Bahari ya mapenzi

Bahari ya mapenzi

Partager

16/05/2026

SOMO LA LEO 👇 👇 👇 👇 👇 👇 👇 👇*USIKIMBILIE KUOMBA MPENZI BORA, ANZA KUWA BORA WEWE MWENYEWE*

Watu wengi huomba Mungu awape mke au mume bora, mwenye tabia njema, heshima, upendo na uaminifu. Lakini kabla ya kuomba kupata mtu wa maisha, ni muhimu kwanza kujiuliza:

“Je, mimi mwenyewe ni bora kwa huyo ninayemhitaji?”

Mahusiano mazuri hayajengwi na maombi pekee, bali huanzia kwenye tabia, maadili na maandalizi ya mtu binafsi.

Kabla hujatamani kupata mwenza sahihi, jitahidi kwanza kujibadilisha wewe mwenyewe.

K**a unahitaji mke mwenye heshima, jiulize:

Je, wewe unajiheshimu

Unajua kuthamini mwanamke?

Una maneno mazuri na tabia njema?

Na k**a unatamani kupata mume bora:

Je, wewe una tabia zinazojenga familia?

Una uvumilivu, heshima na uaminifu?

Unaweza kusimama kwenye kweli na upendo?

Mara nyingi tunataka vitu vizuri vitokee maishani mwetu huku sisi wenyewe hatujabadilika.

Ukweli ni kwamba, mabadiliko huanza na mtu binafsi.

Badilisha kwanza fikra zako, tabia zako, mwenendo wako na namna unavyowachukulia wengine.

Mtu wa maisha anayefaa huja pale ambapo nawe umejiandaa kuwa mtu sahihi.

Vijana wengi leo wanahangaika kutafuta mapenzi ya kweli, lakini hawapo tayari kubeba wajibu wa mahusiano yenye afya.

Mahusiano yanahitaji:
Uaminifu

Heshima
Mawasiliano mazuri
Subira
Na hofu ya Mungu
Usikimbilie kuomba upate mtu bora wakati bado hujajitengeneza kuwa bora.

Jifunze, jikubali, jirekebishe na muombe Mungu akupe hekima ya kuwa mtu mwenye thamani kwanza.

Kumbuka: Mwenza bora huvutiwa na mtu aliye bora pia.
✍️ Ramsey Ramazani.

ASANTE KWA UWELEWA WENU.

FAAMU MASWALI 14 MUIMU SANA YA KUMUULIZA MPENZI WAKO. MPAKA AVUTIWE NA WEWE 21/12/2023

FAAMU MASWALI 14 MUIMU SANA YA KUMUULIZA MPENZI WAKO. MPAKA AVUTIWE NA WEWE Bahari ya mapenzi, usikose ku ku comment naku share Chanel yetu ya YouTube

Vous voulez que votre entreprise soit Salon De Beauté la plus cotée à Bukavu ?
Cliquez ici pour réclamer votre Listage Commercial.

Site Web

Adresse

Ramseyramazani37@gmail. Com
Bukavu