Manothu.com
Mwandishi wa habari za michezo za kitaifa na kimataifa.
OZIL: FURAHA YETU NI KUWA JUU YA TOTTENHAM.
📝Lotti Junior.
Mchezaji nyota wa klabu ya Arsenal fc ya jijini England amesema wanafuraha kuwa juu ya Tottenham katika kipindi ambacho mbio kuelekea mwisho wa msimu katika ligi kuu England zinazidi kupamba moto.
Washika mitutu hao waliwabamiza Newcastle hapo jana (jumatatu) na kuweza kuwapiku mahasimu wao kutoka London(Spurs) katika nafasi ya tatu.
Spurs wamedumu kwa muda mrefu katika nafasi ya tatu na kuonekana k**a ndio washindani wakuu wa Liverpool na Manchester city katika mbio za ubingwa mwanzoni mwa mwaka huu.
Lakini kwa sasa klabu ya Arsenal imeweza kugeuza meza,na kiungo mshambuaji Ozil ni mwenye furaha sana kuwa katika nafasi ya kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya kuelekea ukingoni mwa msimu huu.
"Mipango yetu ni kuwa katika klabu nne za juu, hakika tunafuraha sana kwamba tupo juu ya Tottenham. Mara zote tuna ushindani mkubwa nao" Ozil akielezea baada ya ushindi wa hapo jana.
"K**a tutacheza k**a leo,tuna mechi chache usoni na tunataka kushinda.Tunataka kuchukua alama zote na kuingia katika nne bora mwishoni mwa msimu".
©2019
22/03/2019
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uganda (FUFA), limemtangaza Samuel Fabin Kwesi raia wa Ghana kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 na miaka 20.
:
Fabian Kwesi atakioongoza kikosi cha Uganda U-17 katika fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Tanzania Aprili 14 - 28.
21/03/2019
Leo vimezaliwa hivi vyuma, Siku ya Washindi hii leo🏆💪💪
Click here to claim your Sponsored Listing.