Maria ken

Maria ken

Share

Maria on TikTok 11/10/2024

https://vm.tiktok.com/ZMhDXTuH3/

Maria on TikTok 14 Followers, 21 Following, 26 Likes - Watch awesome short videos created by Maria

12/01/2024

Muda mfupi uliopita, kulikuwa na mwanamke
ambaye alitaka kujua jinsi mume wake
angefanya ikiwa angeondoka bila
kumwambia alikokwenda.

Aliamua kumwandikia barua akisema
amemchoka na hataki kuishi naye tena.

Baada ya kuandika barua hiyo, aliiweka juu
ya meza ya chumbani kisha akaingia chini ya
kitanda kujificha hadi mumewe alipofika
nyumbani.

Hatimaye aliporudi nyumbani, aliona barua
kwenye meza na kuisoma.

Baada ya kimya cha muda mchache
akachukua kalamu na kuongeza kitu kwenye
ile barua.

Kisha akaanza kubadilisha nguo, akipiga
miluzi ya furaha na kuimba na kucheza huku
akifanya hivyo. Alichukua simu yake na
kupiga namba.

Mkewe alisikiliza akiwa chini ya kitanda huku
akianza kuzungumza na mtu.

"Hey babe, nabadilisha nguo tu basi
nitaungana na wewe," alisema.

"Kuhusu yule mjinga , hatimaye akili ilimjia
kwamba nilikuwa namdanganya na
kuondoka. Kweli nilikosea kuoa kuku
natamani tungekutana mapema. Tuonane
mpenzi"

Kisha akakata simu na kutoka nje ya chumba
kile.

Huku akitokwa na machozi na kuhuzunika
sana, alitoka chini ya kitanda na kukaa ili
kusoma yale ambayo mume wake mzinifu
alikuwa ameandika mwishoni mwa barua
yake.

Kupitia macho yake yaliojaa machozi,
alisoma: "Nimeona miguu yako wewe mjinga,
naenda kununua mkate."

Mwisho😎

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Kitale?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

Kitale