SautiNote

SautiNote

Share

14/06/2026

Mtandao wa Facebook umethibitisha kuwa Rasmi umeanza Utaratibu wa Kuondoa/Kusitisha kwa Muda Programu za Kulipwa (Content Monetisation, Stars, Creator Storefront) kwa Kurasa zote zitakazo jaribu kupost Maudhui ya Aina moja kwa zaidi ya Mara moja katika nyakati tofauti ili kujipatia Mapato zaidi (Revenue), Ushawishi (Engagements) na Watazamaji (Views).

Meta Imesema kuwa Baadhi ya Kurasa zimekuwa zikijaribu kujipatia kipato zaidi kwa maudhui ya kujirudia ambapo ni kinyume na Partner Monetisation Policies, Meta imesisitiza Content Creators kushare maudhui ya aina moja mara moja.

Aidha, Meta imethibitisha kuwa Baadhi ya Programu zake hazitopatikana Nchini Tanzania kutokana na sheria za Nchi na Makubaliano ya Serikali.

06/06/2026

Taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wakala wa Uchunguzi wa Fedha wa Equatorial Guinea, Baltasar Ebang Engonga, ameachiwa huru kutoka gerezani zimeonekana kukosa uthibitisho rasmi, huku vyanzo mbalimbali vya uhakiki wa taarifa vikizitaja k**a uvumi au madai yasiyothibitishwa.

Engonga alipata umaarufu mkubwa duniani mwaka 2024 baada ya mamia ya video zake za faragha kusambaa mtandaoni. Hata hivyo, kesi iliyomfikisha mahak**ani haikuhusiana na video hizo, bali ilihusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya madaraka na makosa mengine ya kifedha.

Katika wiki za hivi karibuni, Machapisho katika Majukwaa ya Mitandao ya Kijamii na Blogs yamekuwa yakidai kuwa Engonga ameachiwa huru. Hata hivyo, uchunguzi wa madai hayo umeonyesha kuwa hakuna tamko rasmi kutoka serikali ya Equatorial Guinea, mahak**a au mamlaka za magereza linalothibitisha kuachiliwa kwake. Baadhi ya taasisi za uhakiki wa habari zimeeleza wazi kuwa madai hayo ni ya uongo au hayana ushahidi wa kutosha.

🖋️

03/06/2026

: Msanii wa Chief Godlove alia kwa UCHUNGU, Aomba kurejeshewa YouTube yake.

01/06/2026

Ukisikia Mwisho wa Ubaya ni Aibu, ndio hii sasa 🤔🙌

01/06/2026

Wazazi Nchini Tanzania wakerwa na maudhui haya yaliyochapishwa Mitandaoni yakimuonyesha Mzazi (Baba) akizungumza na Bintiye kwa namna yao.

Wazazi wadai yanaharibu Tamaduni, Heshima na Maadili kwa watoto. Wazazi wadai maudhui haya na mengine fanani yanapaswa kukemewa vikali na wahusika Kuonywa au kuchukuliwa hatua.

Nini Maoni yako Mwana SautiNote? 🤔

Soma zaidi: https://sautinote.com/social/maadiliwazazi

24/05/2026

Miamba wanne katika Picha moja, nani aina yake ya Uongozi ilikukosha zaidi? 🤔🙌

23/05/2026

Hapa Kipaji tunacho au hatuna? 🤔🙌

21/05/2026

Shuhuda wa Tukio la Utekaji wa Msaidizi wa Lissu afunguka Mwanzo Mwisho.

19/05/2026

Nini Maoni yako?

19/05/2026

UGONJWA WA EBOLA: Dalili, Madhara na Namna ya Kujikinga

Ebola Virus Disease ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya Ebola. Ugonjwa huu huenea kupitia kugusana moja kwa moja na damu, jasho, mate, matapishi, mkojo au majimaji mengine ya mwili wa mtu aliyeambukizwa.

DALILI ZA EBOLA
Dalili huweza kuanza kuonekana ndani ya siku 2 hadi 21 baada ya maambukizi. Miongoni mwa dalili hizo ni:

• Homa kali ya ghafla
• Uchovu mkubwa
• Maumivu ya kichwa
• Maumivu ya misuli na viungo
• Koo kuuma
• Kutapika
• Kuharisha
• Maumivu ya tumbo
• Kukosa hamu ya kula
• Macho kuwa mekundu
• Kutokwa damu puani, mdomoni au sehemu nyingine za mwili katika hatua kali za ugonjwa

MADHARA YA EBOLA
Ebola inaweza kusababisha madhara makubwa kiafya ikiwa mgonjwa hatapatiwa matibabu mapema, ikiwemo:

• Upungufu mkubwa wa maji mwilini
• Kushindwa kufanya kazi kwa ini na figo
• Kushuka kwa presha ya damu
• Kudhoofika kwa mwili kwa kiwango kikubwa
• Kifo
• Baadhi ya waliopona pia wanaweza kubaki na madhara ya muda mrefu k**a uchovu, maumivu ya viungo na matatizo ya macho.

NAMNA YA KUJIKINGA
• Epuka kugusa majimaji ya mwili ya mtu mwenye dalili za Ebola
• Nawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni
• Epuka kugusa maiti bila vifaa maalum vya kinga
• Fuata maelekezo ya wataalamu wa afya
• Wahi hospitali mapema unapohisi dalili
• Wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa utambuzi wa mapema na matibabu ya haraka huongeza nafasi ya mgonjwa kupona.

Fuatilia zaidi Dondoo za Afya kupitia katika tovuti yetu.

Want your business to be the top-listed Media Company in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address

Dar Es Salaam