalia alivyo mrembooo...
Maya akaongezea
"Ndiyo si nilikuambia, Lola ni mrembo mno
Walinisifia pale hadi nikaona aibu nikawa
natizama chini tu.
"Sol Mnaendeleaje Kelth? Hujaja kwangu siku nyingi utadhani tuna ugomvi? Mama Rico
alilalamika
"No Aunt si unajua nina jukumu kubwa la Lola! So most of the time nakua busy ofisini, busy
nyumbani but hakuna kilicho aribika! Am sorry
kwa kufanya uni miss sana" alijibu Keith
"Naelewa dr, uzuri leo umekuja No problem So
k**a hamtajali acha niende na hawa warembo jikoni then nyie mka relax huko nje mkisubiri
msosi Mama Rico alituchukua mimi na Maya tukaenda jikoni kwaajili ya kuandaa mapocho pocho
Tukiwa jikoni niligundua mama Rico alikuwa
ananijali sana tofauti na siku ya mwanzo.
Alikuwa mpole mwenyewe nikahisi k**a
ameanza kunipenda
"Usiniogope Lola mimi sing'ati! Najua labda ni kwa sababu ya nilichosema mara ya kwanza
ulipokuja, sometimes mdomo wangu hauna break ila please usiniogope okay??"
Nikajibu "sawa Mama hakuna shida"
"Haya Tupike nini leo?"
"Pilau nyama, kachumban, chips na rosti la kuku alidakia Maya
Mama Rico akacheka "Vyote hivyo?
Maya akasema "Ndiyo, leo ni siku special familia
nzima ipo hapa
"Okay hakuna shida kipenzi tutapika vyote ivyo
Basi Tukaanza heka heka za kupika, ajabu Maya
aliondoka akaenda sebuleni kuchezea simu. Mama Rico hakupenda lakini hakusema.
chochote ili tu asije kukwazana na Maya.
Jikoni Tukabaki mimi, mama Rico na
wafanyakazi wawili waliokua wanatusaidia. Tulikuwa tunacheka na kupiga storil Kale ka
moment kalikua kazuri mno
Mda huo huko Nje upande wa Garden, Keith na
Rico walikuwa kimya kila mmoja na simu yake.
Toka walipandishiane kule restaurant kila mmoja
alikua kamkaushia mwenzake.
Rico alipoona hakuna cha kuongea, akaona ni
heri aje jikoni kuchukua angalau kinywaji. Lakini kabla hajafika jikoni alimuona Maya kakunja nne
sebuleni Akamfuata
"Babe Mmeshamaliza kupika?"
"Me Sijul, Nadhani itakua bado"
"K**a bado hawajamaliza, mbona uko hapa?"
"Unajua sipendi kupika pika nimewaachia wenyewe huko jikoni
Rico akakasirika "Angalau ungeenda kuwasaidia au ukae nao muongee. Hivi unajitenga unadhani
ni sawa?"
"Rico, siwezi hata kukaa kwa amani nyumbani
kwa wakwe wangu? Mama yako hajasema chochote also mimi sio housegirl hapa"
"What??? Maya.. please embua acha drama.
zakol Najua kabisa Mama hajapenda
"K**a hakupenda angeniambia. So please
niache"
Rico hakujibu Akampita akaja mpaka jikoni. Alipofungua mlango, akatuona tukicheka na
kufurahia.
All enjoy kuniona nipo nimejiachia sana na
mama yake. Akatamani ningekuwa mkwe pale
maana nilipatana na mama ake kushinda hata
huyo Maya
Akahairisha kuchukua kinywaji badala yake.
akaenda chumbani kwake na kukaa kitandani.
"Nimefanya nini sasa?? Best wife ni Lola na nilifanya makosa sana kumpuuzia. Najuta hata
kwanini nilipoteza mda wangu kwa Maya...! Daaahinabidi nifanye kitu ili nimpate Maya.
tena lasivyo Keith atanizidi kete"
Rico akawaza kidogo kisha akatoa simu yake, akatafuta namba aliyo isave k**a Patricia,
akaipiga.
Simu ikaita mara mbili then ikapokelewa na Sauti nyororo ya k**e.
"Ah Rico shemeji angu, Inaonekana umeni miss
sana
Rico akasema "Ndiyo, nimekumiss kinomal Unarudi lini?"
"Sijui. Niko bize sana na biashara yangu inaenda vizuri
"Mhhh hongera! Na Vipi kuhusu Keith?"
"Mimi na Keith tuliachana au ulisahau. Nilichagua kazi badala ya kuolewa na yeye
"Lakini bado unampenda
"Ofcourse, Na yeye pia ananipenda. Keith hawezi kumpenda mwanamke mwingine zaidi yangu"
akacheka
"Mambo yamebadilika sasa. Keith anaanza kumpenda mwanamke mwingine"
Patricia akasema kwa mshangao "Nini?
Impossible
"Ukweli ndo huo! Ukichelewa, utamkuta ameoa"
"My God kwanini lakini! Daah so inabidi nirudi haraka lasivyo itakula kwangu! Thanks Rico kwa
taarifal Byeee Patricia akakata simu na kumfanya Rico atabasamu.
Mpango wake ulikuwa kumrudisha ex wa Keith
ili kuharibu kila kitu. Rico alijua Keith alimpenda
Patricia sana.
Walikuwa wanapendana sana na Keith alikua
tayari kumuoa Patricia ila siku moja kabla ya harusi Paticia akapata taarifa kuwa kapata kazi huko Paris ya mitindo.
Kwaiyo harusi ikavunjika Patricia akaenda Paris akimuacha Keith na maumivu. Wallachana
Japo inasemekana bado walikua wanapendana.
Na Patricia alisema akishamaliza kazi zake zote huko Paris atarudi Tanzania kwaajili ya Keith.
Alikua na confidence kuwa hata akimpigia Simu Keith usiku wa manane akiomba warudiane
Keith hawezi kukataa. Yooh nimekwisha mimi
Unajua kitakachofuata? Nakuja
Chapters
Full 1000
Whatsp 0784468229
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Mbeya