Isack Jonas Jr.
31/05/2022
Imani ina uwezo wa kujenga vitu vikubwa sana na hofu huweza kubomoa kila kitu maishani mwako.
Chagua Imani
30/05/2022
Uaminifu ni jambo linalokujenga wewe na pia kutendea vyema jamii.
Chagua UAMINIFU zaidi ya kitu kingine chochote...!
25/05/2022
Kuna furaha katika kufanikiwa kufanya mtu mwingine afurahi.
24/05/2022
Mche MUNGU
PENDA watu.
PERIOD.
24/05/2022
Mabadiliko in jambo muhimu sana kwa sababu hutusaidia kuwa bora zaidi yatulivyo sasa au hata kutuondolea hali tutusizofurahia. Kitu pekee cha kuepuka katika kujifanyia mabadiliko ni kubadilika kunakoweza kukudhuru au kubadilika kuwa usivyotaka kwa ajili ya kufurahisha mtu asiyedhamini kujitoa kwako kwa ajili yake.
Kubadilika kunakofaa ni k**a:
1. Kuacha tabia au mambo yanayowakwaza wazazi wako.
2. Kuboresha afya ya mwili wako k**a kupunguza unene.
3. Kuepukana na tabia zinazokupotezea sifa njema kwa Mungu na jamii yako.
4. Kuacha matumizi ya vitu vinavyokuletea madhara kiafya, kiimani au kijamii.
Wote tuna chumba cha kuwa bora kila wakati. Mabadiliko ni kuufungua mlango huo na kuingia.
Click here to claim your Sponsored Listing.