Tenga Legal Solutions.
Tuanze mwaka kwa hili maalumu kwa wale wakopaji.
TAASISI ZA MIKOPO ZINAPASWA KUFANYA TATHIMINI YA MALI KABLA YA KUUZA REHANI YA MKOPAJI KWA MNADA.
Je mnafahamu kwamba mkopeshaji [Benk au Taasisi za mikopo] pindi pale mkopaji anaposhindwa kulipa deni lake,wanapaswa kabla ya kuuza Mali iliyowekwa rehani kwa mnada, kufuata utarajibu wa kisheria kwa mujibu wa sheria ya ardhi [Land Act CAP 11 #3 RE 2023] katika kifungu cha 143(1) na (2)
Vifungu hivi vya sheria vinamtaka mkopeshaji (Benk) kuuza rehani ya mkopaji ( mortgaged property) kwa mnada pale inapobidi na atapaswa kuuza kwa bei bora zaidi (best price).
Ikumbukwe kwamba, ili kupata bei iliyo bora zaidi(best price) mkopeshaji(benk) anapaswa kufanya tathimini (valuation) ya rehani(mortgaged property ) kabla ya kuuza.
Kushindwa kufanya tathimini ( valuation) kabla ya kuuza Mali ya rehani kwa mnada ni uvunjifu mkubwa wa sheria na utapelekea uuzaji huo kubatilishwa (nullification of sale) na mahak**a.
Ivi karibuni Mahak**a Ya Rufani ya Tanzania (Court of Appeal) katika kesi ya CRDB BANK .VS. JONAS MARCO MGENI CIvil Appeal No 335 of 2024[2025] TZCA 1246 10 December 2025 TANZILII imetoa msimamo thabiti wa kubatilisha uuzaji wa rehani kwa mnada pale ambapo itabainika kwamba tathimini haikufanywa kabla ya kuuzwa kwa Mali ya rehani.
Hivyo basi kwa wale waliouziwa Mali zao au Mali zao zipo hatarini kuuzwa na benk au taasisi yoyote ya mikopo na wanauwakikika tathimini haikufanywa na benk kabla ya uuzaji wa rehani zao (mortgaged property) basi wanayo nafasi ya kwenda mahak**ani na kuiomba mahak**a ibatilishe uuzaji huo haramu kwani utaratibu uliopo kwa mujibu wa sheria haukufuatwa.
Lengo kuu la kufanya tathimini ya rehani kabla ya kuuza ni kujua thamani ya rehani kwa wakati huo(market value) jambo ambalo litapelekea rehani hiyo kuuzwa kwa bei bora zaidi.
Na endapo rehani itauzwa kwa bei kubwa zaidi ya deni basi mkopeshaji atapaswa kuchukua kiasi cha deni lake na kiasi kinachobaki kinapaswa kurejeshwa kwa mkopaji.
NB ikumbukwe kwamba tathimini (valuation) ni lazima Iwe imefanywa na professional valuer na imethibitishwa na Chief Valuer.
( Happy new year 2026)
Advocate Benjamin Tenga.
(0782523796).
30/01/2023
JE UNAJUA KWAMBA,
kila mwajiriwa anayo haki ya kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi (trade union) pasipo kulazimishwa na mwajiri wake hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Sheria No 6 ya mwaka 2004 Iliyofanyiwa Mapitio (2019).
Mfanyakazi atahitajika kujaza Form maalumu(TUF 15) ili kumruhusu mwajiri wake kufanya makato katika mshahara wake k**a malipo ya uanachama(membership fee). Mwajiri atapaswa kukata makato hayo kulingana na kiwango kilichowekwa na katiba ya chama husika(trade union) k**a Mchango wa uanachama (membership fee) hii ni kutokana na kifungu cha 61(1) (2) cha sheria No 6 ya mwaka 2004 iliyotajwa hapo juu.
Hata hivyo Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 iliyofanyiwa marejeo 2019 katika vifungu vya 61(4)(5) vinampa mwajiriwa haki ya kusitisha uanachama wake katika chama hicho cha wafanyakazi,hapa mwajiriwa atatakiwa kutoa notisi ya mwezi mmoja ya kusitisha uanachama wake katika chama hicho cha wafanyakazi(trade union)
Notisi ya mwezi mmoja itapaswa kutumwa kwa mwajiri na kwa chama husika.
Mwajiri atatakiwa baada ya kipindi cha notisi ya mwezi mmoja kupita kusitisha kufanya makato ya uanachama(cease to deduct employee salary for the membership fee) kutoka katika mshahara wa mwajiriwa.
Ni kinyume na haikubaliki kisheria kwa mwajiri kuendelea kukata makato ya michango ya uanachama wa vyama vya wafanyakazi(trade union membership contribution fee) kutoka katika mshahara wa mwajiriwa ambaye alishasitisha uanachama wake katika chama husika.
Wakili:Benjamin Tenga.
0782523796.
Tenga Legal Solutions. The firm has specialized in corporate, Conveyancing laws,labour laws,tax law,family laws, probate and litigation.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the practice
Website
Address
Arusha