Story funzo
23/12/2025
SIMULIZI: MVUJA JASHO
MTUNZI: DANIFORDY BEN
MAWASILIANO: +255711444410
SEHEMU YA 03
TULIISHIA.
Jerinda amempeleka sofania maeneo ya fordy bar baada ya kuagizwa na mama zurufa. Je ni mzigo gani anaufikisha eneo hilo kwa ujira mrefu?
SASA TUENDELEE.
Ama hakika waghani lugha hawakukosea kusema sura siyo roho, furaha ya sofania ni kupita na kuingia sehemu ghari k**a zile ambazo aliziona kwa mbali wakati wa matembezi. Furaha yake ilimkumbusha kila muda sura ya mama zurfa ambaye kwake ama hakika alikuwa mwema kila sekunde ubongoni mwake. Hakuna hata thumuni ya kosa ingethubutu kuchafua wema wa mama zurufa kwa sofania. Jerinda alitoa maelekezo ya ishara tu kumtambulisha sofania, k**a vile wapiga debe wafanyavyo stendi kwa ile kauli yao ya kusema hii ni namba yangu nimeichora kuashiria kuwa wammpigia debe mteja. Sofania hakutambua chochote kilichokuwa kikiendelea kwake, zaidi alipewa maelekezo ya kukaa katika kiti moja wapo ndani ya saloon ile iliyojazwa nakshi haswa.
Upambaji ulianza kwa binti yule ambaye alikuwa amebuka na maisha ya ufukara, licha ya kuoga kila siku lakini haikufanya apendeze kwa muonekano wake. Hivyo ilifaa apendezeshwe zaidi ili tu kufanania na kazi aliyokuwa akiifanya. Dakika za kuhesabu muonekano wake ulianza kubadirika na urembo wake ukaanza kujidhihirisha wazi. Wakati huo jerinda alikuwa ametoka na kujipakia katika gari lake na kuondoka, kabla ya muda mchache kurejea akiwa na mifuko miwili ambayo alifika na kuiweka katika kiti kisha akawaeleza wahudumu wale kuwa ni kwaajiri ya sofania na kumkabidhi begi ambalo aliambiwa anapaswa kulilinda sana, kisha akamwambia anamsubiri garini. Punde tu baada ya kumaliza kumremba sofania akarembeka ndipo walipomkabidhi mifuko ile na kumuelekeza mahali pa kwenda nayo. Ilikuwa ni mifuko yenye nguo ghari sana, nguo ambazo alipaswa kuzivaa kwa muda huu, amahakika zilikuwa zimempendeza ila tu. Hofu ilikuwa dhidi yake kwa muonekano ule wa suruali pekee kutembea nayo maana hakuwahi kabisa kuvaa hivyo.
Ila haikuwa na namna ilimlazimu, ijapo roho yake ilikuwa ikisita sana akaihisi kuwa uvaaji huo ni nje ya maadili aliyofunzwa, sofania alitoka ndani mule akiwa mtu mwingine kabisa. Alikabidhiwa begi lake na kisha safari ikaanza kulifuata gari, hakika alibadirika haswa hali iliyomfanya mpaka jerinda kuduwazwa na muonekano ule ambao hakuwa ameutegemea kabisa.
"You look great". Alizungumza jerinda na kumuacha sofania akiwa anatabasamu tu, asijue nini maana ya kile alichokuwa ameambiwa.
Jerinda aliwasha gari na kulisogeza mita kadhaa hapa ilikuwa ni nje kabisa ya fordy bar, mahali ambapo ndipo alipaswa kuupeleka mzigo ule ambao hakuwa akijua ni nini haswa kilichokuwa ndani yake. Alipewa maelezo nini akifanya pindi aingiapo ndani mule na ni code gani azitaje, hivyo hakuwa na muda wa kusubiri alitekeleza alichoambiwa na hatimaye baada ya kukamilisha biashara ile aliyoambiwa, alitoka akiwa amebarisha lile begi la mwanzo na kuwa na jingine jeusi la lezzer, hili lilikuwa zito kiasi lakini kwa masharti aliyopewa ndivyo ilibidi afuate, hakupaswa kufungua kabisa mzigo huo. Alirudi garini na jerinda akalichapa gear kuelekea kwa mama zulfa, lakini sasa haikuwa dukani pale tena zaidi sasa mwelekeo ulikuwa nyumbani.
