Carlos Ricky Wilson Kirimbai

Carlos Ricky Wilson Kirimbai

Share

13/06/2026

Mtu wa Mungu wa thamani, huwezi ukaishinda vita dhidi ya dhambi, dunia na matendo ya mwili kwa kujitahidi.

Bidii zaidi haitakufanya uwe huru mbali na dhambi, dunia na matendo ya mwili.

Nguvu ya maamuzi na utashi haiwezi ikakupa ushindi dhidi ya dhambi, dunia na matendo ya mwili.

Kuwa mkali na mwamini hakuwezi kumfanya kuwa huru mbali na dhambi, dunia na matendo ya mwili.

Namna ya pekee ya mwamini kukua hatua kwa hatua na kupata ushindi juu ya dhambi, dunia na matendo ya mwili ni kuenenda ya Roho.

Kwa mujibu wa tafsiri ya bibilia ya kiingereza ya Amplified Classic (AMPC) kuenenda kwa Roho ni kuishi kwa kumwitikia Roho Mtakatifu, kuendeshwa Naye na kuongozwa Naye.

Hii ndo namna ya pekee kwa mwamini kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi, dunia na matendo ya mwili.

Kujitiisha kwa Roho Mtakatifu, kujisalimisha Kwake na kujiweka wakfu Kwake ndo tumaini la pekee la ushindi juu ya dhambi, dunia na matendo ya mwili kwa mwamini.

Ushindi dhidi ya haya ni muhimu mno kwa mwamini ili aweze kuurithi Ufalme wa Mbinguni maana maandiko yapo wazi kuwa atendaye dhambi, matendo ya mwili na udunia hawezi kuurithi Ufalme wa Mbinguni.

Sasa tusifanye kosa la kudhani tunaweza kuishinda dhambi, udunia na matendo ya mwili kwa nguvu zetu wenyewe.

Hili linawezekana tu katika maisha ya mwamini kwa mwamini kuishi maisha kwa msaada na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.

Ndiyo maana Roho Mtakatifu alipelekwa kwetu ili kutuwezesha waamini kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi, udunia na matendo ya mwili.

MUNGU ATUSAIDIE TUELEWE NINI MAANA YA KUENENDA KWA ROHO NA KUISHI MAISHA YETU KWA KUENENDA KWA ROHO ILI TUISHI KWA USHINDI JUU YA DHAMBI, UDUNIA NA MATENDO YA MWILI.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

Arusha