JamboMail

JamboMail

Share

15/07/2026

Picha mpya kabisa kutoka kwa mwanamuziki wa Bongofleva, Nandy.

Je, hilo pozi la picha ya kwanza linaitwaje?.

15/07/2026

Sosholaiti Zari The Bosslady hatimaye amevunja ukimya baada ya muonekano wa uso wake [picha ya kulia] kuzua mjadala mzito katika mitandao ya kijamii.

Mama huyo wa watoto watano alisema ameshangazwa na jinsi sura yake ilivyogeuka kuwa mjadala mkubwa, akitania kwamba pamoja na mambo mengi yanayoendelea, watu wameamua kujadili uso wake.

"Kwa namna fulani, uso wangu umekuwa mjadala wa kitaifa. Kati ya mambo yote yanayostahili kujadiliwa, mmeamua kujadili uso wangu," alisema.

Zari alikiri kuwa alifanyiwa temporal lift, ambao ni utaratibu wa urembo unaofanyika eneo la pembeni mwa macho, lakini akakanusha madai kwamba alifanyiwa upasuaji kamili wa kuvuta ngozi ya uso (facelift).

"Nilifanyiwa temporal lift, ambao unahusisha eneo la macho. Sio facelift kamili, kwa sababu facelift ya kawaida huhusisha kukatwa na taratibu nyingine za upasuaji," alieleza.

Pia alifafanua kuwa muonekano uliowaacha wengi wakishangaa kwenye picha zilizosambaa mitandaoni ulitokana zaidi na aina ya vipodozi alivyopakwa. Kwa mujibu wa Zari, mpambaji wake, Sami, alitaka kujaribu mtindo mpya wa fox eye, ambao ulifanya macho yake yaonekane yamevutwa juu zaidi kuliko hali halisi.

"Vipodozi vilikuwa vimezidi kidogo. Sami alitaka kujaribu mtindo mpya kwenye uso wangu, na mwishowe macho yangu yalionekana yamevutwa juu sana," alisema.

Akitetea uamuzi wake, Zari alisema hafichi chochote kuhusu taratibu za urembo na hana sababu ya kuwaficha wengine taarifa hizo.

"Sifichi chochote. K**a kuna jambo litakalokufanya ujisikie vizuri zaidi kuhusu mwonekano wako, kwa nini usilifanye?" alisema.

Mfanyabiashara huyo pia alisisitiza kuwa amekuwa mwanamke mrembo siku zote, na kwamba alichofanya ni kuboresha muonekano wake kadiri anavyoendelea kuzeeka.

"Nimekuwa mwanamke mrembo siku zote. Ninachofanya ni kuboresha mwonekano wangu kadiri tunavyozeeka, kwa sababu mambo hubadilika," aliongeza.

15/07/2026

Mfanyabiashara Zari The Bosslady ameshinda kesi ya mgawanyo za mali za aliyekuwa mume wake marehemu Ivan Ssemwanga.

Mahakama ya kifamilia Kampala, Uganda, imeamua kuwa mali za Ivan Ssemwanga, zitakuwa za watoto wake pamoja na mama yao, Zari Hassan.

Ikumbukwe Zari na Ivan Ssemwanga walijaliwa kupata watoto watatu pamoja. Katika picha ni Zari pamoja na watoto wake wakiwa ndani ya mahakama.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Mikocheni
Dar Es Salaam