RCFI. FM

RCFI. FM

Partager

26/07/2022

DRCONGO: Kivu - Kaskazini/ Maandamano dhidi ya Monusco.

RAÏA WAANDAMANA DHIDI YA UMOJA WA MATAÏFA( UN ) NA JESHI LA MONUSCO/ by Madiba Mahoye.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Watu watano wameuawa baada ya kupigwa risasi wakati wengine wapatao 50 wamejeruhiwa wakati wa maandamano ya kupinga uwepo wa vikosi vya walinda usalama wa umoja wa mataïfa katika eneo la Goma, mashariki mwa Jamuhuri ya Kifemokrasia ya Kongo, imethibitisha taarifa yake msemaji wa serikali ya Patrick Muyaya.

Jumatatu ya wiki hii, mamia ya waandamanaji wamefunga baadhi ya barabara mjini Goma kabla kuvamia makao makuu ya walinda amani wa umoja wa mataïfa.

Inasadikiwa kuwa watu hao wenye hasira walivunja vio na kuiba vitu vya thamani kutoka ufisi hizo.

Wafanya kazi wa umoja wa mataïfa wameondolewa katika majengo hayo kwa kutumia ndege za helikopta wakati polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

Machafuko hayo yameendelea kushuhudiwa mapema asubuhi jumanne hii tariki 26 Jully 2022 nje ya makao ya UN.

Ujumbe wa umoja wa mataïfa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unao tambuliwa k**a MONUSCO , ni moja wapo ya vikosi vikubwa vya walinda amani duniani .

Kwa muda sasa raïa wa DRC wamekuwa wakiwatuhumu walinda amani hao MONUSCO wamekua wakizembea kazini wakati wamauaji dhidi ya raïa yakitekelezwa na makundi ya wanamgambo.

Zaïdi ya makundi 120 ya wanamgambo wenyekumiliki silaha yametajwa yanaendeleza operesheni nchini ,huku milioni wakilazimika kuyahama makazi yao na kutorokea ambapo kunausalama.

26/08/2020

*BURUNDI NA RWANDA ZAANZA MAZUNGUMZO YA KUREJESHA MAHUSIANO* .

Maafisa wa usalama wa Burundi na Rwanda wameanza mazungumzo ya kurejesha uhusiano, ikiwa ni mara ya kwanza mazungumzo kufanyika ndani ya kipindi cha miaka mitano wakati nchi hizo zikiwa kwenye mkwamo wa kisiasa.

Mazungumzo hayo yaliyosimamiwa na Idara ya Usalama ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) yalifanyika kwenye mpaka wa Nemba ulioko mashariki mwa Rwanda kwenye eneo ambalo halimilikiwi na Rwanda wala Burundi.

Ulikuwa mkutano ulioukutanisha ujumbe mzito kutoka kila upande huku maafisa wa idara ya ujasusi kutoka pande hizo tatu - Rwanda, Burundi na ICGLR - ukitangaza mtazamo wake juu ya mkutano huo wa kwanza ndani ya kipindi cha miaka mitano tokea nchi mbili hizo zilipoingia kwenye mzozo wa kidiplomasia.

Mkuu wa ujumbe wa Rwanda, Brigedia Jenerali Vincent Nyakarundi, alisema nchi yake "inathamini nafasi ya ICGLR katika kutatua mizozo, na kujituma kwa wajumbe wake ambao hufanya kila jitihada za kurejesha usalama kwenye eneo hili la maziwa makuu na siku zote kupambana ili hali ya ujirani mwema na kuaminiana kwenye mataifa hayo iendelee kuwepo."

"Hii ndiyo sababu kuu yetu sote kukutana hapa hii leo na namini baada ya mkutano huu, wote tutakuwa tumekwishatambua chanzo cha ukosefu wa amani unaosababishwa na makundi yenye silaha ya CRND na FNL yanayoisumbua Rwanda kupitia msitu wa Kibira upande wa Burundi.'' Alisema Nyakarundi, ambaye pia ni mkuu wa idara ya ujasusi kwenye jeshi la Rwanda.

*Burundi yataka ushirikiano urudi*

Kwa upande wake, mkuu wa ujumbe wa Burundi, Kanali Ernest Musaba, alisema hali mbaya iliyopo ilikuwa ikichochewa pia na hali ya usalama kwenye eneo la mashariki mwa DRC, hususan katika mpaka unaozitenganisha nchi za Rwanda na Burundi, ambayo si nzuri.

*Rais Paul Kagame wa Rwanda*

"Mkutano huu kwa hiyo ni fursa nzuri kwetu sote kuzungumza kwa uwazi juu ya sababu zinazochangia usalama huo mdogo na tunaamini kuwa hakutakuwepo na upendeleo wowote, ili ukweli uwe

13/08/2020

*WANAMGAMBO WENYE MFUNGAMANO NA DAESH WAMETEKA BANDARI MUHIMU NCHINI MSUMBIJI.*

Vyombo vya usalama nchini Msumbiji vimetangaza kuwa, wapiganaji wa kundi lenye mfungamano na kundi la kigaidi la Daesh wameiteka na kuidhibiti bandari moja muhimu kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi jana walifanikiwa kudhibiti bandari muhimu yenye utajiri wa gesi katika mji wa Mocimboa da Praia uliopo kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wanamgambo hao ambao wanajiita Ahlu Sunnah Wa-Jamaa wamefanikiwa kuidhibiti bandari hiyo yenye utajiri baada ya mapigano na mashambuluo ya wiki katikaa baina yao na vikosi vya serikali.

Wakati huo huo vikosi vya ulinzi na usalama vya Msumbiji (FDS) vimetangaza kuwa, vimewaua magaidi 59 katika wikki za hivi karibuni katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado kufuatia operesheni za vikosi hivyo dhidi ya wanamgambo wa Ahlu Sunnah Wa-Jamaa.

Uasi wa wanamgambo nchini Msumbiji umeibuka na kuwa vita vya wazi katika miaka ya ya hivi karibuni, huku kukiwa na ripoti za mauaji, watu kukatwa vichwa na kutekwa kwa miji miwili katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado.

Vijiji vya mkoa huo wa Cabo Delgado ulioko kaskazini mwa Msumbiji tangu mwezi Oktoba mwaka 2017 vimekuwa vikishuhudia mashambulizi ya umwagaji damu ya wanachama wa kundi linalojiita Ahlu Sunna Wal Jamaa, ambao wakazi wa maeneo hayo wanawatambua kwa jina la al-Shaabab.

Kundi hilo la kigaidi limekuwa likifanya mashambulizi hayo licha ya serikali ya Msumbiji kutuma wanajeshi na polisi katika maeneo hayo ambayo yapo katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania.

Vous voulez que votre entreprise soit Entreprise De Médias la plus cotée à Baraka ?
Cliquez ici pour réclamer votre Listage Commercial.

Téléphone

Site Web

Adresse

La Radio Communautaire Fizi FM, Est Situé à L'est De La République Démocratique Du Congo Au Sud Est De La Province Du Sud Kivu, Sur Le Litoral Du Lac Tanganyika
Baraka