CEPAC Sayuni Sange.

CEPAC Sayuni Sange.

Share

06/06/2026

https://www.facebook.com/profile.php?id=100076284666592

CEPAC Sayuni Sange. Elewa kuwa Kuishi kwako ni mapenzi ya MUNGU, sasa ni wakati wako wakujiswali maswali haya: 1. kwanini MUNGU amenifanya nizaliwe?, 2. Kwanini wengi hufa ila mimi naendelea Kuishi?.


Ukijijibu vema basi fanya maamuzi ya vile utakavyo ishi.

06/06/2026

𝗜𝗹𝗶𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮 𝘀𝗶𝗸𝘂 𝗮𝗺𝗯𝗮𝗽𝗼 𝗺𝗮𝗹𝗮𝗶𝗸𝗮𝐚 𝘄𝗮𝘁𝗮𝘁𝘂
𝘄𝗮𝗹𝗶𝘁𝗲𝗺𝗯𝗲𝗹𝗲𝗮 𝗳𝗮𝗺𝗶𝗹𝗶𝗮 𝗺𝗼𝗷𝗮 𝘁𝗮𝗷𝗶𝗿𝗶.

Walipokwisha karibishwa ndani.
Wenye nyumba walipata kuwapa chumba.
Hata hivyo kile chumba walichopewa wale malaika hakikuwa kizuri, kilikuwa kibaya mno mfano wa stoo.
Kitanda chake kilikuwa kibovu kiasi cha kuwalazimu walale chini.
Kipindi wapo chumbani malaika mmoja MZEE anapata kuona tundu katika ukuta na kwa kutumia uweza wa MUNGU akaziba lile tundu malaika kijana akamuuliza "kwanini una fanya hivyo?" Nae akajibu "mambo huwa tofauti na inavyodhaniwa"
Baada ya hapo walipata kuendelea na safari mpaka sehemu nyingine.
wakapata hifadhi mwenye nyumba maskini.
Lakini familia hio iliwakaribisha vyema na kuwapatia chumba kizuri yaani MASTER BEDROOM na wenye nyumba wakawa radhi kulala sehemu mbaya.
Kisha ilipofika asubuhi familia ile ilikuwa kwenye majonzi mazito sana
Na kumbe ng'ombe waliokuwa wakimtegemea kwa kutoa maziwa mengi alikuwa amekufa.
Ndipo malaika kijana akamuuliza malaika mzee "hii sio haki yaani familia ile ya kwanza haikututendea vyema lakini uliziba tundu la nyumba yao lakini hawa wametutendea vyema ume ua ng'ombe wao"
Kisha malaika MZEE akajibu"mambo huwa hayapo k**a yadhaniwavyo. Nyumba ile ya kwanza niligundua kuna dhahabu kwenye tundu ndomana nikaziba lile tundu kwa maana hawakututendea vyema
Nyumba hii ya pili imetutendea vyema hivyo malaika wa Mauti alipofika usiku kutaka kumchukua mama mwenye nyumba nilimuelekeza kwa ng'ombe"

Hata Leo MPENDWA usiangalie Yale yanayo kutokea, jua MUNGU haachi kukuwazia mema
Na siku zote njia za Mungu hazichunguziki hata kidogo! Na mawazo yake si mawazo ya mwanadamu! Unachotakiwa kufanya wewe jilaze kwenye mikono yake k**a mtoto mchanga ajilazavyo kwenye mikono ya mama yake...bila kujali chochote kile uone ukuu wa Mungu juu ya maisha yako. .🙏🙏

Zaburi 34:7-9 inasema:
Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.

SASA SOMA HUU UJUMBE ; Ili upate kukusaidia endapo utauelewa, Amen.

Telephone