Amani Radio FM

Amani Radio FM

Share

10/06/2026

Waamini wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo Kuu Katoliki Arusha wanaendelea kushiriki Kongamano maalum linalofanyika katika Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro, k**a sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo jimboni hapa.

Akiendelea na utoaji wa mada Padre Festus Mangwangwii, Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Mama Bikira Maria Unga Limited, amewaasa wakristo na wanashirika kuchota neema katika fadhila za moyo Mtakatifu wa Yesu. Kwa njia hiyo,"msichoke kutenda mema,nyakati zote," alikazia.

Akijikita katika mada ya; “Kujitambua na kuwajibika kwangu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu katika jamii kwa hali zote," amewataka wanamoyo na wakristo kwa ujumla kujikita katika maisha ya sala,upendo,umoja na mshik**ano katika jamii.

Kupitia mada hiyo, wakristo wanaalikwa kutambua wito wao na kuishi vyema maadili ya kikristo,kwani "Imani bila matendo,imekufa," alisisitiza Padri Festus.

Maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu Jimboni Arusha, ni fursa ya kumshukuru Mungu kwa neema na mafanikio ya shirika hili, pia nafasi kwa wanachama kuimarisha umoja, imani na dhamira ya kulitumikia Kanisa na jamii.

Semina hii ni mwendelezo kwa siku saba hadi Jumapili 13 June 2026 ambapo itatamatishwa na kilele cha Adhimisho la Misa ya Jubilei na kupokelewa kwa wanachama wapya katika Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro.

Sala:
Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, fanya mioyo yetu ifanane na Moyo wako.

10/06/2026

Kingozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amezungumza na hadhira ya vijana katika mkesha wa maombi kupitia shuhuda ambazo zilikuwa sehemu ya mkesha huo, kwa kuwakumbusha kutazama ndani ya mioyo yao na kuepuka kuzidiwa na kasi ya maisha na vishawishi vya nje.Kuhamasisha kuwa na dakika chache kila siku kusoma Injili na kuzungumza na Mungu.

Papa Leo XIV akizungumzia Afya ya akili amedokeza kuwa suala hili linazidi kukua katika jamii zinazojiona kuwa zimeendelea hivyo kuwa na tafsiri potofu ya dhana ya maendeleo na kuongeza shinikizo, matarajio na mivutano ambayo inaathiri usawa wa afya. Akitafakari Mateso ya Kristo, Papa Leo XIV amesema " Yesu alishirki mateso yetu lakini hatupaswi kuyafanya maumivu kuwa ya kiroho, tukiyahusisha na mapenzi ya Mungu kwani Mungu hataki mateso anayabeba nasi."

Kuhusu msamaha Papa Leo XIV ameeleza kuwa ni mchakato wa taratibu kwamba tujifunze kuuona msamaha, tiba yenye nguvu ya uovu inayoponya majeraha yetu ya ndani k**a sehemu ya mchakato na safari. Ameongeza kuwa mara pengine sio lazima uhusiano huo urudi k**a awali lakini hisia za chuki na kisasi zisiwepo bali maombi na mtazamo mzuri kuhusu mtu uliyemsamehe ni muhimu.

10/06/2026

Mtakatifu Landri alizaliwa nchini Ufaransa mwishoni mwa karne ya 6, baada ya kuingia kwenye utume aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo la Paris.

Mt. Landri alisifika sana kwa kuwa mtu mwenye huruma sana kwa wagonjwa na maskini, hata akajenga Hospitali kubwa Mjini Paris aliyoita Hospitali ya Mungu.Wakati fulani Jimbo lake lilikumbwa na njaa kali sana, kiasi cha yeye kutoa mali zake kwa ajili ya kuwanunulia watu chakula, na kilifika kipindi aliuza baadhi ya vyombo vitakatifu Kanisani ili apate fedha kwa ajili ya kuwanunulia waamini wake chakula.

Baada ya kifo chake watu bado walimkumbuka na kuenzi ukarimu wake, wagonjwa walikuwa wakienda katika kaburi lake na kwa msaada wa maombezi yake walipona. Ajali ya moto mkubwa ilitokea na kuunguza nyumba nyingi Mjini Paris watu walichukua sanda lake na kuweka mbele ya moto huo ambao baadaye ulizimika.
Mtakatifu Landri Utuombeee.

KONGAMANO LA SHIRIKA LA MOYO MT. WA YESU JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA. 09/06/2026

SIKU YA PILI:
KONGAMANO LA SHIRIKA LA MOYO MT. WA YESU JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA,IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA JUBILEI YA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWA SHIRIKA HILI,KONGAMANO HILI LINAFANYIKA KATIKA PAROKIA YA ROHO MT. NGARENARO

KONGAMANO LA SHIRIKA LA MOYO MT. WA YESU JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA. SIKU YA PILI: KONGAMANO LA SHIRIKA LA MOYO MT. WA YESU JIMBO KUU K...

