Manuva Forum
Hili Kabila Gani ...?
Happy new year 🎉
09/12/2025
😂😂
06/12/2025
😂😂😂
06/12/2025
29/11/2025
Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kuwa changamoto nyingi zinazolikabili bara la Afrika hazitokani na ukosefu wa rasilimali, bali ni kukataa kuchukua hatua licha ya fursa kuwa wazi.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kigali, Kagame alitumia msemo wa kitamaduni kueleza hali hiyo:
“Unaweza kuwapeleka farasi kisimani, lakini huwezi kuwashurutisha kunywa maji. Afrika tuna maji mbele yetu, tuna kiu, lakini bado tunatafuta visingizio vya kutokunywa.”
Kagame alisema bara hilo lina kila kitu, rasilimali, watu, maarifa na uwezo, lakini bado linajikuta likiporomoka katika maeneo muhimu k**a usalama, utawala bora, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akaongeza kuwa:
“Sifahamu ni kwa nini tunashindwa mara kwa mara, hata katika jukumu la msingi la kuwalinda wananchi wetu. Tuna watu, tuna rasilimali, tuna ujuzi, tunacho kisingizio gani cha kushindwa?”
Kauli hii imeibua mjadala mpana kuhusu sababu halisi za udhaifu wa mifumo ya uongozi Afrika, hasa wakati ambao mataifa mengi yanapitia mivutano ya kisiasa na wimbi la mapinduzi linaloendelea kuongezeka bara zima.
29/11/2025
Kwenye kundi B Yanga ni timu pekee ambayo haijaruhusu goli✍️
28/11/2025
wa george ambangile
✍🏻Kama huwezi kushinda basi hakikisha unazuia vizuri usifungwe , ndio kilichotokea kwa Yanga , kipindi cha kwanza walipata " attacking actions " nzuri za kutulia na kufunga goli ( magoli ) lakini ukosefu wa utulivu na uduni wa ubora ( kwa siku husika ) ulifanya wahamie upande wa pili wa mchezo ambao kuzuia basi wasifungwe dhidi ya JS Kabylie
✍🏻Yanga hawakutaka kabisa kuruhusu JS Kabylie kucheza vizuri ndani ya uwanja, katika kila pasi ya mpinzani wao wanakuwa haraka kufika eneo la mpira kuweka presha au kupora kabisa mpira kitu ambacho kilifanya JS Kabylie kutafuta njia nyingine ambayo ilionekana inaweza kuwapa kitu
✍🏻Kuwa na idadi nzuri ya wachezaji pembeni ya uwanja dhidi ya fullbacks wa Yanga , mmoja kwenye mpira na mwingine kufanya runs na hii walifanya sana mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kipindi cha pili , shida kwa kipindi cha pili kwao ni kwamba safari hii Pacome na Edmund walikuwa wana track back sana kiasi kwamba Israh na Zimbwe / Boka wanakuwa k**a mabeki wa kati pembeni ( back six ) na mstari wao wa kiungo upo karibu sana na walinzi hakuna spaces between the lines
✍🏻Kama unaamua kuzuia sana , angalau basi hakikisha ukiupata mpira wafikirishe wapinzani kwamba wasije tena kwako wakiwa huru . Nafikiri Yanga hata kipindi cha pili mara kadhaa walipata counter attacking actions lakini sana utekelezaji wa vitendo vya mpira ulikuwa duni sana tena kwa wachezaji wote ambao walikuwa wanafika mbele ( kuvuka mstari wa katikati )
NOTE
1: Ryad Boudebouz ndio alionekana pekee kubeba ufunguo wa JSK kwenye kutengeneza nafasi bora , nafikiri mchezaji ambaye alipaswa kuwa na mpira zaidi
2: Maxi na Abuya hawakukubali kuwa abiria katikati ya uwanja , sehemu hatari mchezoni 🔥
3: Leo decision making kwa wachezaji wa Yanga ulikuwa duni katika nyakati muhimu wakiwa wanafika mbele
4: Djigui Diarra katika nyakati ambazo huwa anatakiwa kusimama na kuhesabiwa huwa anaonesha thamani yake . Saves kadhaa muhimu na kuwakumbusha wenzake kuhusu umakini : LEADER
FT : JS Kabylie 0-0 Yanga SC
28/11/2025
Kwenye CAF Confederation Cup Azam wame poteza michezo yote miwili ya awali, kwenye Ligi kuu wame shinda mechi moja tuu kati ya 3
Wapo nafasi ya mwisho kwenye Group lao na wapo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi kuu
Bado tuna jiuliza tatizo nini?
28/11/2025
Kwenye Group la Kifo🙌🏼 Mwamba Pedro Goncalves amewaongoza Yanga kuvuna alama4 katika michezo miwili ya mwanzo 🔥
Msimu uliopita k**a sasahivi Yanga alikua na alama0, alisha pasuka dhidi ya Al Hilal home na away dhidi ya Mc Alger
Mwanzo mzuri mnoo, Yanga wame tawala kila kitu katika soka la ndani kazi ilikua kurudisha heshima ya Wananchi katika michuano ya Caf 🔥
Bado hili ni Group la kifo... Michezo mi4 ya Yanga ilio salia dhidi ya Ahly home and away, dhidi ya Rabat ugenini na Js Kabylie 🙌
WANANCHI WAPO KILELENI MWA GROUP LA KIFO
28/11/2025
Kutoka Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kesi ya kudharau amri ya Mahak**a iliyokuwa imefunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche yametupiliwa mbali
Akisoma uamuzi wa Mahak**a hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa kwa hati ya dharura amesema, Mahak**a imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima.Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahak**ani hapo nje ya muda
Jaji Mbagwa amesema kesi ya msingi namba 8960/2025 iliyoko chini ya Jaji Hamidu Mwanga ndio iliyokuwa msingi wa kesi iliyokuwa mbele yake, na kwamba amri ya Mahak**a kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA ilitolewa na Mahak**a Juni 10.2025
Aidha, Jaji Mbagwa ameendelea kufafanua kuwa kesi ya kudharau amri ya Mahak**a ililetwa Mahak**ani hapo Oktoba 03 mwaka huu takribani siku 106 jambo ambalo halikubaliki kisheria, Sheria inataka maombi ya aina hiyo yaletwe ndani ya siku 60.
Credit Jambo TV
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Arusha
15300