Mbele ya uzio mkubwa wa jumba la kifahari kulipambwa na madhari nzuri sana, juu ya kuta za fensi kulikuwa na uzio wa umeme, na kwa mbali ungetazama kwa nje jengo hili lilikuwa la ghorofa. Muda wote sofania alikuwa kimya tu akijikagua kagua namna alivyokuwa amependeza siku hii hata hakuwa na umakini wa safari ni wapi ametoka na wapi aendako. Zaidi alish*tushwa ghafla na ulio mkali wa honi, yes ni nukta chache geti likasogea upande wa kulia taratibu na gari lao likaanza kuingia ndani ya mji ule wa gharama ya juu, ughari wa jumba lililokuwa mbele ya macho ya sofania ulijaza maswali lukuki unongoni mwake, kwa ile wazawazua ninani aishiye humo ndani.
Gari liliendeshwa taratibu na kupaki upande wa kulia wa jengo hili na jerinda ndiye alikuwa wa kwanza kushuka, kabla ya sofania kufuata. Sofania kila kitu kilimshangaza hasa pale alipokuwa akishangaa geti lililokuwa likijifunga pasi kuwapo mtu, hakika kwake hii aliona k**a mi ushirikina, ila tu alikosa wa kumuuliza swali kutokana na ubusy wa muda wote kwa jerinda Walipiga hatua za taratibu kuusogelea mlango lakini kabla hawajafungua konde zito lilitua kichwani mwa sofania ambaye taratibu macho yalipoteza nuru, nguvu zikamuisha na taratibu akashuka na kutua ardhini k**a mzigo.
ITAENDELEA.
JE! nini kitaendelea unadhani na nini hatima ya mkasa huu?
Basi usikose sehemu inayofuata
15/11/2025
MTUNZI:DANIFORDY BEN
MWASILIANO: +255711444410
SIMULIZI: MVUJA JASHO.
Sifuni ni jina nililozawadiwa baada ya kilio changu cha kwanza ndani ya ulimwengu huu wa watu wa hira na wema, nakumbuka niliwahi sikia watu wakisema subira yavuta heri, na laiti ingelikuwa mtu anaweza kuona vilivyo mbele kabla ya uzao wake basi ningeomba kuzaliwa baadae na sio kwa wakati huu, na k**a tungepewa uwezo kuona mbele nadhani kuna vingi mwanadamu asingefanya ili kukwepa majuto yaliyopo mbele yake baada ya kufanya kosa, Na ile methali ya majuto ni mjukuu isingetamkika vinywani mwa watu daima. Lakini nani awezaye kugeuza jicho lake litazame kisogoni k**a kinyonga afanyavyo? Jibu hakuna ila tu tumejaliwa kuona vya nyuma baada ya kuvipita na kugeuka tuvitazame tena, na mara zote huwa vinaweza kuwa vyema au vibaya. Na k**a ni vibaya basi ni lazima utatamani upewe maaajabu ya mdudu kinyonga abadirikaye rangi aonapo hatari mbele yake, ijapo naye abadiri ubaya wake kuwa wema ili tu kurudisha imani na amani kwa walimwengu.
Jina langu linabeba uzani mkubwa wa kisichotikiswa wala kutetereshwa, nilitamani sana nifanane na ule mlima sayuni. Lakini chozi la maumivu lilininyong'onyesha kwa kushindwa kuhimiri mapito yangu. Uyatima ulinijenga kuwa jasiri wakati wa utoto, njaa haikuwa adhabu kwangu kwakuwa tayari nilishazoea mlo mmoja kwa siku kwenye maisha yale ya mahangaiko nikiwa na mama yangu, wakati tukiranda mtaani. Siku jua kuhusu A wala Be, ila nilijifunza kuokota vibuni, chuma na baadhi ya mabati ili tu nikauze ili tupate chakula. Mama yangu kuna muda tuliungana katika kazi hii, ila mara chache alipata day worker mashambani na kazi ndogondogo zilizohitaji usaidizi, hivyo aliniacha niendelee na vibuni. Kila kesho ya matarajio ilikuwa haina tofauti na jana ya bora liende.
