Better Health

Better Health

Share

09/08/2020

FANGASI SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME
FANGASI SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME

Idadi kubwa ya watu husumbuliwa na tatizo la kuwashwa sehemu za siri bila kujari jinsia na umri.

Kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi mbalimbali ndani ya mwili wako pengine isiwe ni fangasi na ikawa ni mzio(allergy) tu.

Lakini watu wengi wanaamini kuwashwa sehemu za siri kunasababishwa na fangasi tu, sio kila muwasho ni fangasi

Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe kitu hicho kikiondolewa. Kuondolewa kwa kitu hicho kunatia ndani ya matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata mammbukizi tena. Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi. Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari. Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo.

SABABU ZA MUWASHO SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME

Kuwashwa uume au sehemu zingine za mwanaume husababishwa na sababu zile zile zinazosababisha muwasho sehemu nyingine za mwili.

Maradhi ya fangasi husababisha muwasho kwa wanaume wengi sababu nyingine ni k**a ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa, mzio na maabukizi mengine ya bacteria, maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume.

FANGASI SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME

Maradhi ya fangasi (candidiasis) husababishwa na vimelea viitwavyo candida albicans. Vimelea hivi hushambulia jinsia zote ingawa hushambulia sana jinsia ya k**e kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu kitu kinasosababisha wao kuathiriwa zaidi.

Watu wengi wana vimelea hivi katika miili yao kwa kiwango kidogo sana. Kinga ya mwili ikisaidiwa na bacteria walinzi wa mwili huweza kupambana na vimelea hivi.

Better Health Send a message to learn more

03/08/2020
Want your business to be the top-listed Beauty Salon in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address

Arusha