psb_designs_architectural
11/06/2023
Mtozi na Mwanagezi sikuwa Mbali na Utalii huu.
11/06/2023
Royal Tour Mkoa wa Mbeya na Rc Juma zuberi Homera, Wilaya ya Kyela iliyofanyika na Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Mbeya tarehe 10 Juni 2023, imeleta Hamasa ya kuvitangaza Vivutio vyote vya Utalii vilivyopo Katika Mkoa wa Mbeya.
Imetolewa na Kitengo cha Tehama Wilaya ya Kyela.
Architect Technologist: Paul Biswalo (Mkuu wa Kitengo).
12/04/2023
Tamati ya Wiki ya wazazi Mkoa wa Mbeya kwa wilaya ya Mbeya Mjini ni Tarehe 13 April 2023. Karibu ujumuike Nasi kuwafariji na kuwapatia Mahitaji Watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu na Wenye Mahitaji Maalum.
Kwa Wilaya ya Kyela ni Tarehe 14 April 2023. Karibu ujumuike nasi katika Kusaidia Ujenzi wa Kituo cha Afya kinachojengwa Kata ya Makwale -Ngeleka, Maendeleo yanajengwa na Wananchi kwa kushirikiana na Serikali.
Imetolewa na;
Architect Technologist: Paul Biswalo.
Afisa Tehama Jumuiya Wazazi Mkoa,
Mkuu wa Idara ya Tehama.
13/03/2023
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya kikiwa kwenye Ziara na Kamati Ya siasa Mkoa wa Mbeya Wilayani Kyela, kukagua na kuangalia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020 - 2025 jinsi unavyotekelezwa ili kuwaletea Wananchi Maendeleo kwa wakati, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Ndg. STEPHEN ISAAC MWAKAJUMILO akiongoza Kamati hii ya Siasa ya CCM Mkoa Mbeya, alitoa maelekezo mbalimbali kwa Serikali ambayo ndio inatekeleza Miradi hii kuhakikisha wanafanya kazi kwa Ubora na Ufanisi mkubwa huku wakitakiwa kukabidhi Miradi hii kwa wakati ikiendana na Thamani ya Pesa iliyotumika. Mwenyekiti alifanya Majumuisho tarehe 12 Machi 2023 na Watendaji wote wa Serikali Wilaya ya Kyela ambao ndio watekelezaji wa Miradi hii na kuwaeleza kuwa wanatakiwa kufanya Kazi zao kwa Moyo ili kuhakikisha Fedha zinazoletwa na Mh.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zinafanya Kazi k**a jinsi alivyokusudia na si vinginevyo. Kwa kuhitimisha ziara hii Mwenyekiti aliwashukuru Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya kwa Kusimamia Maendeleo Yanayofanyika katika Wilaya yao na kuwataka kuwa wamoja kwenye Miradi yote inayotekelezwa ili kuifanya kuwa na viwango Bora kutokana na Umakini wao wa kushiriki pamoja na serikali kutekeleza.
Imetolewa na Idara ya Tehama.
CCM Wilaya
Kyela.
Arch-Tech; Paul Biswalo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mbeya