Ni miaka michache sana ya upevukaji wangu ilitosha kujifunza vichache kutoka kwa mama yangu ambaye ndiye alikuwa baba na mama yangu, kwakuwa sikuwahi kuiona sura ya baba. Mama Hakuwahi kuniambia chochote kuhusu ndugu zangu katika siku zoye za uhai wake, zaidi nilisikia kwa majirani kuwa mama yangu alibakwa na mtu asiyemfahamu ndiyo ujauzito wangu ulipotungwa. Miaka 14 ilitosha kabisa kuishi ndani ya upendo wa mama ambaye hakupenda kuniona nalia naye akacheka, ila aliweza kulia ili tu mimi jicheke. Alikuwa tayari kulala njaa ilimradi mimi nishibe. Hivyo kwangu nilimpa heshima ya hayati, ijapo wengine waliona ni marehemu na kuna wachache walimjua k**a maiti.
Maisha ya mtaa yalinipokea na kunihifadhi ndani yake ili niyaishi. Kwa mwanzo majirani walikuwa ni sehemu ya maisha yangu ila kuna muda walibadirika na kuanza kuninyanyapaa, na hata walipoigiza kunipa msaada basi walihakikisha kuwa na ulipa kwa gharama kubwa, yenye maumivu na majuto ya kupokea msaada huo.
"Sifuni... Nipo tayari kukupa msaada wa elimu na maisha. Je upo tayari?".
Alihoji mama zurufa kwa sifuni ambaye sasa alikuwa sakara haswa kutokana na maisha yaliyomkokonya bila huruma.
"Nipo tayari mama yangu, nipo tayari na Mungu akubariki na kukuondolea dhunubu zote zilizo juu yako. Nitashukuru kwa wema huo".
Alizungumza sifuni wakati machozi yakianza kumlengalenga kwa furaha iliyotabakuru rohoni mwake. Alijikuta akihaha tu bila kujua apige goti ama abaki wima k**a mlingoti wa bendera, alikuwa akifurahia kwenda shule ambayo hata hakujua ni shule gani. Furaha iliyozunguka ndani ya roho na akili ilifanya hata njaa ikose nafasi mwilini mwake sasa alijihisi mtu alieshiba shibe ya kiwango cha juu tena yenye chakula ambacho alikipenda kula.
"Aaah sawa nipo tayari kukusaidia, ila tu ni kwa sharti moja tu! Na k**a utakubali nitakupeleka shule na pia nitakufungulia biashara yako binafsi, ili ikufae kwa mahitaji madogo madogo wakati ukiwa katika masomo yako".
Mama zurufa aliweka ukomo kiasi, kutoka katika maelekezo yake wakati huu akimeza funda zito la mate, sawia kabisa na kushusha pumzi ndefu ambayo iliashiria yajayo mdomoni mwake yalihitaji hewa nyingi ili kusukuma yatoke, wakati huo sifuni alitulia tuli kimsikiliza na ile furaha ya awali ilipungua, akibaki kumtazama mama zurufa. Mama aliyefahamika mjiji hapo kwa wengi kuwa ni mfanya biashara mkubwa wa nguo, vipodozi na pia mmiriki wa baadhi ya salon za k**e. Ni mama wa haja hasa aliyepewa urembo na umbo kubwa, muonekano na harufu yake ya marashi ilidhihirisha wazi ughali aliokuwa nao katika maisha hasa ungemkuta katika gari lake ameshika usikani, hakika usingehitaji kuelezewa kuwa yule ni mwanamke wa viwango vya juu.
