PDK generation

PDK generation

Share

28/07/2025

JINSI YA KUPUNGUZA MADENI YA BIDHAA ZA AFYA BOHARI YA DAWA MEDICAL STORES DEPARTMENT MSD

Hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya hapa Nchini imeendelea kuimarika siku hadi siku. Licha ya kuimarika huko, bado kuna changamoto kadhaa ambazo tunapaswa kukabiliana nazo. Mojawapo ya changamoto hizo ni madeni ambayo bohari ya dawa (medical stores department) inadai kwa baadhi ya wateja wake.

Madeni haya yana visababishi kadhaa ikiwemo matumizi ya fedha za mapato ya vituo yasiyofuata miongozo pamoja na kutoelewa vizuri kutafsiri taarifa mbalimbali zinazopatikana katika mifumo ya ugavi wa bidhaa za afya.

Katika makala hii kwenye YouTube channel ya PDK Generation tumeeleza kwa kutumia mifano halisi namna ambavyo makosa yanafanyika wakati wa kuagiza bidhaa za afya kwa waagizaji kushindwa kutafsiri vizuri taarifa zilizopo kwenye mfumo wanaotumia kuagiza unaofahamika k**a electronic logistics management information system (eLMIS)

21/03/2025

DAWA YA COLCHICINE INAYOTIBU MAGONJWA K**A GOUT , ARTHRITIS NA RHEUMATISM IKO KWENYE MMEA HUU

Mmea huu ambao kwa jina la kisayansi unajulikana k**a Gloriosa superba una kiasi kikubwa cha dawa ya colchicine ambayo hutumika katika kutibu na kuzuia ugonjwa wa gout (gauti) na magonjwa mengine kadhaa.

Mmea huu unaopatikana katika maeneo mbalimbali ya Bara la Africa na kwingineko duniani, kwa sasa upo hatarini kutoweka.
Ili kuuona mmea huu na kusikiliza mengi zaidi yanayouhusu, tembelea YouTube channel yetu ya PDK Generation.

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address

Arusha