09/06/2026

Papa Leo XIV amesema familia ni shule ya kwanza ya ubinadamu, ambapo, kabla ya mahali pengine popote, tunajifunza maana ya misingi ya kuishi pamoja ikiwa ni pamoja na maisha ya kukaribisha, kuwajali wengine, kusamehe, kuhudumia, na kuwa mali.

Papa Leo XIV ameeleza hayo leo Juni 8 akiwa ziarani nchini Uhispania na kugusia maeneo mengine k**a masuala ya kisiasa, amani, mazungumzo, upangaji upya, uhamiaji, sheria, mgawanyiko, mada za kimaadili, familia na ulinzi wa maisha kisha alitoa wito wa uhuru wa dhamiri na dini ikiwa ni pamoja na usiri wa maungamo,kuwatunza maskini, na hatimaye ujumbe kwa Hispania, Ulaya, na dunia nzima.

Pia ameeleza kuwa Taasisi za elimu zina jukumu muhimu ili kuwezesha vizazi vipya kujifunza kutafuta na kupenda ukweli, kuhoji maana ya maisha na hadhi ya kila mtu. Hivyo wazazi wengi, wakiwa na hamu ya watoto wao kujifunza kuhusiana na wengine, kufikiria kwa kina, na kupata maadili thabiti, huwawekea matumaini makubwa k**a washirika wa thamani katika malezi yao.

09/06/2026

Mtakatifu Efrem alizaliwa Nisibisi, Mesopotamia nchini Iraq mwaka 306. Akiwa kijana alifukuzwa nyumbani kwa wazazi wake kwasababu ya kupenda dini ya kikiristo, baada ya hapo alifundishwa mafundisho ya dini ya kikiristo na kwa miaka nane aliishi na watawa katika pweke nchini Misri.

Mt. Efrem alikataa kupewa Daraja la Upadre na Uaskofu. Alikuwa akipinga mafundisho ya kizushi kwa mahubiri na mafundisho yake na kwa njia ya uandishi wa vitabu nautunzi wa nyimbo nyingi za ibada alifanikiwa kukomesha mafundisho ya kizushi.

Mt.Efrem ni maarufu kwa uandishi wake wa tafakari ya Biblia huko nchini Syria. katika nukuu yake moja anatupa tafakari kwamba” Ubikira/ Useja ni farasi wa vita, utapaishwa juu k**a nabii Eliya wale wanaoutunza”. Tumtakie Heri ya kumbukizi ya Mtakatifu somo wake

08/06/2026

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha Mha. Isaac Amani amewakumbusha waamini kuwa Kanisa linaadhimisha mafumbo makuu manne k**a misingi ya Imani.

Askofu Mha. Isaac Amani ameeleza hayo katika homilia yake kwenye Adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya Sherehe ya Mwili na Damu ya Yesu Kanisa kuu la Mt. Teresia wa Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki Arusha.

08/06/2026

Kongamano kuelekea kilele cha sherehe ya Jubilei ya miaka 50 ya Shirika la Roho Mtakatifu Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Kuanzia Jumatatu ya tarehe 8 Juni hadi tarehe 13 Juni katika Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro.

Kongamano linawezeshwa na Padre Festus Mangwangi wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Nyote Mnakaribishwa.

08/06/2026

Papa Leo XIV akihutubia Bunge nchini Hispania na ulimwengu mzima kupitia jukwaa hilo amesema kwamba uhuru ni mojawapo ya zawadi za thamani zaidi ambazo mbingu imewapa wanadamu.

Papa Leo XIV ameeleza hayo leo Juni 8 akiwa ziarani nchini Uhispania na kugusia maeneo mengine k**a masuala ya kisiasa, amani, mazungumzo, upangaji upya, uhamiaji, sheria, mgawanyiko, mada za kimaadili, familia na ulinzi wa maisha kisha alitoa wito wa uhuru wa dhamiri na dini ikiwa ni pamoja na usiri wa maungamo,kuwatunza maskini, na hatimaye ujumbe kwa Hispania, Ulaya, na dunia nzima.

Katika hatua nyingine Papa Leo XIV amesema kuwa Kila maisha ya mwanadamu lazima yatambuliwe na kulindwa tangu kutungwa mimba hadi mwisho wake wa asili, katika kila hali ya kuwepo kwake. Ulinzi wa maisha ya mwanadamu si jambo la maslahi au ungamo maalum ni lengo la ustaarabu.

Want your business to be the top-listed Media Company in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address

3044
Arusha
23000