The winner group
09/10/2019
Kila utakapoamua KUFANYA ama KUSIMAMIA kitu fulani kuna WATU na MATUKIO ambayo yatakuja ili kukutoa kwenye MSTARI yenye nia ya kukupoteza utoke kwenye “FOCUS” yako.Hii ndio maana kila siku lazima udhamirie kutumia MUDA mwingi katika ulichoamua kufanya zaidi ya kitu kingine chochote.
Winston Churchil aliwahi kusema “Hauwezi kufikia hatima yako k**a kila Mbwa anayekubwekea unasimama na kuanza kumrushia mawe”(You will never reach your destiny if you stop and throw stones to every dog that barks).
Kila siku kwenye maisha yako kuna “Mbwa” ambao wametumwa kukutoa kwenye mstari wako.Baadhi yao huja kabisa kwa njia ya KUKOSOA,KUKUKATISHA TAMAA,KUKUHAMISHA hoja n.k nia yao kubwa hapa ni uache kile unachofanya na uanze KUSHUGHULIKA nao.Usipokuwa makini utajikuta unatumia nguvu kubwa kudeal nao badala ya KUSONGA mbele.Be Smart.
Wengine watakuja k**a wana nia nzuri kwa kuleta FURSA ambayo inaonekana nzuri sana ambayo itakufanya uanze kuitamani na kuacha ulichodhamiria kufanya.Kumbuka sio kila FURSA NZURI ni fursa SAHIHI kwako:Jua kutofautisha.Kumbuka fursa nzuri hazitaisha kial siku zitakuja mpya,ni wajibu wako kuamua na kuchagua UNACHOTAKA kwenye maisha.
Leo kuna “Mbwa” wengi wamejiandaa kukubwekea ili wakutoe kwenye mstari, uwe makini usipoteze muda kushughulika nao,weka NGUVU na MUDA wako katika jambo MUHIMU.Kumbuka ukianza kuwarushia mawe ndio FURAHA na USHINDI wao na wataongeza SAUTI ya KUKUBWEKEA na wewe utaongeza UBIZE wa kuwarushia mawe mengi zaidi,na hapo utazidi kupoteza muda zaidi.
Ulishawahi kukutana na watu wa namna hii?Vipi wameshaanza KUBWEKA?Wakianza leo waambie “Nimekushtukia,hunitoi nje ya mstari” 😂😂😂
See You At The Top
23/09/2019
Dunia huwa inatupa kile tunachokitaka na tunakizungumzia kila mara katika midomo yetu. katika jamii zetu kulalamika ndiyo utamaduni uliozoeleka, ukienda ofisini watu wanalalamika, kwenye usafiri watu wanalalamika, kwenye nyumba za ibada watu wanalalamika. Hivi ni eneo gani la maisha yako umeona sehemu ambayo watu hawana utamaduni wa kulalamika?
Binadamu tumekuwa ni watu ambao tumekosa shukrani, hata tupewe nini hatuwezi kukosa shukrani. Tunajiona hatuna kitu fulani kwa sababu maisha yetu tumeyaweka katika vitu, tunaishi kwa ulinganishi wa vitu na pale tunapojaribu kulinganisha tunajikuta tunaumia na hatuna kitu.
Hakuna mtu ambaye amejitosheleza kwa kila kitu, tunatakiwa kushukuru kwa kile ambacho kipo ndani mwetu, tusiangalie tumekosa nini, badala yake tukumbuke tumepata nini, tukiwa tunaangalia vile ambavyo tunavyo maisha ni mazuri sana lakini tukiwa tunaangalia vile ambavyo hatuna maisha yanakuwa siyo mazuri sana.
Tunapoteza maana ya maisha yetu pale tunapokuwa tunajilinganisha na watu wengine. maisha yako ni maisha yako, yapende na yafurahie kwa sababu hakuna mtu mwenye maisha mazuri k**a wewe hapa duniani.
Rafiki, siku hii ya leo fanya zoezi la kutolalamika na badala yake fanya zoezi la kushukuru tu, shukuru kwa kile ambacho unacho na siyo kile ambacho huna. Furahia kwa kile ambacho kipo mkononi mwako na usitegemee kile ambacho hakipo mkononi mwako, kitegemee pale ambako tayari umekuwa nacho mkononi lakini vinginevyo hapana.
Kulalamika ni roho ya umasikini, utamaduni wa kulalamika una haribu dunia yetu, tumekuwa na jamii ya watu wanaolalamika kwenye kila eneo la maisha watu wanaolalamika wapo. Dunia ina uhaba wa watu wanaoshukuru ndiyo maana leo nakusihi sana fanya zoezi la kushukuru tu na kufurahia kwa yale ambayo Mungu amekujalia katika maisha yako. sherekea kwa kile ambacho unacho, jione wewe ni wa kipekee na umebarikiwa kuliko watu wote.
Tunaondoa Baraka katika maisha yetu kwa sababu ya kulalamika. Tunajiona ni watu tulioonewa, hivyo tunaona kulalamika ndiyo njia kuu ya kupata kile tunachotaka. Tunapolalamika tunapoteza nguvu na muda hivyo ni bora kukaa kimya k**a umeshindwa kuchukua hatua ya kukibadilisha kile unachotaka kiwe.
Ukiwa unahisi dunia imekutenga, una mawazo hasi basi na mara nyingi utajikuta maisha yako yanafanana na mawazo ambayo yako akilini mwako. Usijiwazie mabaya wala kulalamika, kila siku jione mtu aliyebarikiwa kwenye kila eneo la maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; jione wewe ni mshindi, jitamkie maneno chanya na vunja laana ya kulalamika, unapolalamika juu ya kitu fulani unakuwa unajizibia Baraka eneo hilo, hutaona mazuri bali mabaya tu.
Kwahiyo, maisha ni mazuri k**a tukiwa ni watu wa kushukuru kwa vile ambavyo tunavyo na siyo kulalamika kwa vile ambavyo hatuna.
Kumbuka, ulichonacho kinatosha k**a ukifikiria vya kutosha.
Jey@
31/08/2019
Focusing on.......
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Arusha
255