Jacque Networker
*WATENDEE WATU WOTE WEMA*
Habarini za asubuhi champions. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiandaa kwenda kuyatimiza majukumu yako siku ya Leo. Leo ni siku muhimu, usikubali kuipoteza bure. One day can make you grow.
Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandali. Watu wengi wamekuwa wakitenda mambo mema kwa wale watu wanaowafahamu au wenye vyeo fulani. Huu ni mtizamo basi ambao inabidi jamii zetu ziachane nao.
Mara nyingi unaweza kukuta mtu anampa msaada mtu fulani kwa sababu anafahamiana naye. Hii inaleta mtizamo hasi kwa watu wengine. Unapojifanya kuwa mwema kwa bosi wako na kuwafanyia wengine ndivyo sivyo kumbuka hata bosi wako alianzia huko chini.
Kumbe siku moja mtu uliyekuwa ukimfanyia mabaya ndiye atakuja kuwa bosi wako.
Wazazi wengine wamekuwa wakiwanyima watoto wao mambo Fulani Fulani na kuwaendeleza wengine. Mfano unakuta mtoto Fulani ananyimwa kitu Fulani na wengine wanapata. Kuna watu wengine huko nyuma wazazi wao walikataa kuwasomesha lakini Leo hii ndio kitega uchumi cha familia. Wale waliosoma hawazisaidii familia zao. Kumbe wazazi wanayo haja ya kutoa malezi yaliyo sawa kwa kila mtoto.
Kila mtu unayekutana naye kila siku mtendee wema, hujui siku moja atakuwa nani au utamkuta wapi. Kwenye biashara jambo ili ni muhimu sana jali sana wateja wako wote hata k**a ni wa siku moja. Kumbuka watu wananunua kwa mtu wanayemjua na kumuamini. Sasa k**a huwatendei watu mambo mema unategemea kweli waje kwenye biashara yako k**a wateja?
Kumbe inatubidi tubadilike. Tujali kila mtu na tusibaguane.
*See you champions at the top and in the beaches of the world*
Click here to claim your Sponsored Listing.