Ishi Njozi

Ishi Njozi

Share

22/03/2023

Sehemu Ya Pili,

*Huu Ndiyo Ushauri Ikiwa Unataka Kufikia Lengo Lako*

Na wakati Fulani unafikiria kuwa umelogwa?

Hapana,

Ila Huenda sababu ipo hapa,

Unalengo kubwa sawa...

•Matendo Madogo Madogo unayofanya sio ya kukufanya ufikie Lengo lako,

•Aina ya watu ulio nao karibu Ni wale wanaokuridisha nyuma Bila ya wewe kujua,

•Hauna watu maalumu ambao unataka kujifunza kutoka kwao,
n.k

Sababu zaweza kuwa nyingi,

Jiulize swali Hili kwa kila unalofanya,

"Je hili ninalofanya sasa litanisaidia kufikia Lengo langu?"

Na uzuri wa sheria hii Ni kwamba,

Waweza badilisha Mambo leo,

Ambayo yatakufanya ufikie hatma yako,

Fikiria Sasa kwa Nini unakwama?

Lazima Kuna sababu fulani,

Unapoanza wiki hii fahamu sababu zinazokufanya ubaki hapo hapo Bila kufikia Lengo lako,

Umejifunza kitu hapa?

Umeelewa?

Usisite kunitumia Ujumbe,

Mpaka Wakati mwingine,

@ Ishi Njozi Media.

20/03/2023

*Jinsi Ya Kupata Kila Unachotaka*

Si umewahi angalia zile movie za "Pete Ya Ajabu?"

Yaani unakuwa na Pete alafu unaiambia kila Aina ya kitu unachotaka na unaletewa,

Sasa wewe ungekuwa na nafasi hiyo ungeomba Nini Sasa?

Ni kitu gani ungesema Pete ikupe?

Bila shaka ungeomba kutoka katika Maumivu unayopitia Sasa,

Yaweza usiwe ugonjwa, Ajali n.k

Bado Kuna Maumivu unayopitia ambayo kwa namna ya kawaida huwezi kusema,

Hivi unajua hata wewe unayo Pete ya namna hiyo?

"Unasema Nini?" Najua ndivyo unavyoniuliza,

Narudia Tena,

"Pete Ya Ajabu Hata Wewe Unayo"

Nina sema Pete ya namna hiyo unayo yaani uwezo wa kupata kila unachotaka upo,

Kwa sababu Nyenzo muhimu ya kukufanya upate unachotaka unayo,

Nayo Ni....

*Akili Yako*

Huo ndio ukweli halisi,

Sasa ili,

Ili uweze kila kitu unachotaka fanya hivi...

Hizi Ni hatua tatu ambazo unatakiwa kuzifuata,

1. Angalia tatizo unalopata.

Wewe unapitia tatizo gani?

Ni jambo gani ambalo ukilifikiria kuna wakati unashindwa la kufanya?

Maumivu gani unayahisi Sasa?

Hakuna haja ya kufikiria kwa sababu unajua Hali ya sasa.

2. Weka picha ya mbele baada ya kushinda yaani kufanikiwa,

Yaani ona katika Akili yako ukiwa umeshinda tatizo ambalo unapitia,

Ona ukiwa hauna Maumivu Tena.

Tayari?

3. Pumzika kwa amani ya kwamba limetokea,

Hivi unapokuwa una shida ya kiasi fulani Cha fedha na unaambiwa kuna mtu analipa utafanyaje?

Utafurahia si hivyo?

Huo ndiyo uhalisia,

Kiufupi hatua zipo hivi,

Tambua tatizo lako, Amini limetatuliwa na Kuwa na Amani Ya kushinda tatizo lako,

Hapo si umenielewa?

Rafiki ikiwa hujanielewa basi niambie,

Kanuni hii imeandikwa na Joseph Murphy katika kitabu,

"The Power Of Subconscious Mind"

Waweza kupata na kukisoma kitabu hicho.

Nakutakia asubuhi Njema!

Njozi Media.

14/02/2023

*Benki ya ajabu...*

Tafakari hili,

Unaamka asubuhi na kuona hauna fedha,

Kisha unakumbuka kuna kiasi Cha fedha lipo benki na hivyo unapanga safari ya kwenda Kuchukua,

Ukiwa benki unashangazwa kuona Kuna kiwango kikubwa Cha fedha kuliko ulichokuwa nacho,

Yaani Ni Dola za kimarekani 86,000.

Na kwa tathmini ya haraka karaka,

Dola moja ya kimarekani Ni sawa na shilingi za kitanzania 2300/=

Haya,

86,000×2,300 = 198,720,000/=.

Ni MILION MIA MOJA TISINI NA NANE LAKI SABA YA ISHIRINI.

Unapokuwa umechanganyikiwa furaha siyo furaha, huzuni siyo huzuni,

Ndipo anakuja mfanyakazi wa benki na kukwambia,

"Kiasi hiki Cha fedha kipo Leo TU! Unatakiwa kuwekeza ndipo utapata kingine kesho, Usipowekeza utapoteza fedha zote"

Utawezaje kuwekeza fedha hiyo kwa siku moja?

Fikiria kwa sekunde tano!

1,2,3,4,5.

Unaweza kuona Ni ndoto ya abunuasi ukiambiwa hivyo...

Lakini kweli kabisa,

Kila mtu Ana,

•Masaa 24 kwa siku,

•Dakika 1440 kwa siku,

•Na Sekunde 86,000/= kwa siku.

Je huwa unatumia muda kwa usahihi,

Kuna usemi ambao huwa Ni "Time is Money"

"Muda Ni fedha"

Ila nitakwambia haupo sahihi kwa sababu hii,

"Muda hauongezeki Ni uleule kila siku, Lakini fedha waweza kupata kiasi chochote unachotaka kwa siku inategemea unatumia njia gani halali"

Hivyo chukua tahadhari,

Muda ulio nao sasa hautajirudia,

Wekeza kwa akili,

Yaani tumia muda kwa usahihi kabisa,

Najua waweza kusema Sasa kwamba

"Nitakuwa bize na Mambo yangu,sitapoteza muda"

Ninamnukuu Dan Lok huyu Ni Millionea anasema,,
"Kuwa bize Ni njia nyingine ya kuwa mvivu"

Sasa sikia,

Unakuwa bize masaa nane,Kumi,Kumi na mbili,n.k
Unafanya Nini?

Je baada ya kuulizwa matokeo utasema Ni yapi?

Maana wengi wanaosema "Niko bize" hatimaye huonekana hawajafanya kitu,

Yaani "Kuwa bize kwa hamna"

Waingereza wanasema "Busy for Nothing"

Anza Sasa tumia muda sahihi,

Naamin umejifunza kitu hapa,

Mpaka Wakati mwingine,

Njozi Media.

Want your restaurant to be the top-listed Restaurant in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address

Mbeya

Opening Hours

Monday 05:00 - 11:00
Tuesday 05:00 - 11:00
Wednesday 05:00 - 16:00
Thursday 05:00 - 11:00
Friday 05:00 - 11:00
Sunday 05:00 - 11:00