"Lakini mama mimi siwezi kukusaidia vingine zaidi ya kuendelea kufanya usafi hapa kazini kwako, maana sina ujuzi mwingine wowote zaidi ya kuokota vibuni (makopo ya maji na soda), hivyo ndiyo mama yangu alinifundisha. Nitawezaje kazi nyingine na sijui hesabu wala kusoma? Harafu na muo.... ".
Alijieleza sifuni ambaye alikatishwa maongezi yake na mama yule wakati bado alikuwa na jambo la kuzungumza, msaada aliuhitaji wakati huo hofu ikianza kumuingia juu ya msaada atao upata. Ila kiroho alikumbuka neno lisemalo ogopa kupewa viatu na mtu aliyevaa kandambili. Ndani yake bado kuna nafsi ilikuwa inamsukuma kuwa bado anahitaji msaada hivyo hapaswi kuogopa changamoto.
"Tuliza munkari, nimekwambia nataka kukusaidia sasa izo fyokofyoko zinatoka wapi! Unanielezea kwani mimi sijui? Jishikilie vizuri nisije kudondosha kabla sijakaza nguo, sijui nimeeleweka..? "
Alimaliza mama yule kuzungumza. Sasa hata sura yake ilibadirika haikuwa na tabasamu tena k**a awali na kumfanya sifuni kuogopa kuzungumza zaidi ya kuwa msikilizaji wa kusubiri msaada wa mama zurufa.
ITAENDELEA.
Je! Nini hatima ya mkasa huu unadhani na nini kitaendelea kwa sifuni, msada gani anatarajia kuupata! Basi usikose sehemu ijayo.
03/10/2025
Nisikilize Mwanangu…
Dunia ya sasa imejaa watu wa hila, wasio thabiti, na wenye tabia ya kupita mbele kwa kudanganya. Mwanangu, usidhani kila kicheko ni kweli, kila maneno ni ya dhahiri. Kuna wengine wanaonekana wema ili wakutaplishe, wawe na faida kutoka kwako, na kuondoka bila heshima.
Mwanangu, hekima yako ni silaha kubwa zaidi. Ukiishi kwa kuamini kila mtu anayeonekana mzuri, utapoteza heshima, pesa, muda, na wakati mwingine hata ndoto zako. Usikubali uongo wa wengine ukudanganye. Kujua kusoma tabia ya mtu ni ulinzi wa thamani zako.
Nisikilize vizuri mwanangu… Hakuna mtu anayekutumia vizuri k**a wewe mwenyewe. Hila na uongo wa wengine ni mwanga wa haraka – huanguka k**a jua linapochomoza na kuanguka. Lakini nidhamu, hekima, na ujasiri wako ni nguzo thabiti ambazo hazitazidishwa na dhoruba yoyote.
Mwanangu, fanya kila uamuzi kwa akili na moyo wako. Usikimbilie starehe za muda mfupi, mapenzi yasiyo thabiti, au mashindano yasiyo na maana. Hili ndilo somo kubwa la maisha ya sasa: dhahiri sio kila kitu kilicho mbele yako ni kioo cha kweli. Angalia ndani, hakikisha kila hatua unayoichukua ina maana halisi.
Mwisho, nisikilize tena mwanangu… Hila za wengine ni changamoto yako. Ukiweza kudumisha nidhamu, hekima na moyo thabiti, hakuna uongo wa mtu mwingine utakayekuondoa kwenye nafasi yako ya heshima. Dunia ya sasa inamheshimu yule anayejua thamani yake, anayesimama imara, na haachii mwingine akumwangamize.
🗣️Kikao kimeisha Mwanangu… sasa ni juu yako kulifanyia kazi somo hili. Usisahau kufollow channel yangu ili tuendelee kujifunza pamoja
26/09/2025
NIMEREJEA TENA. Tuendelee kusupport kwa kushare kazi zangu, nami nasema
"Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo k**a ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga".
Yohana 14:27
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the establishment
Telephone
Address
Iringa