jodic.ticd
09/07/2022
Karibuni kwa elimu bora na uhakika wa fursa za kujiajiri, kuajiri wengine na hata kuajiriwa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Kitaifa na Kimataifa na pia Serikalini.
13/01/2022
TICD kupitia Kituo chake cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidigitali yafanya Utafiti, Yatoa Suluhisho kwa Matatizo ya Kijamii kwa Vijiji 13.
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) imetekeleza kwa vitendo jukumu la kufanya utafiti kwa kubainisha mahitaji ya jamii na kuyatengenezea mpango mkakati shirikishi.
Utafiti huu ulifanywa mwaka 2020 ambapo takribani vijiji 13 vilivyopo katika Wilaya ya Arumeru viliweza kufikiwa na zoezi hili la utafiti.
Baadhi ya changamoto zilizobainishwa kupitia utafiti huo ni pamoja ukosefu wa maji safi na salama, ubovu wa barabara, ukosefu wa ajira kwa vijana na ukosefu wa vifaa tiba.
Hata hivyo, matokeo ya utafiti huo yanaonesha uwepo wa fursa anuai katika kutatua baadhi ya matatizo ikiwemo uwepo wa nguvu kazi, mikopo kwa vijana, akina mama na makundi maalum ambapo wawezeshaji walitumia majibu hayo ya utafiti huo kuhamasisha jamii kuhusu kutumia fursa hizo ili kujikwamua na changamoto hizo.
Katika mikutano mbalimbali iliyoendelea kufanyika katika vijiji hivi 13 ikiwemo Olgilai, ambapo Taasisi ilifika kutoa mrejesho na kufanya uchechemuzi, Januari 10, 2022 baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho akiwemo Einoth Lomayan, Sima Naftari na Richard Boaz waliipongeza TICD kwa kutekeleza moja ya Jukumu lao la Msingi la kufanya utafiti.
"Kazi mliyofanya (TICD) kwa kweli ni kupigiwa mfano, mlitambua changamoto zinazotukabili na tazama sasa mnaleta mrejesho kwa kubaini fursa zilizipo kwenye jamii yetu ikiwemo fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri za Wilaya kwa vijana wetu", alisisitiza Joseph Mollel mmoja wa wakazi wa kijiji cha Olgilai.
Zoezi la kutoa mrejesho na kufanya uchechemuzi litafanywa kwenye vijiji vyote 13 vilifanyiwa utafiti huu kikiwemo kijiji cha Olgilai, Engorika, Sekei, Naurei na Akheri.
Aidha vijijini vingine vitakuwa ni Nguruma, Patandi, Kikwe, Matevesi, Kiutu, Karangai, Maweni na Nambala.
Utafiti huu pia ulifamywa ikiwa ni utekelezaji wa mpango Mkakati wa Taasisi hii kwa mwaka 2017 - 2021.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Arusha
23000